Hivi wanaume wenye watoto, hasa wa kike mnaweza fanya hili.?

Carleen

JF-Expert Member
Nov 6, 2018
7,503
25,117
Hi guys, Hope mko na weekend poa...!!

Naomba niulize hili swali hasa kwa wababa wenye wako na watoto wa kike..!!

Nina rafiki yangu mmoja mrembo, niliwahi fanya naye kazi pahala flani miaka flani ya nyuma kidogo, alikuwa na mdogo wake wa kike wote nilifanikiwa kuwafahamu sababu tulifanya kazi sehemu moja.!

Huyo binti na mdogowe walikuwa wanaishi nyumbani kwao, baada ya muda kupita mdogo wake akapata ujauzito wa mwanaume ambaye alikuwa anatambulika hapo nyumbani kwao kama mchumba wake, bahati nzuri akafanikiwa kupata watoto mapacha wa kiume, na ukimtazama huwezi mdhania alikua na kamwili kadooncho hasa, hao mapacha vile aliweza wabeba doh' muwe mnatuheshimu tu siye kinamama, tukampa MUNGU Utukufu maisha yakaendelea,

Wakafanya mambo official akawa amehamia kwa mumewe mkoa mwingine na kumuacha dada yake hapo nyumbani, baada ya muda dada mtu naye akaamua akapange ajitegemee, hivyo akaruhusiwa akawa anajitegemea.!!

Mie nikawa nimeacha kazi hapo nikawa nimeendelea na maisha yangu mengine huko kwa dunia, Unluckily, muda mrefu haukupita kampuni nayo ikawa imepunguza wafanyakazi akiwemo na rafiki yangu huyo, ugumu ukaanzia hapo akaona njia bora ni kurudisha mpira kwa kipa, hivyo akawa anaendelea kuhangaika na kutafuta jinsi gani aweze kusimama tena huku akiwepo hapo nyumbani akiamini ni pahala salaama,

Kilichonishtua, anakuja kunitafuta ananambia Baba yake kamfukuza nyumbani, I was like whaat? Kwanini afanye hivyo..? Baba kamuambia atoke nyumbani akaolewe, nikabaki nashangaa, nikamuuliza sasa mama ukaolewe na nani? Au umfuate mwanaume umuambie nioe?? Ananambia hapa hata mwenyewe sielewi, nimechanganyikiwa, nikauliza upo wapi hivi sasa? Akajibu kwa dada yangu'.. Kazi je? Akasema kuna kazi ameipata ila ndo kaanza hana hata 1 week,

Nikamuambia a big No, hakuna baba anayeweza mfukuza binti yake nyumbani tena bila sababu za msingi, Nikamuambia kuna kitu umemkera mzee wa watu, akasema hapana, sababu binti aliita kikao na nduguze wakiwemo akimtaka mzee japo wazungumze ajue shida ni nini? Mzee kagoma kufanya hicho kikao anachotaka yeye ni binti akaolewe full stop..!

Binti ana miaka 26 hivi sasa, na ana kamwili kadogo waweza mrudisha hata shule ukijua ni katoto, siyo kama siye wakubwa kama nyumba, Mpaka nikawaza kwa sauti ingekuwa ndo mie mbona ningetimuliwa toka nipo msingi (joking)..!! 😂

NB; siyo mjamzito wala..!!

Nilitaka niwaulize wazazi wa jinsia ya kiume mliopo humu ndani, hivi kuna uwezekano ukamfukuza nyumbani binti yako wa kumzaa ukitaka kwa nguvu akaolewe??
 
Nina watoto wa kike watatu ingawa hawajafikia umri wa kukitegemea ila hata ikifikia umri huo hawatatoka nyumbani kwangu mpaka watakapobahatika kupata ubavu wao wa pili.

Vinginevyo watazeeka wakiwa chini ya himaya yangu, mtoto wa kike ndiye mlezi halisi wa nyumbani kwa wazazi wake hivyo ukikosea misingi ya kumlea atakuwa mzigo mpaka anakufa.

Mzee mwenzetu hapo juu nadhani anahisi binti yake anachagua wanaume huku akiwa bado anagegedwa kama kawaida hivyo anaona bora binti akajisimamie.
 
Nina watoto wa kike watatu ingawa hawajafikia umri wa kukitegemea ila hata ikifikia umri huo hawatatoka nyumbani kwangu mpaka watakapobahatika kupata ubavu wao wa pili.

Vinginevyo watazeeka wakiwa chini ya himaya yangu , mtoto wa kike ndiye mlezi halisi wa nyumbani kwa wazazi wake hivyo ukikosea misingi ya kumlea atakuwa mzigo mpaka anakufa .

Mzee mwenzetu hapo juu nadhani anahisi binti yake anachagua wanaume huku akiwa bado anagegedwa kama kawaida hivyo anaona bora binti akajisimamie.
How super daddy you are, Hongera Mkuu.!!
 
Kama mwanamme mmoja kaenda Mirember huwezi tuuliza ambao hatuko Mirember kwa Nini kaenda, common sense kwa kweli umekosa.... Mimi watoto wangu hata wangekaa milele nyumbani Haina shida, nafikiri Kuna kitu kawaficha wote
 
Huyo mwanaume aliyefukuza binti yake ni shetani kabisa.

Katika dunia ya leo,karne hii ya 21,unaanzaje kumfukuza mtoto wako tena binti nyumbani? Mimi siwezi,hata akipata ujazito mara 100,na hata awe na miaka 50,siwezi kufukuza binti yangu nyumbani.

Naweza kumtimua kijana wangu wa kiume(kwa kumpa msaada lakini)akatafute maisha kama wanaume wengine,lakini kwa binti hapana.

Kwa uzoefu wangu,mtoto wa kike ni hazina,ni vigumu kumsahau mzazi wake,hata akiwa na maisha magumu huko kwenye ndoa yake, hawezi kumsahau baba yake,na ndugu zake wengine. Mtoto wa kiume, akishakuwa na maisha yake, tena awe amepata mke kutoka ukoo wa (delila wa samson!)huyo kukutosa ni rahisi sana.
 
siwezi Fanya ujinga huo Kama mkuu alivyosema hapo juu mtoto wa kike ni mlezi halisi wa nyumbani halafu ni damu yangu naanzaje hyo roho ya kinyama


Ila ningefurahi mungu anijalie mtoto wa kike au hata mapacha ya kike wawili walibwende wangu katika uzao wangu

Inshallah Allah atafanikisha. Ameen
Ameen Mkuu,
MUNGU akayajibu maombi yako!!
 
Kama mwanamme mmoja kaenda Mirember huwezi tuuliza ambao hatuko Mirember kwa Nini kaenda, common sense kwa kweli umekosa.... Mimi watoto wangu hata wangekaa milele nyumbani Haina shida, nafikiri Kuna kitu kawaficha wote
Sijajua ni kipi hasa kaficha though huwa hanifichi chochote.!!
 
Back
Top Bottom