Hivi ukimsaidia mtu ni lazima uchukulie ujiko?

Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
67,029
173,693
Kuna tabia flani ntaaita ya kishwaini ambayo tunayo wabongo hasa wenye sijui ni ushamba au, mtu kakuomba assistance katika jambo lake flani au kakwama hivi...

Unampa shavu halafu baadae huko ni mwendo wa kujisifia tu kwa watu. "David amepata kazi bana ila bila mie kufanya mambo pale Airtel wasingemchukua" hapo ni kwenye mkusanyiko wa ndugu labda...au jamaa! Wengine wanaenda deep kwamba jamaa toka nimtaftie kazi hata simu tu hajapiga.

Mwengine nae..."Fredy alikuja kututembelea last weekend tukala lunch nikampa na elfu 50 atie mfukoni"...Kulikuwa na haja gani ya kusema ulimpa hela?

Do you really need to do that? Kuna ulazima wa kujimwambafy ukimsaidia mtu?
 
Ninakumbuka nilipokuwa SECONDARY nilikuwa ninakwenda kumtazama ndugu yangu mmoja kwake....
Alhamdulillah Mwenyezi Mungu ambariki kwani alikuwa ananipa buku 5 hadi 10 ambazo kwa mwanafunzi wa BOARDING si haba....

Kitendo cha kuondoka tu kwake...anapiga simu home kwetu na kwa ndugu wengine kuwa AMENIPA LAKI.....

Hali hiyo ilijirudia mara kadhaa...🤣

Kikubwa MWANADAMU Bora ni yule mwenye GOOD CHARACTER na MSIRI mengine mbwembwe tu....

Shout out kwa wote WALIOTUFIKISHA TULIPO bila ya kupiga "makelele"!!🙏🙏🙏
 
Nilimsaidia demu fulani tulisoma nae chuo kimoja na kozi moja, mwanzo tuko chuo nilikuwa namfatilia na nilikuwa nampenda sana hadi leo, alivopata kazi kupitia mimi nikawa nakumbushia utongozaji daaah alinijibu "UNATAKA RUSHWA YA NGONO" nitakurepoti kwa mamlaka!!

Daaah nilishangaa sana, sasa mfano issue kama hii nisimwambie mtu wangu wa karibu au rafiki yake kubwa ikiwa ni kuweka sawa?

So kuna namna ya Ku present hizo fagilia zikaonekana ushamba au majivuno, sio zote uki breach no mbaya nyingine unalazimika.
 
Kwani wakati unamsaidia ulimwambia na kuwekeana mkataba kuwa atakapofanikiwa ATAKULIPA HAYO UTAKAYO?!!!
 
Hapana tena tulikuwa na mawasiliano mazuri tu sema mzigo ndo alikuwa ananichenga.
Sasa unalalamika nini?!!
Sasa unayaripoti kwa wengine ili iweje?!!

Na hawa wanaume wenzetu waliotubeba maishani ndio tuwalipe "migongo" maana kuna wengine ni "mabaahaashaa"?!!🤣
 
Sasa unalalamika nini?!!
Sasa unayaripoti kwa wengine ili iweje?!!

Na hawa wanaume wenzetu waliotubeba maishani ndio tuwalipe "migongo" maana kuna wengine ni "mabaahaashaa"?!!
Tafakari kwa kina sijalalamika, nimesoma Uzi nikakumbuka hili lililonitokea kwa sababu ilibidi nihusishe baadhi ya watu tulisove maisha yaendee nikaishia pale pale kumfatilia lakini hakuwahi kusema hata ahsante !
 
Asante uliyoitaka ni kukupa "unyevu" si ndio?!!🤣🤣
 
Kuna tabia flani ntaaita ya kishwaini ambayo tunayo wabongo hasa wenye sijui ni ushamba au, mtu kakuomba assistance katika jambo lake flani au kakwama hivi...

Unampa shavu halafu baadae huko ni mwendo wa kujisifia tu kwa watu. "David amepata kazi bana ila bila mie kufanya mambo pale Airtel wasingemchukua" hapo ni kwenye mkusanyiko wa ndugu labda...au jamaa! Wengine wanaenda deep kwamba jamaa toka nimtaftie kazi hata simu tu hajapiga.

Do you really need to do that? Kuna ulazima wa kujimwambafy ukimsaidia mtu?
Ukiona mtu anafanya hivyo ujue ni utoto.

Lakini pia kuna mazingira mtu anaweza sema au testify kwa nia njema na kwa faida na kwa ajiri ya kujifunza.. lakini kuna wengine hufanya kwa kuji mwabafai..
 
Back
Top Bottom