Its Tesha
Senior Member
- Oct 6, 2025
- 168
- 604
Viongozi wa jamii ya Kimaasai nchini Tanzania, maarufu kama Malaigwanani, wametoa tamko rasmi la kuunga mkono kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025, huku wakipinga vikali wito wa maandamano unaosambazwa katika maeneo mbalimbali nchini.
Tamko hilo limetolewa katika eneo la Donyomorwak, Wilaya ya Siha, Mkoa wa Kilimanjaro, wakati wa mkutano wao wa kawaida wa Orkiama, ambapo Katibu wa Malaigwanani Tanzania, Bw. Jeremia Laizer, akisoma kwa niaba ya viongozi hao, amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kupiga kura na kuchagua viongozi wanaowataka kwa amani.
Ameongeza kuwa jamii ya Kimasai itaendelea kumuunga mkono kiongozi mwenye kuweka mbele maslahi ya wananchi na kulinda amani ya taifa, akisisitiza kuwa utulivu ni msingi wa maendeleo.
Mgeni rasmi katika mkutano huo, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Namelok Sokoine, amewapongeza Malaigwanani kwa msimamo wao huo na kwa kuridhika kwao na utekelezaji wa miradi ya maendeleo chini ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Aidha, baadhi ya viongozi wa jamii hiyo wameahidi kuwa mabalozi wa amani katika maeneo yao wakati wa kipindi cha uchaguzi, wakisisitiza kuwa maandamano yasiyofuata taratibu yamekuwa chanzo cha uvunjifu wa amani na madhara makubwa kwa wanawake, watoto na wazee.