Hivi Wanawake kama Huyu Wapo Humu JF?

RRONDO

JF-Expert Member
Jan 3, 2010
51,719
107,835
Juzi nilipata kibarua cha kukata majani huko Goba. Nilipewa pande hili na jamaa yangu mmoja hivi. Kwahio nilikuwa naenda kwenye kibarua huku boss simjui. Kufika eneo la kazi mjengo nilioukuta si mchezo, hapo kwenye garden pembeni zimepaki ndinga tatu kwa uzoefu wangu ya bei ya chini ni 28m hivi!

Baada ya kufika hapo nikaambiwa nimsubiri boss, akatokea dada mmoja mzuri sana nikaambiwa ndio boss mwenyewe niongee nae. Basi nikaongea na yule dada tukakubaliana ujira wangu nikaendelea na kazi huku najiuliza huyu binti mdogo hivi silaha hizi anazomiliki kwa zama hizi kazipata wapi?

Kama kawaida yangu nikikutana na mtu yuko vizuri huwa sijivungi nauliza siri ya mafanikio, dada huyu pamoja na mafanikio yake hana nyodo kabisa, tuliongea mengi na mwisho nikajua ni boss fulani katika moja ya kampuni kubwa Tanzania. Je nyinyi mnaotuponda humu sisi masikini tusio na magari wala nyumba ndio mko level za huyu dada nini? Je wanawake kama huyu dada(young, successful and humble) mpo humu?
 
searching...................................0%......................... still searching ...............0%.................. again and again ...................0%.................endelea kusubiri bado ina search
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom