Hivi unawezaje kuishi na kumvumilia mwanamke mwenye tabia za ujeuri na ubishi kwako?

Kifaru86

JF-Expert Member
Apr 22, 2017
1,734
3,802
Wanawake bana wanataofautiana tabia wako wapole, wakarimu, wacheshi, wakorofi na wajeuri sasa Leo nataka nizungumzia wanawake wenye tabia za ujeuri ambao wanaendeshwa na hisia na mawazo ya ubishi na ujeuri ambao huwa hawapendagi kukubali kama wamekosa wala kuelekezwa jambo

Hivi mwanamke wa namna hii unawezaje kumvumilia mapungufu yake akiwa ndani ya ndoa au kabla hamjafunga ndoa au mkiwa wapenzi maana imefika hatua wanaume wenzangu hatupendi kushindana

Hebu tupeane ushauli kidogo
 
Binafsi nilishindwa kabisa kuishi na mwanamke wangu sababu ya tabia hizo .....kauli ya eti 'wanawake tuishi nao kwa akili ' ..haina mashiko kabisa kwa wanawake kama hawa.......sana sana ukitaka kuishi naye ukubali kuwa fala au mshenzi mshenzi kabisa .....

Mimi nilikataa kuwa fala au mshenzi sababu kwa jeuri na dharau za mwanamke yule ningeishia jela na yeye futi sita chini halafu watoto wangekosa wazazi wote wawili....ni bora niliamua kuachana naye ili tulee watoto tu wote tukiwa wazima......ni ngumu sana kuishi na wanawake kama hawa labda uwe marioo huna ishu kabisa.
 
Walio tutangulia waliyajua hayo ndio maana waliweka utaratibu wa UCHUMBA ambapo hiki ndio kipindi cha KUCHUNGUZANA kitabia na mengineyo

Lkn pia utaratibu wa UCHUMBA una manufaa makubwa zaidi kwa mwanaume maana ndie anaye fanya uchaguzi wa awali kuona yupi anakufaa ndipo uchumba unaanza kwa kumshirikisha mke

Ikumbukwe kuwa uchumba unaweza kuvunjika dakika yoyote endapo mmoja kati yenu atagundua kuwa mwenendo au tabia za mke au mume mtarajiwa hazimpendezi na akatafuta mwenza mwingine pia huu ni mchakato ambao unapaswa kufanyika kwa makini na kushirikisha jamii ya eneo husika

JE HAYA HUWA MNAYAZINGITIA VIJANA AU MNAWAZA KUPIGA GAME TU?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sisi ni binadamu tu tutabaki hivyo hivyo labda ubahatishe malaika nasijui utamtolea wapi
Kilicho fanya Nika zaliwa na kukua sio raha ya ndoa Bali nikuzijua tamaa na njaa na kupambania mkuu pambana na uhusiano wako ukikushinda piga chini
 
Wanaume tunapaswa kutambua kuwa sisi ni watawala wanawake ni wasaidizi wetu tu hivyo kuna tofauti kubwa kifikra kati yetu na wao

Kimsingi hata wao hutambua kuwa mwanaume ndio last say na wao ni washauri tu hivyo pale anapo jaribu kutikisa kiberiti nivyema kusimama imara

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MKAKA HALISI,
UCHUMBA Hauna guarantee ya kumjua mtu wako ....mara nyingi nimeona watu wanakaa miaka migi kwenye uchumba halafu wakiingia kwenye ndoa inavunjika ndani ya muda mfupi....hii ni nimejionea mwenyewe zaidi ya mara moja
 
UCHUMBA Hauna guarantee ya kumjua mtu wako ....mara nyingi nimeona watu wanakaa miaka migi kwenye uchumba halafu wakiingia kwenye ndoa inavunjika ndani ya muda mfupi....hii ni nimejionea mwenyewe zaidi ya mara moja
Iko hivi ; unaweza kwenda shambani saa 12 asubuhi na mwingine akaenda 2 asubuhi na wote mkarudi saa sita Lkn ukiangalia work efficiencies huyu wa saa mbili ikawa kubwa kuliko wa 12 japo ndie alie tangulia

Kuna vitu unatakiwa ufanye wewe na sio kuangalia mtu mwingine kwani umakini na vipaombele huweza kuchangia mafanikio au hasara

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafsi nilishindwa kabisa kuishi na mwanamke wangu sababu ya tabia hizo .....kauli ya eti 'wanawake tuishi nao kwa akili ' ..haina mashiko kabisa kwa wanawake kama hawa.......sana sana ukitaka kuishi naye ukubali kuwa fala au mshenzi mshenzi kabisa .....

Mimi nilikataa kuwa fala au mshenzi sababu kwa jeuri na dharau za mwanamke yule ningeishia jela na yeye futi sita chini halafu watoto wangekosa wazazi wote wawili....ni bora niliamua kuachana naye ili tulee watoto tu wote tukiwa wazima......ni ngumu sana kuishi na wanawake kama hawa labda uwe marioo huna ishu kabisa
Na Mimi naongezea Ni ngumu Sana sanaaaaaa labda mwanaume awe karogwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
yan mkiwa kwenye uchumba na ndoa ni vitu viwili tofauti...
unaweza ukaka kwenye uchumba na mtu miaka kumi ukaona uyu anafaa lkn kaa mae ndani mwezi mmoja tu utaona vitu ambavyo hujawahi hata waza kama anaweza kiwa navyo...@MKAKA HALISI,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom