Hivi wapo waliochomoka kimaisha kwa kutegemea mshahara wa chini ya million 1 tu?

dimaa

JF-Expert Member
Jul 30, 2016
4,143
5,610
Habari waungwana,
Kwangu naona kama haiwezekeni kutegemea mshahara pekee wakunifanya nijikwamue kimaisha, hivyo imenilazimu niingie kwenye biashara kwa haraka sana.

Sikuona kama nitapiga hatua zaidi kwa kutegemea mshahara pekee, na ukiwa na majukumu makubwa ya wanaokutegemea.

By
Dimaa.
 
Njaa imeteka watu sana, lakini tusikubali akili zitekwe
 
hakuna tajiri alieajiriwa.... labda uwe vyeo vya juu sana vya kufanya decision making kama chenge enz zake... hapo utakuwa tajiri tu...

ila hutaweza kuutumia utajiri wako nchini kwako maana utaulizwa maswali umezipataje na kuporwa mali zako na serikali...
 
Ukiwa kwenye uhalisia yaani umeajiriwa na una wanaokutegemea pokea laki tisa yako kwamwezi kisha wapeleke shule , matibabu, chakula , mavazi n.k mwenyewe utakuwa mwalimu wako mwenyewe kuwa inahitajika kujiongeza ,
 
Habari waungwana, kwangu naona kama haiwezekeni kutegemea mshahara pekee wakunifanya nijikwamue kimaisha, hivyo imenilazimu niingie kwenye biashara kwa haraka sana.

Sikuona kama nitapiga hatua zaidi kwa kutegemea mshahara pekee, na ukiwa namajukumu makubwa ya wanaokutegemea.

By

Dimaa.
Utachomokaje bila katiba Mpya?
 
Mimi binafsi kipato changu kwa mwezi hakizidi laki 7 lakini kwa sasa namiliki nyumba ya kisasa na mwisho wa mwaka huu naagiza gari kwa ajili ya usafirishaji..kila kitu ni mipango na malengo...jitathimin na jielewe kidogo kina maana kuliko kikubwa
 
Back
Top Bottom