Hivi waarabu wanaweza kuiangusha Ulaya katika biashara ya soka duniani?

crankshaft

JF-Expert Member
Jun 12, 2019
1,410
3,376
Ulaya imejisimika kama mfalme wa biashara ya soka duniani kana kwamba wachezaji wote huona kufika huko ndio mafanikio ya soka duniani.

Wana kipi special hawa jamaa?

Nini kinawapa haki ya kutoa mchezaji anayeitwa bora zaidi duniani kutoka ligi zao?

Nini kinawapa haki ya kuzi rank timu na ligi zao kuwa ndio bora zaidi duniani?

ronaldo alipotua saudi arabia walimtia majungu sana kwenye media zao.

Why not asia or american teams?

Kwa jeuri ya pesa waliyonayo waarabu kwa sasa wanaweza kumchukua mchezaji yoyote pale ulaya. Hivi kwa hii trend iliyopo ya kunyakua mastaa wakubwa wa Ulaya, kuna siku wataweza kuondoa utawala wa Ulaya katika soka la dunia?
 
usiwape sifa waarab kwa kununua gazeti jioni kwa 5000 wakati wenzie walilinunua asubuhi likiwa bado la moto kwa 500 tu
lakini wanachokifanya inaonesha kuwa wanaweza kumpata yoyote wanaoweza kumpata wazungu. Hivyo kutishia maslahi yao mbeleni.
 
Kama Ulaya wameshindwa kuwazidi Brazil na Argentina...basi waraabu kuwazidi Ulaya haiwezekani
 
km hilo lipo basi linawea kutokea miaka 200 ijao...kwa sasa wazungu washaset standar zao na kila siku wanaumiza vichwa kuboresha soka la ulaya yao
 
Kama Ulaya wameshindwa kuwazidi Brazil na Argentina...basi waraabu kuwazidi Ulaya haiwezekani

kinacho matter hapa ni influence ya pesa kuwang'oa mastaa wakubwa ulaya. Wachezaji bora wa america kusini, ulaya huwa ni kama destination kwao kutokana na pesa. Lakini sasa waarabu nao wameanza kumwaga pesa kuliko hata ulaya na wanazo nyingi. Hii maana yake hata hawa wachezaji bora watalazimika kukimbia ulaya kwenda uarabuni.
 
Ulaya imejisimika kama mfalme wa biashara ya soka duniani kana kwamba wachezaji wote huona kufika huko ndio mafanikio ya soka duniani.

Wana kipi special hawa jamaa?

Nini kinawapa haki ya kutoa mchezaji anayeitwa bora zaidi duniani kutoka ligi zao?

Nini kinawapa haki ya kuzi rank timu na ligi zao kuwa ndio bora zaidi duniani?

ronaldo alipotua saudi arabia walimtia majungu sana kwenye media zao.

Why not asia or american teams?

Kwa jeuri ya pesa waliyonayo waarabu kwa sasa wanaweza kumchukua mchezaji yoyote pale ulaya. Hivi kwa hii trend iliyopo ya kunyakua mastaa wakubwa wa Ulaya, kuna siku wataweza kuondoa utawala wa Ulaya katika soka la dunia?
Kununua wachezaji waliofikisha age ya kucheza bonanza pale leaders ndiyo unaita jeuri?
 
kinacho matter hapa ni influence ya pesa kuwang'oa mastaa wakubwa ulaya. Wachezaji bora wa america kusini, ulaya huwa ni kama destination kwao kutokana na pesa. Lakini sasa waarabu nao wameanza kumwaga pesa kuliko hata ulaya na wanazo nyingi. Hii maana yake hata hawa wachezaji bora watalazimika kukimbia ulaya kwenda uarabuni.
Hakuna Star atakayeenda kucheza soka uarabuni akiwa na umri wa miaka 20 hata wamlipe nini.
Wewe unafikiri wao hawawataki akina na akina Antoine Griezmann, Mo Salah, Erling Haaland, Mmbappe n.? Wanawataka sana sema wanasubiri giza liingie ndiyo wakawaombe.
Neymar mwenyewe inabidi wamsubirie kama miaka mitatu mbele.
 
Umeuliza wana kipi special? wana pesa hao jamaa.

Mishahara wanayowaahidi wachezaji wanaoelekea kustaafu/maliza mikataba yao ligi za ulaya ni kufuru.

Naanza kuona kuna kundi kubwa la wachezaji toka ulaya watakaokwenda Arabuni this summer.

Kuanzia kwa Benzema, Messi, Hazard, Ramos na wengine wote watakimbilia Arabuni wakavune pesa za bure.

Lakini kwenye kuondoa ufalme wa ulaya kwenye mpira wa miguu, hapo naona hali yao itakuwa ngumu, itakuwa kazi ngumu sana kwao kushindana na ligi kama ya Uingereza yenye mashabiki dunia nzima.
 
Binafsi naamini hakuna kinachoshindikana mbele ya pesa. Icheki man city, inashine kwa sababu ya pesa ya mwarabu anayotumia kununua mastaa bora zaidi duniani kwa sasa. Vipi wakianza kuwavutia nyumbani kwao?

Nani alidhani ronaldo na messi waangeweza kucheza saudi arabia siku moja?
ukizingatia hii trend ndo inaanza kushika kasi, ngoja tuone.
 
Hakuna Star atakayeenda kucheza soka uarabuni akiwa na umri wa miaka 20 hata wamlipe nini.
Wewe unafikiri wao hawawataki akina na akina Antoine Griezmann, Mo Salah, Erling Haaland, Mmbappe n.? Wanawataka sana sema wanasubiri giza liingie ndiyo wakawaombe.
Neymar mwenyewe inabidi wamsubirie kama miaka mitatu mbele.

kwa kipi special kilichopo ulaya mpaka mchezaji akatae pesa nyingi za mwarabu?

ukizingatia hii trend ndo inaanza kushika kasi, karibuni wanaweza kuwang'oa kina haaland na pesa wanazo.
 
Kabla ya Mwarabu alianza Mchina.
Ukitaka kujua kwa lipi basi waambie wawanunue wakiwa wabichi
 
Ulaya imejisimika kama mfalme wa biashara ya soka duniani kana kwamba wachezaji wote huona kufika huko ndio mafanikio ya soka duniani.

Wana kipi special hawa jamaa?

Nini kinawapa haki ya kutoa mchezaji anayeitwa bora zaidi duniani kutoka ligi zao?

Nini kinawapa haki ya kuzi rank timu na ligi zao kuwa ndio bora zaidi duniani?

ronaldo alipotua saudi arabia walimtia majungu sana kwenye media zao.

Why not asia or american teams?

Kwa jeuri ya pesa waliyonayo waarabu kwa sasa wanaweza kumchukua mchezaji yoyote pale ulaya. Hivi kwa hii trend iliyopo ya kunyakua mastaa wakubwa wa Ulaya, kuna siku wataweza kuondoa utawala wa Ulaya katika soka la dunia?
We jamaa hujui mpira au kilaza sana. Nani katika peak uliwahi ona anaenda kucheza soka uarabuni? Yaani hapo pa kutumia tu akili za darasa la pili unashindwa? Yaani wenzio wanamtumia binti akiwa kigori. Wewe unakuja kuoa akiwa mzee kwa pesa nyingi.....
 
kinacho matter hapa ni influence ya pesa kuwang'oa mastaa wakubwa ulaya. Wachezaji bora wa america kusini, ulaya huwa ni kama destination kwao kutokana na pesa. Lakini sasa waarabu nao wameanza kumwaga pesa kuliko hata ulaya na wanazo nyingi. Hii maana yake hata hawa wachezaji bora watalazimika kukimbia ulaya kwenda uarabuni.
China nao walianza kununua wachezaji ghali wa Ulaya ili ligi yao iwe kubwa, lakini leo hii wameishia wapi?

Ligi inaundwa na wachezaji wa ndani na wachezaji wa nje, kama nchi haina wachezaji wazuri wa ndani ni ngumu sana kuwa na ligi bora
 
Binafsi naamini hakuna kinachoshindikana mbele ya pesa. Icheki man city, inashine kwa sababu ya pesa ya mwarabu anayotumia kununua mastaa bora zaidi duniani kwa sasa. Vipi wakianza kuwavutia nyumbani kwao?

Nani alidhani ronaldo na messi waangeweza kucheza saudi arabia siku moja?
ukizingatia hii trend ndo inaanza kushika kasi, ngoja tuone.
Itachukua labda karne moja
Maana ligi za Ulaya ni global brands tayari na zina hela pia, zina mashabiki wengi duniani, na utamu wa soka ni mashabiki, ambao ligi za kiarabu hazina
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom