Hivi, wanaume mnaposema kuwa wanawake wa siku hizi tunapenda usawa huwa mnamaanisha nini?

Habari za usiku huu wana JF?

Mie wala siyo mwingi wa habari ila nilitaka tu kuwauliza ninyi kaka zetu hili swali kama kichwa cha mada kinavyojieleza hapo juu.

Swali: Hivi, wanaume mnaposema kuwa wanawake wa siku hizi tunapenda usawa huwa mnamaanisha usawa kivipi yaani kwenye mambo yepi haswa?

Swali la nyongeza: Je, mnataka wanawake tusifanye makosa ila wanaume mfanye makosa halafu wanawake tukae kimya tusiwaambie na wala tusiwafanye chochote au mnatakaje?

Naombeni majibu yenu tafadhali na hata wanawake wenzangu pia mnaweza kujibu chochote mnachojua kuhusiana na hayo maswali maana mimi sina majibu kabisa.
Hapa tunamaanisha wanawake wanatongoza na kuwagegeda wanaume
 
Nahisi nipo nje ya mada kidogo lakini sometimes wanawake tunajichanganya

Tunataka haki sawa kwa wote wakati huo huo tuna ile kauli mbiu yetu eti wanawake tukiwezeshwa tunaweza...SMH!

Kwanini tuhitaji kuwezeshwa wakati tuko na mikono na miguu miwili mixer ubongo kama wanaume
Tatizo ni mgawanyo wa majukumu wanaume hawataki kufanya majukumu yetu ila wanataka wanawake tufanye majukumu yao na matokeo yake wanawake tunajikuta tunafanya majukumu mengi kuliko wanaume something which is not fair I think.
 
Mimi siyo mjuzi ila ninaeleza kile ninacho elewa mimi.

Tunapoongelea usawa tunamaanisha tuondoe ule mnaouita mfumo dume kwamba binadamu wote ni sawa kitu ambacho si kweli. Mnaouita mfumo dume ni ule unaom favor mwanaume zaidi katika nafasi mbalimbali. Lakini kiukweli huo usawa mnaoulilia hauwezi kuja kutokea kwa sababu hata mkipewa nafasi bado hamtaweza kufanya vitu ambavyo mwanaume anafanya.

Mwanaume kaumbiwa roho ya ukakamavu, uvumilivu, na kujitoa muhanga katika hatari wakati huo mwanamke ana hali ya unyonge, kulia lia kila kitu na mwepesi kukata tamaa. Sasa mtu kama huyu anataka usawa na mwanaume.

Usawa tunaoulalamikia sisi ni ule wa kuingilia mipaka yetu achana hiyo uliyoongelea hapo.
Nimekuelewa mkuu lakini unafikiri ni nini chanzo cha wanawake kutaka usawa na kutaka kuingilia mipaka ya wanaume?
 
Tatizo ni mgawanyo wa majukumu wanaume hawataki kufanya majukumu yetu ila wanataka wanawake tufanye majukumu yao na matokeo yake wanawake tunajikuta tunafanya majukumu mengi kuliko wanaume something which is not fair I think.

Wanataka tufanye majukumu yao kama yapi?

Mie nachoona kiko fair ni kila mtu haijalishi ni mwanaume ama mwanamke kufanya anachoweza kufanya ambacho kiko ndani ya uwezo wake....sio eti kusubiri ooh hiki kitu anatakiwa afanye mwanamke ama kile afanye mwanaume
 
Kwenye suala la pesa mishipa inawatoka hatari, utaitwa kila majina. Ila sio kwenye mambo mengine.
ndo hapo sasa nataka leo watuweke sawa hapa ili tuelewe wanamaanisha usawa upi tunaoutaka wakati kwenye kutafuta pesa wao ndo wanataka usawa?
 
Hapa tunamaanisha wanawake wanatongoza na kuwagegeda wanaume
You aren't serious are you? Halafu kwenye kutongoza mbona wanaume siku hizi mnatulazimisha tuwatongoze? Hamuoni kama hata hapo napo nyie ndo mnaotaka usawa?
 
Mimi ninahisi uwezo aliopewa mwanamke Ni mkubwa Sana kulinganisha na mwanaume. Mwanamke ndiye mwenye uwezo wa kuuhifadhi uhai wa binadamu kwa miezi 9 na pia kuutunza kwa miaka mingi zaidi. Mwanamke ni safe keeper wa jamii, mwanamke Ni chombo Cha manung'uniko ya dunia hii kwa nafasi Kama mke na Kama mama. Pepo ya dunia hii ipo kwenye miguu ya mwanamke

Huwa nasikitika nikiona mwanamke akijaribu kuwa Kama mwanaume ili ajihisi superior. MWANAMKE YOYOTE ANAYETAFUTA USAWA NA MWANAUME HUPOTEZA NGUVU YAKE KAMA MWANAMKE.
 
Habari za usiku huu wana JF?

Mie wala siyo mwingi wa habari ila nilitaka tu kuwauliza ninyi kaka zetu hili swali kama kichwa cha mada kinavyojieleza hapo juu.

Swali: Hivi, wanaume mnaposema kuwa wanawake wa siku hizi tunapenda usawa huwa mnamaanisha usawa kivipi yaani kwenye mambo yepi haswa?

Swali la nyongeza: Je, mnataka wanawake tusifanye makosa ila wanaume mfanye makosa halafu wanawake tukae kimya tusiwaambie na wala tusiwafanye chochote au mnatakaje?

Naombeni majibu yenu tafadhali na hata wanawake wenzangu pia mnaweza kujibu chochote mnachojua kuhusiana na hayo maswali maana mimi sina majibu kabisa.
mfano wewe nikuulize ukinijibu langu nitakupa lako ...mwanamke anaposema haki sawa kwa wote anakua anamaanishanini? toa mfano wa kitu ambacho mwanaume anapata kwa kuwa ni mwanaume na mwanamke ananyimw kwa kuwa ni mwanamke...?au mwanamke anaposema haki sawa kwa wote anakua ana lenga wapi hasa ni haki zipi ?
 
Habari za usiku huu wana JF?

Mie wala siyo mwingi wa habari ila nilitaka tu kuwauliza ninyi kaka zetu hili swali kama kichwa cha mada kinavyojieleza hapo juu.

Swali: Hivi, wanaume mnaposema kuwa wanawake wa siku hizi tunapenda usawa huwa mnamaanisha usawa kivipi yaani kwenye mambo yepi haswa?

Swali la nyongeza: Je, mnataka wanawake tusifanye makosa ila wanaume mfanye makosa halafu wanawake tukae kimya tusiwaambie na wala tusiwafanye chochote au mnatakaje?

Naombeni majibu yenu tafadhali na hata wanawake wenzangu pia mnaweza kujibu chochote mnachojua kuhusiana na hayo maswali maana mimi sina majibu kabisa.
Feminine should remain feminine same applied to masculine should remain masculine.
Not otherwise!
 
Wanataka tufanye majukumu yao kama yapi?

Mie nachoona kiko fair ni kila mtu haijalishi ni mwanaume ama mwanamke kufanya anachoweza kufanya ambacho kiko ndani ya uwezo wake....sio eti kusubiri ooh hiki kitu anatakiwa afanye mwanamke ama kile afanye mwanaume
Ni sawa ila mimi naona kama mara nyingi wanawake ndo tunaweza kufanya majukumu yote ambayo yapo ndani ya uwezo wetu ila wanaume kuna baadhi ya majukumu hawawezi kufanya hata kama yapo ndani ya uwezo wao eti kwa sababu tu kwenye jamii yamezoeleka kuwa ni majukumu ya kike na inaonekana ni aibu kwa mwanaume kuyafanya hii imekaaje?
 
Habari za usiku huu wana JF?

Mie wala siyo mwingi wa habari ila nilitaka tu kuwauliza ninyi kaka zetu hili swali kama kichwa cha mada kinavyojieleza hapo juu.

Swali: Hivi, wanaume mnaposema kuwa wanawake wa siku hizi tunapenda usawa huwa mnamaanisha usawa kivipi yaani kwenye mambo yepi haswa?

Swali la nyongeza: Je, mnataka wanawake tusifanye makosa ila wanaume mfanye makosa halafu wanawake tukae kimya tusiwaambie na wala tusiwafanye chochote au mnatakaje?

Naombeni majibu yenu tafadhali na hata wanawake wenzangu pia mnaweza kujibu chochote mnachojua kuhusiana na hayo maswali maana mimi sina majibu kabisa.
Kwani SLOGAN YA HAKI SAWA ni ya wanaume? Beijing mlienda kufanya nini kwenye ule mkutano?

Sisi tunaitaja tu slogan yenu
 
Mimi ninahisi uwezo aliopewa mwanamke Ni mkubwa Sana kulinganisha na mwanaume. Mwanamke ndiye mwenye uwezo wa kuuhifadhi uhai wa binadamu kwa miezi 9 na pia kuutunza kwa miaka mingi zaidi. Mwanamke ni safe keeper wa jamii, mwanamke Ni chombo Cha manung'uniko ya dunia hii kwa nafasi Kama mke na Kama mama. Pepo ya dunia hii ipo kwenye miguu ya mwanamke

Huwa nasikitika nikiona mwanamke akijaribu kuwa Kama mwanaume ili ajihisi superior. MWANAMKE YOYOTE ANAYETAFUTA USAWA NA MWANAUME HUPOTEZA NGUVU YAKE KAMA MWANAMKE.
upo sawa mkuu ila hakuna cha uwezo mkubwa wa mwanamke wala nini... ndio wajibu wake na kazi aliyoumbwa kuja hapa duniani kuifanya ndio maana ana uterus, ovary na uwezo wa kukaa na mtoto huyo pia kapewa ingelikua na sisi wanaume tunavyo hapo ndio wangekua na la kusema....kwa mfano wao pia hawaezi kupata hiko kiumbe bila ya kuwepo na mwanaume...mungu aliamua kubalance na kumpa kila mtu majukumu yake na kila mtu afanye yake kwa upande wake
 
Namaanisha kuna uwezekano hayo malalamishi yetu kuhusu wanawake kupenda usawa yapo humu tu kwenye JF na si huku mitaani, yawezekana huku mtaani mambo yanaenda pasina ulalamishi

Yaani there is huge difference between real life and the internet ( Mwanamke anafanya zaidi kwenye jamii kuliko mwanamme).
Uko sahihi kabisa mkuu hata mimi kuna wakati huwa nawaza hivyo kuwa wanaume wanaujua sana ukweli ila basi tu wanapenda kujilalamisha humu mitandaoni
 
Back
Top Bottom