Hivi tunanunua kwa utashi au uhitaji? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi tunanunua kwa utashi au uhitaji?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mtambuzi, Mar 17, 2009.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Mar 17, 2009
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Hivi unafahamu kwamba kuna watu wengi sana miongoni mwetu ambao hutumia fedha nyingi kwa vitu au mambo yasiyo ya lazima? Kwa kadri tunavyojipatia fedha zaidi ndivyo tunavyoitumia bila mpangilio. Hali hii ya mfumo wa maisha yanayo jail mali zaidi, imefanya watu wengi kuchanganyikiwa nakushindwa kujua tofauti kati ya uhitaji na utashi.

  Kwa mfano mtu anaposema, ‘nahitaji televisheni ya nchi 36 sebuleni kwangu ‘ au ‘unahitaji viatu vinavyoendana au kumechi na nguo zangu.’ Je haya ni mahitaji au utashi, yaani kutaka kitu? Siku zote utashi umefungwa kwenye vitu au mambo ambayo ukiangalia kwa kina utagundua kwamba hayawezi kumfanya mtu ashindwe kuishi endapo atayakosa.

  Kwa kutaka kwetu huwa tunajikuta hatimaye tukiingia kwenye maisha ya mashaka na hofu tunapofikia umri wa kati (miaka 35 hadi 55), kwa sababu ndiyo umri mgumu sana linapokuja suala la mtu kuamua kama akubaliane na maisha anayoishi au ajichanganye.

  Kwa nini nilianza kwa kuzungumzia suala la hitaji na utashi? Jawabu ni kwamba kwa kuyajua vizuri maswala haya ndipo tunavyoweza kujitoa kwenye tafrani hii ya kimaisha. Kufahamu tofauti iliyopo kati ya hitaji na utashi kunaweza kabisa kutufanya kujua namna ya kutafuta yale ambayo ni mahitaji badala ya utashi.

  Huwa tunahitaji chakula, mavazi, makazi/malazi, elimu, usafiri wa kuaminika, na tekinolojia kwa sababu ya kurahisisha shughuli zetu. Lakini pia tunahitaji mara chache kuwajali watu wa familia zetu.

  Mbali na hayo hatuhitaji kuwa na televisheni ya inchi 36 yenye kushika stesheni 500 kwenye sebule zetu, gari flani la kifahari, nyumba yenye njia panda ndani au swimming Pool yenye kufanya kila kitu yenyewe. Huhitaji hayo kamwe lakini huwa tunakuwa na utashi nayo tunayataka. Sisi huku kutaka tunakuita kuhitaji.

  Kumbuka kwamba hakuna makosa kwa mtu yeyote kumilika vitu hivyo na siyo vibaya kwa mtu kuvitafuta. Lakini ubaya ni kwamba vitu hivi kamwe haviwezi kutupa furaha. Badala yake mara zote vinatuunganisha na mnyororo unaotupeleka katika kufanya shughuli tusizozipenda.

  Kwa nini kuna wauza ‘unga’ mjambazi, makuadi wa kisiasa na wengine wa aina hiyo? Thubutu! Wanafanya kwa sababu wanadhani wanachohitaji ni mahitaji wakati ni utashi.

  Kuna wale wanaofanya shughuli halali lakini hawazipendi hata kidogo. Wanapata hata BP kutokana na shughuli kwa kawa huweza ikawa ni ngumu mno za hatari sana lakini wanang’ang’ania kwa sababu tu zinawapa kinachoweza kupata yale wanayodhani ni mahitaji.

  Kuna wale wanaofanya shughuli zao mbalimbali kwa sababu wanazipenda na siyo kwa kuwaingizia pato la kuwapa yale wanayodhani ni mahitaji. Kwao inakuwa vigumu kuingiza pato na hata misukosuko ya kufilisika nayo huwa mingi. Lakini wanapokuja kusimama husimama kweli. Wale wanaofuata mlio wa fedha kwa kufanya chochote siku zote awali huwa na hali nzuri lakini baadae lazima waanguke vibaya.

  Kuna haja ya kukumbuka kuwa, kuamini kwamba mali maana yake ni mafanikio na kila kitu cha gharama kubwa kifedha ni cha mahitaji ni tabia tu. Kama hiyo ni tabia inaweza ikabadilishwa.

  Kwa mfano sasa imethibitika kwamba mtu anaweza kujifunza kufanya matumizi kidogo na ikawa ndiyo tabia yake. Kufanya matumizi kidogo ina maana ya kutafuta mahitaji kweli na siyo yale tunayodhani yatatupa thamani. Kwa kutegemea kidogo sana mambo ambayo wala siyo mahitaji katika kutupandisha thamani, huweza kutupa amani na furaha ya ukweli.

  Kwani vitu vya thamani kamwe haviwezi kupima thamani aliyonayo mtu kwa kujitofautisha na wengine wasio navyo, ambapo kwa dhana hiyo wanaonekana kutokuwa na thamani.

  Tukae tukijikumbusha tu kwamba thamani ya mtu haiwezi kupimwa kwa kulundika vitu ambavyo ni utashi na wala siyo mahitaji.

  Lakini kuna ukweli kwamba mahitaji hayana maana yanapokuwa mengi au makubwa kwani ni mahitaji tu, maji ya kunywa ni gilasi moja hata kama una mapipa mia moja, huyahitaji kwa wakati mmoja hayo yote..
   
 2. Kitia

  Kitia JF-Expert Member

  #2
  Mar 17, 2009
  Joined: Dec 2, 2006
  Messages: 410
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hongera Mtambuzi kwa mada yako nzuri ya kuelimisha. Ni kweli katika hayo unayoyasema, kuwa mtu anahitaji kutambua matumizi yake ya lazima na yale ya utashi. Hata hivyo ni vigumu sana kuweza kutambua hivyo kwa vile, kwa mara nyingi, moyo wako hukusukuma kuhitaji vitu vile, na usipovipata, moyo hautatulia. Hata hivyo unaweza kuweza kupambanua mahitaji yako kutokana na hali unayopitia katika maisha, kwa mfano, ukipungukiwa na uwezo wa kununua vile vitu, utakuja kugundua kuwa maisha yanaendelea vizuri tu bila kuwa navyo. Pili, ni kupata elimu kama hiyo uliyotoa hapo juu. Kipingamizi kikubwa cha kuweza kutambua mahitaji muhimu na yale ya utashi ni umri. Binadamu akiwa katika umri wa ujana anapenda naye aonekane katika jamii kuwa amefikia hali fulani, bila kujali, wakati mwingine athari zake.

  Hata hivyo uanapoongezeka kiumri, unakuwa na majukumu mengi amabyo ni lazima uyape kiupaumbele, na hapo itabidi uchague. Ukishaanza kuchagua utaona kuwa kumbe mambo mengine uliyoyaona ni ya maana na ya kukufurahisha sio lazima.
   
Loading...