Hivi vitu ni propaganda au??

Takwimu ndio kitu cha msingi mkuu . hata ukimwi Kuna watu toka wazaliwe hadi leo watu wazima Kinga ziko stable japo wanavirusi
Ila Hata mimi huwa sielewi ni nani aliyesema ukivuta bangi pafu moja madhara miaka Saba? Nimegoogle kote hicho kitu hakipo ila yapo madhara ya bangi.

Sehemu ambapo uvutaji wa bangi ni mkubwa na rate za uhalifu ziko juu mno...
 
Is 20% Normal ( Huyo ni mtu maarufu anayefahamika na ni mvuta bange )
Jamaa amevuta bangi, zikamsaidia kutunga nyimbo mzuri mpaka Tanzania ikamfahamu na akanyakua tuzo 5 kwa mpigo, Bado unasema jamaa ni chizi?
Basi akina Enstein nao ni machizi
 
Hivyo vitu havina madahara mkuu wangu we kama unatumia tumia tu wala usiogope
 
Kwa upande wangu naona wavutaji bangi wengi wapo na self awarenes,
na hawapendi kupelekeshwa.
Sasa inapotokea mtu amemzingua huwa hawawazi marambili, so chochote kitakachomjia atakifanya ili kujiponya maumivu aliyosababishiwa, hiki kitu ndio kinageuka na kuitwa uhalifu.!!
Yani
Kumpiga ngumi mtu aliyekudharau ni ualifu tehe tehe
 
Yani bange vuuuuuutaaaaa sigara ndo usiseme we vuta ila katika yote usitumie madawa ya kulevya drug abuse
 
Na watu kama hao unakuta hawatetereki afya, Mfano P funk Majani...
Jamaa tangu enzi zile mpaka sasa ni mwendo mdundo
Nani kakwambia kua afya ya mtu hupimwa kwa kumuangalia mtu kwa macho tuu?!
 
Unataka kusema wanaotoa ushauri huwa wanafanya kwa mazoea tu? Lakini sicho wanachokimaanisha?
Siwezi kuwahukumu watu wote wanaotoa ushauri kama unavyowaza wewe,bali nimedhamiria kua sio kila anayekupa ushauri wa jambo fulani basi nilazima naye awe analitimiza,

Kama mtu amekushauri kua usitumie "unga" coz una madhara kiafya,na ikiwa utamuona huyo mtu aliyekushauri yeye akitumia huo unga,hiyo haimaanishi kua unga ni salama coz hata aliyekushauri usitumie yeye anautumia.
 
Wewe kama unatumia usijishtukie kuja kutafuta uhalali wa kuvuta bangi zako, wewe endelea tu, ila muda utaongea
 
Nani kakwambia kua afya ya mtu hupimwa kwa kumuangalia mtu kwa macho tuu?!
Mzee nimetolea mfano huyo jamaa kwavile ni famous, haya nambie unataka nitoe mfano kwa mtu gani kama hadi Fidel castro utakataa
 
Tuachane na unga, turudi kwenye mada kuu, hasa kwa watu niliowatolea mifano hapo juu, mfano Castro, bob marley, bi kidude, obama, che guevara, nyerere n.k
 
Wewe kama unatumia usijishtukie kuja kutafuta uhalali wa kuvuta bangi zako, wewe endelea tu, ila muda utaongea
Wacha kuhemkwa, usitumie makalio kujibu hoja zangu, sawa dogo?
 
Tuachane na unga, turudi kwenye mada kuu, hasa kwa watu niliowatolea mifano hapo juu, mfano Castro, bob marley, bi kidude, obama, che guevara, nyerere n.k
Huwezi kutumia watu wachache sana kupata result kua jambo fulani halina madhara! Research zina kanuni zake,pia ni fani inayosomewa.
 
Huwezi kutumia watu wachache sana kupata result kua jambo fulani halina madhara! Research zina kanuni zake,pia ni fani inayosomewa.
Basi sawa, tuangalie mazingira yanayotuzunguka, ni wangapi mtaani kwenu wanaoumwa kansa kwa kuvuta sigara?
N.B
mtaani kwangu hakuna
 
Basi sawa, tuangalie mazingira yanayotuzunguka, ni wangapi mtaani kwenu wanaoumwa kansa kwa kuvuta sigara?
N.B
mtaani kwangu hakuna
Ugonjwa ni siri ya mgonjwa,hata kanuni za kidaktari haruhusiwi kutangaza ugonjwa wa mgonjwa kwa watu wengine,si rahisi kama unavyofikiria kujua mtaani kwako nani ni mgonjwa wa kansa? Tena juu ya hivyo ujue hiyo kansa yake imesababishwa na Sigara!!

Mkuu ukitaka kupata accurate figure ya results ya hivi vitu,unatakiwa upate from reliable source.
 
Mkuu usijaribu kujiingiza kwenye jambo ambalo watu walitumialo jambo hilo hujitahidi kutoka lakini wanashindwa.
 
Hata papuchika inapigwa vita sana. Fikiria kwanini
 
Mkuu usijaribu kujiingiza kwenye jambo ambalo watu walitumialo jambo hilo hujitahidi kutoka lakini wanashindwa.
Uko sahihi kabisa Mkuu,kuna watu Sigara zinawatesa lakini ni ngumu kwao kuacha kuzivuta coz wamekua tayari ni addicted,hakuna mvuta Sigara asiyejua madhara ya Sigara!

Kuna watu wamekua ni watumwa wa Pombe lakini wameshindwa kuziacha! Zipo thread nyingi tu humu JF watu wakitaka ushauri jinsi ya kuacha pombe na sigara, kua muangalifu sana unapotaka kufanya jambo,usidanganyike na muonekano wa nje wa watu.
 
Kuna haja gani yakuweka tahadhari kwa kitu chenye madhara?, kwanini kisiteketezwe tu? Kama ni biashara kubwa basi haina mantiki. Kama ni hivo basi hata bange, unga ngada vyote ni biashara kubwa sana ya mabilioni kama Pombe na sigara, je ni halali kuidhinisha matumizi yake ila tuweke tu tahadhari kwa watumiaji?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…