Hivi wabunge wa ccm kuzomea huo ni ustaarabu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi wabunge wa ccm kuzomea huo ni ustaarabu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kibunda, Mar 6, 2011.

 1. k

  kibunda JF-Expert Member

  #1
  Mar 6, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 403
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Binafsi nimekuwa najiuli, hivi kwa nini serikali, na wachambuzi wengi walikuwa kinyume na hatua ya wabunge wa cdm kususia hotuba ya rais pale bungeni. Tena, hata hatua yao ya kutoka wakati wa marekebisho ya kifisadi ya kanuni za bunge. Lakini hakuna mchambuzi yoyote aliyekemea kitendo cha wabunge wa ccm kupiga kelele na kuwazomea wenzao wa cdm. Hata kama wabunge wa chadema hawakufanya ustarabu na kwamba walikosa uungwana kama wanavyosema ccm na wachambuzi wengine wenye mawazo kama wao, swali langu, je wao walikuwa wastaarabu na wavumilivu kwa kupiga kelele na kuwazomea watu wanaotoka kimya kimya tena kwa heshima zote.

  Lakini kilichoniacha hoi zaidi ni pale na rais kukosa subira na kuanza kupiga vijembe na kujigamba mwisho wa hotuba yake ya pale bungeni. Hata hivyo, majigambo hayo hatukuyaona kwenye hotuba ya mwisho wa mwezi. Aliposema wazi kabisa kuwa bila ya viongozi wa cdm kutoa ushirikiano yeye na serikali hawawezi. Hili wana jf mnalionaje?
   
 2. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #2
  Mar 6, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,086
  Likes Received: 4,032
  Trophy Points: 280
  soo ni wakizomewa wao na wananchi wanawika, angalia walivyokemea kitendo cha watu kumzomea Mkapa kipindi kile...
   
 3. k

  kibunda JF-Expert Member

  #3
  Mar 6, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 403
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mimi nilishangaa sana wachambuzi kutoliona hili. Nimeona leo hata lile sakata la arusha kwenye hii documetary wale madiwani wa ccm walishangilia na kuzomea pale lema alipokamatwa tena kinyume na sheria. Kwani mbunge hawezi kukamatwa bila kibali maalum cha rais ama speak wa bunge. Lakini lema amekuwa akikamatwa na madiwani wa ccm wanazomea.
   
 4. T

  Tiote Senior Member

  #4
  Mar 6, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 139
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiyo ndiyo demokrasia ya mabunge yetu yanayofuata mfumo wa vyama vingi. Hata westminster haya huwa yanatokea kila leo.
   
Loading...