Hivi walimu wa A level( Form five na six ) wana sifa gani?

Askari Muoga

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
6,113
4,655
Nimesoma A level ila bado sijui sifa za kuwa mwalimu wa A level

1. Kiwango cha Elimu yao
2. Je wanapatikanaje yani utaratibu wa ajira zao

My take
Walimu wengi wa A level uwezo wao wa kufundisha ni mdogo. Naombeni mnifungue nijue sifa za kuwa mwalimu wa A level
 
Sifa KUU ya kuwa mwalimu WA Alevel ni degree Huyu mwenye shahada anauwezo WA kufundisha kuanzia kidato cha tatu mpaka kidato cha sita
 
Mkuu pole sana kwa kufundishwa na walimu wenye uwezo mdogo na ni bahati mbaya!

Mwalimu mwenye degree uwezo wake ni mkubwa na unakidhi matakwa, tafadhari usigeneralize kwa kupitia hao walimu wapo!

Pia mada yako imelenga tu kuwalinganisha walimu wa shahada vs stashahad!
stashahada mtatimuliwa vumbi sana, nenda kasome utoke huko uenjoy uelewa na raha za kuwa na shahada!
 
Nimesoma A level ila bado sijui sifa za kuwa mwalimu wa A level

1. Kiwango cha Elimu yao
2. Je wanapatikanaje yani utaratibu wa ajira zao

My take
Walimu wengi wa A level uwezo wao wa kufundisha ni mdogo. Naombeni mnifungue nijue sifa za kuwa mwalimu wa A level
Sifa za kuwa Mwalimu wa Advanced Level ni kuhitimu Elimu ya Juu yaani Shahada. Hivyo ukishapata Degree, unaweza kuajiriwa kufundisha Kidato cha 5 na 6. Lakini pia unaweza kufundisha O'Level.

Utaratibu wa Uajiri, miaka iliyopita Serikali ilikua inawaajiri wahitimu wote katika shule zake nchini (bila kuomba) lakini kwa miaka miwili hivi kuanzia wahitimu wa 2015, serikali haijaweza kuwaajiri isipokuwa imewataka walimu wa Sayansi kutuma vyeti vyao vihakikiwe na baadae watapangiwa katika vituo vya kazi kitu ambacho mpaka sasa hakijafanyika.
 
Uhalisia ni:
1.Astashada -Primary
2.Stashahada- O'level kidato cha kwanza na cha pili.
3.Shahada-O'level kidato cha tatu na cha NNE.
4.Uzamili-Advanced level
5.Uzamivu- Vyuo na vyuo vikuu.
Lakini kwa sababu ya upungufu was walimu has a sayansi unaweza kufundishwa A'level na diploma holder. Usibeze sana hata Mimi nilifundishwa primary na primary mwenzangu(Mwl was UPE) lakini nilifaulu na sasa Niko mbali.
Kaza buti utafaulu tu
 
Sasa mbona huku vyuoni kuna tutors wengi ambao ni degree holders tu??? Advance shule niliyosoma mwlm aliyekuwa na masters ni mmoja tu wengine wote walikuwa degree holders.
 
Sasa mbona huku vyuoni kuna tutors wengi ambao ni degree holders tu??? Advance shule niliyosoma mwlm aliyekuwa na masters ni mmoja tu wengine wote walikuwa degree holders.
Hilo usishangae. Assistant tutor vyuoni wengi ni walofaulu kwa GPA kubwa3.8 and above kulingana na chuo. Wengine in ndugu wa ...... Hawa wanaandaliwa kuwa maprofesa baadaye na wanapewa muda maalum wa kuwa na degree hiyo. Wanasomeshwa na vyuo hivyo.
Usishangae ukiwa na GPA ya 4.8 bado usiwe tutor. Kuna vigezo Vingi vinavyozingatiwa.
 
Back
Top Bottom