Hivi Tunaelewana Tunaposema Tunajenga Uchumi Wa Viwanda?

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
Ndugu zangu,

Ninaposikiliza mijadala bungeni juu ya dhana ya uchumi wa viwanda napata uelewa mpya kuwa huenda hatuelewani kama taifa tuna maana gani katika hilo la uchumi wa viwanda.

Mimi nadhani, kuwa tunaposema viwanda tunapaswa pia kuangalia ngazi; vidogo, vya kati na vikubwa.

Kwa mujibu wa ripoti za OECD na Africa Economic Outlook, Tanzania inatajwa kuwa ni emerging economy na emerging market. Kwamba nchi yetu ina viashiria vya kuwa na mazingira na uchumi na soko linalokua.

Ni kwenye mijadala hii ya Bungeni, unaona, kuwa yumkini kwenye safari yetu hii ya maendeleo ya uchumi wa viwanda bado njia tunayopita haijawa clearly defined, kwamba wenye wajibu wa kuonyesha njia wakati mwingine wanashikwa na vigugumizi. Na wakati mwingine wanaonyesha kabisa kutojiamini kwenye kuongoza safari yenyewe.

Ni lazima wenye dhamana za uongozi watangulie na wawe na uelewa mpana wa kile wanachokisimamia. Wawe na uwezo wa kuifafanua dhana hii ya ujenzi wa uchumi wa viwanda.

Wanavyoonyesha kushindwa kuifanya kazi hiyo, ndipo negative forces na zaidi zenye kusukumwa na maslahi binafsi ya kisiasa, zinapojitokeza na kuonyesha magugu mengi kwenye njia tunayopita. Ndio haya ya kudhani viwanda ni kama vile vya Urafiki, Sunguratex, Bora Shoes na kadhalika. Ni industrial nostalgia. Katika mazingira ya sasa, ni vigumu kurudi kwenye Bora Shoes Company na Serikali kumiliki viwanda. Kuna mtazamo mpya kwenye dunia ya sasa. Ujenzi wa viwanda uongozwe na sekta binafsi na Serikali kazi yake kubwa ni kuandaa mazingira bora ya kukua kwa uchumi wa viwanda.

Ni dhahiri, kuelekea kwenye maendeleo ya viwanda kuna changamoto nyingi, lakini, kuna fursa nyingi pia. Tukiangalia changamoto tu, safari yetu hatutaimaliza.

Na mafanikio ya ujenzi wa uchumi wa viwanda si suala la kufikiwa ndani ya miaka kumi. Yaweza kuchukua hata miaka 30, lakini misingi lazima ijengwe sasa.

Mara nyingi naandika, kuwa historia ni Mwalimu Mzuri. Katika hili la viwanda tunaweza kuziangalia tofauti za kimitazamo hata miaka ile ya sitini.

Kwenye hili la uchumi wa viwanda, Julius Nyerere na Oscar Kambona walikuwa ni kama Gandhi na Nehru kwa India. Nyerere na Kambona walikuwa na uzalendo na utashi wa kuijenga nchi yao waliyozaliwa na waliyoipigania- Tanganyika.

Isipokuwa, walitofautiana kwenye njia ya kupita. Julius alitaka kupita njia ya Ghandi- Village Swaraj. Kwa maana ya kuimarisha vijiji vya Ujamaa na kujenga misingi ya Ujamaa na Kujitegemea. Kwamba vijiji vijitegemee kwa chakula. Uzalishaji uwe wa ushirika na mengineyo yenye kutofautiana na njia ya ubepari kama ya Nehru.

Nehru , tofauti na Ghandi, aliamini kuwa maendeleo ya India yangepatikana kwa kuimarisha viwanda na biashara. Kwa kutumia sayansi na teknolojia ya kisasa kwa viwandani. Na ndivyo ilivyokuwa kwa Kambona.

Naamini, kuwa Julius na Oscar walikuwa na ya kuchanganya kwenye maono yao. Kisha wangepata mseto ulio bora kwa Nchi.
Ndivyo ilivyo sasa kwetu.

Kuna umuhimu wa kuchukua kila kilicho bora katika kila mtazamo na baadae kuchanganya.

Pichani ni kijijini kwetu Nyeregete.
Maggid Mjengwa.

0754 678 252
 

Attachments

  • 2.jpg
    2.jpg
    55 KB · Views: 90
Ndugu zangu,

Ninaposikiliza mijadala bungeni juu ya dhana ya uchumi wa viwanda napata uelewa mpya kuwa huenda hatuelewani kama taifa tuna maana gani katika hilo la uchumi wa viwanda.

Mimi nadhani, kuwa tunaposema viwanda tunapaswa pia kuangalia ngazi; vidogo, vya kati na vikubwa.

Kwa mujibu wa ripoti za OECD na Africa Economic Outlook, Tanzania inatajwa kuwa ni emerging economy na emerging market. Kwamba nchi yetu ina viashiria vya kuwa na mazingira na uchumi na soko linalokua.

Ni kwenye mijadala hii ya Bungeni, unaona, kuwa yumkini kwenye safari yetu hii ya maendeleo ya uchumi wa viwanda bado njia tunayopita haijawa clearly defined, kwamba wenye wajibu wa kuonyesha njia wakati mwingine wanashikwa na vigugumizi. Na wakati mwingine wanaonyesha kabisa kutojiamini kwenye kuongoza safari yenyewe.

Ni lazima wenye dhamana za uongozi watangulie na wawe na uelewa mpana wa kile wanachokisimamia. Wawe na uwezo wa kuifafanua dhana hii ya ujenzi wa uchumi wa viwanda.

Wanavyoonyesha kushindwa kuifanya kazi hiyo, ndipo negative forces na zaidi zenye kusukumwa na maslahi binafsi ya kisiasa, zinapojitokeza na kuonyesha magugu mengi kwenye njia tunayopita. Ndio haya ya kudhani viwanda ni kama vile vya Urafiki, Sunguratex, Bora Shoes na kadhalika. Ni industrial nostalgia. Katika mazingira ya sasa, ni vigumu kurudi kwenye Bora Shoes Company na Serikali kumiliki viwanda. Kuna mtazamo mpya kwenye dunia ya sasa. Ujenzi wa viwanda uongozwe na sekta binafsi na Serikali kazi yake kubwa ni kuandaa mazingira bora ya kukua kwa uchumi wa viwanda.

Ni dhahiri, kuelekea kwenye maendeleo ya viwanda kuna changamoto nyingi, lakini, kuna fursa nyingi pia. Tukiangalia changamoto tu, safari yetu hatutaimaliza.

Na mafanikio ya ujenzi wa uchumi wa viwanda si suala la kufikiwa ndani ya miaka kumi. Yaweza kuchukua hata miaka 30, lakini misingi lazima ijengwe sasa.

Mara nyingi naandika, kuwa historia ni Mwalimu Mzuri. Katika hili la viwanda tunaweza kuziangalia tofauti za kimitazamo hata miaka ile ya sitini.

Kwenye hili la uchumi wa viwanda, Julius Nyerere na Oscar Kambona walikuwa ni kama Gandhi na Nehru kwa India. Nyerere na Kambona walikuwa na uzalendo na utashi wa kuijenga nchi yao waliyozaliwa na waliyoipigania- Tanganyika.

Isipokuwa, walitofautiana kwenye njia ya kupita. Julius alitaka kupita njia ya Ghandi- Village Swaraj. Kwa maana ya kuimarisha vijiji vya Ujamaa na kujenga misingi ya Ujamaa na Kujitegemea. Kwamba vijiji vijitegemee kwa chakula. Uzalishaji uwe wa ushirika na mengineyo yenye kutofautiana na njia ya ubepari kama ya Nehru.

Nehru , tofauti na Ghandi, aliamini kuwa maendeleo ya India yangepatikana kwa kuimarisha viwanda na biashara. Kwa kutumia sayansi na teknolojia ya kisasa kwa viwandani. Na ndivyo ilivyokuwa kwa Kambona.

Naamini, kuwa Julius na Oscar walikuwa na ya kuchanganya kwenye maono yao. Kisha wangepata mseto ulio bora kwa Nchi.
Ndivyo ilivyo sasa kwetu.

Kuna umuhimu wa kuchukua kila kilicho bora katika kila mtazamo na baadae kuchanganya.

Pichani ni kijijini kwetu Nyeregete.
Maggid Mjengwa.

0754 678 252
H
We are not serious. This is only wishful thinking. Kwa hivi hakuna umuhimu wa kuelewana. Bashe alielezea tu wishes zake hungeni lakini watendaji wanajua kuwa hii in utopian ideology.
 
Watanzania tunakejeliwa, tunadharauliwa, tunapuuzwa mno.

Kilimo kimetushinda (na ndio uti wa mgongo wa uchumi wetu) kazi inayofanywa na wasomi na wasio wasomi, wenye mitaji na wasio na mitaji, wenye masoko na wasio na masoko.

VIWANDA NI KEJELI.
 
Shida wa watanzania huwa tunashindwa kujadili na kuchambua mambo bila kuwa na upande wowote ambao tunaamini ni wa kisiasa. Ila ukweli ni kwamba tumeshinda kujua tafsiri ya viwanda ni nini na aina gani ya viwanda tunaviitaji katika karne hii, na muheshimiwa aliposema anahitaji Tanzania kuwa nchi ya viwanda alimaanisha viwanda vya namna gani. Inawezekana kuwa hatuelewani kabisa.
 
Wakati Wao ccm wanafikiria kuweka VAT kwenye rambirambi zote zitakazokuwa zinatokea?
 
*HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI MHESHIMIWA ANTHONY CALIST KOMU (MB) WIZARA YA VIWANDA BIASHARA NA UWEKEZAJI KUHUSU MAPITIO YA UTEKELEZAJI KWA MWAKA WA FEDHA 2016/2017 NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018*
*(Inatolewa chini ya Kanuni 99(9) ya Kanuni za Bunge Toleo la mwaka 2016)*
____________________
1. *UTANGULIZI*
Mheshimiwa Spika, Naomba nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijalia afya njema na kuweza kusimama mbele ya Bunge lako tukufu nikiwa mwenye afya njema kuwasilisha maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani kwa Wizara hii ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kuhusu makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2017/18.

Mheshimiwa Spika, Kwa heshima kubwa naomba nimshukuru Mheshimiwa Freeman Mbowe (Mb) wa Hai na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni (KRUB) kwa imani yake kubwa kwangu na Waziri kivuli mwenzangu wa Wizara hii ya Viwanda na Biashara, Mhe. Cecil David Mwambe (Mb).

Mheshimiwa Spika, Niwashukuru sana wananchi wa Jimbo la Moshi vijijini kwa imani yao kwangu, na ushirikiano wanaonipa katika kusukuma maendeleo ya jimbo letu ninaahidi kwamba nitaendelea kuwawakilisha vizuri kwa uadilifu na umakini mkubwa. Aidha, niwashukuru na kuwapongeza waheshimiwa wabunge hasa wajumbe wa Kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira kwa ushirikiano mzuri katika kuhakikisha Bunge linatimiza majukumu yake.

Mheshimiwa Spika, Mwisho lakini si kwa umuhimu ni kwa familia yangu ambayo imekuwa msaada mkubwa sana katika kutekeleza majukumu yangu.

2.0 *SEKTA YA VIWANDA TANZANIA*

2.1 *Bajeti isiyoakisi Maendeleo ya Viwanda (Hewa)*:

Mheshimiwa Spika, ni wazi kuwa Serikali ya awamu ya tano na zile zote zilizotangulia zinashindwa kuongoza mageuzi ya viwanda nchini kutokana na kuendesha masuala nyeti ya Kitaifa bila kuzingatia nyakati husika na kukubali kujifunza kutoka wataalam mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Mheshimiwa Spika, Dira ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati kiviwanda ifikapo mwaka 2025 haina uhalisia, sio kwa sababu ilichelewa kupangwa bali ni kwa sababu Serikali ya CCM haiwezi kuongoza kadiri ya dira inazojiwekea yenyewe. Ili Tanzania ifanikiwe kuwa ya uchumi wa kati kiviwanda ifikapo mwaka 2025 basi sharti sekta ya uzalishaji (manufacturing) ichangie wastani wa chini wa asilimia 40 katika pato la Taifa ifikapo 2025.

Mheshimiwa Spika, leo hii takaribani miaka 8 kabla ya mwaka 2025, sekta ya viwanda vya uzalishaji (manufacturing) inachangia asilimia 5.2 tu ya pato la Taifa kwa mujibu wa kitabu cha Mpango wa Maendeleo wa Miaka mitano (National Five Year Development Plan, 2016/17 – 2020/21.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Serikali ya CCM imechoka kiuwezo, kiakili, kiutashi na kidhamira, hata kama Rais Magufuli akifanikiwa kukaa madarakani kwa miaka 8 ijayo mpaka kufikia mwaka 2025, yeye na Serikali yake yote hataweza kabisa kuigeuza Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati kiviwanda kwa sababu ili afanye hivyo, Kambi Rasmi ya Upinzani inampa changamoto kuwa kila mwaka wa fedha ikiwamo mwaka huu wa 2017/2018, sekta ya uzalishaji (manufucturing) inapaswa kukua kwa asilimia 4.35 kila mwaka wa fedha mpaka ifikapo mwaka 2025 ili kufikia lengo la kuifanya ‘manufacturing’ ichangie asilimia 40 ya pato la Taifa na hatimaye Tanzania kuwa ya uchumi wa kati kiviwanda!

Mheshimiwa Spika, Ukisoma kitabu cha Mpango wa Maendeleo wa Miaka mitano (National Five Year Development Plan, 2016/17 – 2020/21 Serikali ilijipangia kutumia jumla ya Shilingi Trilioni 5.78 kwa ajili ya uwekezaji katika miradi mikubwa ya kimkakati kwenye sekta ya uzalishaji (manufacturing), wakati ahadi (commitment) ya Serikali pekee ikiwa ni bilioni 659 – angalia Jedwali la 1 hapo chini.

Mheshimiwa Spika,Lakini pia ukisoma makadirio yaliyowasilishwa ndani ya Bunge lako tukufu ili kupitishwa kama bajeti ya Maendeleo kwenye eneo la viwanda ni Shilingi Bilioni 2.38 sawa na asilimia 0.36 (0.36%) ya fedha zote za Maendeleo zilizotakiwa kutolewa na Serikali hii ya CCM kama sehemu ya ahadi (commitment yake). – angalia Jedwali la 2 hapo chini.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaposema hoja ya Tanzania ya viwanda ni hoja hewa, inamaanisha inachokisema. Kwa ‘facts’ ambazo tayari tumezianisha katika jedwali la 1 na 2, ni wazi kuwa hakuna Tanzania ya viwanda inayoimbwa kila kukicha na Serikali ya CCM.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali kulielezea Bunge lako tukufu na Watanzania kwa ujumla inapojigamba kuwa inajenga Tanzania ya viwanda, je Tanzania ya Viwanda itajengwa kwa bajeti ipi? Wakati bajeti yake ni asilimia 0.36 ya fedha zote walizotakiwa kupanga kwa mwaka wa fedha 2017/2018.

Mheshimiwa Spika, Asilimia 96.5 ya viwanda vyote ambayo ni viwanda 50,656 ni viwanda vidogo vinavyoajiri wafanyakazi 1 hadi 9. Asilimia 3.5 vinatoa ajira kuanzia watu 10 na kuendelea. Takwimu hizi hazitoi matumaini makubwa ya kuingia katika uchumi wa viwanda Hivi viwanda vya mtu mmoja mpaka kumi ni kujidanganya, ndio maana Mheshimiwa Waziri mwenye dhamana hujigamba kuwa navyo kwa ajili ya kuvigawa.

*Jedwali 1:*
Uwekezaji katika Sekta ya Uzalishaji (Manufacturing Sub Sector
Jina la Mradi Mpango wa Bajeti 2017/2018
TZS Bilioni Government Commitment
for 2017/2018 Under Five Yrs Deveolpment Plan of 2016/17-2020/21
TZS Bilioni
Bagamoyo SEZ 3,412 402.1
Kurasini Logistics Center 220
Mtwara SEZ (Freeport Zone) 12 0.9
Kigoma SEZ 10 5
Tanga SEZ 5 2.7
Ruvuma SEZ 3 2.6
Bunda SEZ 3 2.8
Morogoro - Star City SEZ 337 13
Industrial Park Interventions 23 20.6
MSMEs Parks Strategic Choices 29 13.3
Automotive industry Strategic Choices 160 70.7
Petro and Chemical Industries Strategic Choices 1,144 30.5
Development of Pharmaceutical Industries Strategic Choices 27 5
Textile and Clothing Industries 10 9.5
Building and Construction Industries Strategic Choices 76 5
Leather Industry Strategic Choices 8 3
Agro processing strategic Choices 129 47.2
Iron and Coal Strategic Choices 179 25.01
JUMLA 5,787 659
Chanzo: URT (2016) National Five Year Development Plan 2016/17 - 2020/21, Page 230 - 241

*Jedwali 2:*
Miradi ya Uwekezaji wa Viwanda Kimkakati iliyotengewa fedha 2017/2018 Fungu 44
Jina la Mradi Kiasi cha Fedha za Maendeleo kilichotengwa kwenye Bajeti, 2017/2018
TZS
Lake Natron 2,000,000,000
Revival of General Tyre and Rubber Plant 70,000,000
Integrated Industrial Develoment 10,000,000
Mchuchuma Coal to Electricity Project 100,000,000
Liganga Vanadium Titanium 100,000,000
KAIZEN 100,000,000
JUMLA 2,380,000,000
Chanzo: Volume IV - Public Expenditure Estimates Development Vote (PART A), Page 70 & 71

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa sensa ya viwanda ya mwaka 2013, inaonyesha kuwa Tanzania ina jumla ya viwanda 50,656 ambavyo vipo katika mikoa mbalimbali hapa nchini, lakini miongoni mwake ni viwanda/mashirika 119 ambayo yalibinafsishwa na kati yake 74 vikiwa vinafanya kazi (vizima), 44 vinaendelea vizuri, 13 vinalegalega na 17 vimefungwa kabisa.

Mheshimiwa Spika, Hii nayo ni hadithi ya siku nyingi na bahati mbaya hivi ndivyo viwanda vikubwa vyenye kuajiri watu wengi na vinavyotumia mali ghafi za ndani zinazotokana na mifugo na kilimo mfano vile vya nguo kama Urafiki,mwatex, kilitex na mutex, na vya ngozi nk. Hatua za Serikali haziridhishi kwa kiwango kikubwa kwani maelezo yao mbele ya kamati ya viwanda, Biashara na Mazingira kuhusiana na vile ambavyo vinalegalega/vimefungwa au wawekezaji wamebadili matumizi/makubaliano Serikali iliiambia kamati wahusika wamewanyima ushirikiano hata mahali pengine wamefungiwa nje ya magate.

Mheshimiwa Spika, bila aibu taarifa ya wizara inasema kuwa baadhi ya viwanda vilivyo binafsishwa vilitumika kama dhamana kukopa benki na fedha hizo zilitumika kwa shughuli nyingine badala ya kuviendeleza, huu ni udhaifu kwa upande wa Serikali.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali iache kuwa na ndimimbili katika utendaji wake, iweje tu polisi wa barabarani waweze kuadhibu mtu anayebadili matumizi ya gari lake labda gari la mizigo akasafirishia abiria hapo kwa hapo ishindikane kwa waliogeuza viwanda kuwa maghala ya bidhaa toka nje au malisho ya mbuzi?

Mheshimiwa Spika, wimbo wa Wizara pamoja na msajili wa Hazina kwamba inafanya upembuzi wa utendaji na mikataba ya viwanda/mashirika ili kufikia uamuzi wa kunyang’anya viwanda/mashirika yanayolegalega nakuwapa wawekezaji wenye uwezo umekuwa ukijirudia kila mara.

Mheshimiwa Spika, hoja hapa ni lini kazi hii itakamilika? Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaishauri Serikali kurejea upya mpango wake wa Maendeleo ya Taifa wa miaka 5 na mpango wa mwaka wa fedha 2017/2018 na kueleza ni kwa namna gani Serikali itashiriki zoezi la kufufua viwanda vilivyofia mikononi mwa wawekezaji waliomilikishwa viwanda hivyo kutokana na sera mbovu ya ubinafsishaji ambayo ilikosa umakini kwa kiwango kikubwa sana hivyo kutoa mwanya mkubwa wa kuua sekta ya viwanda badala ya kuiendeleza.

Mheshimiwa Spika,Ni vema ikaeleweka maeneo haya yanayohodhiwa kwa majina ya viwanda lakini hakuna viwanda ni maeneo yaliyokwisha endelezwa kimkakati kwa uwekezaji wa viwanda hivyo ni uendawazimu kuhubiri kila siku kuwa Serikali inahamasisha kutenga maeneo kwa ajili ya viwanda bila kujiuliza yaliyokwisha tengwa na kuendelezwa yanafanyiwa kazi gani, kwani kila mji ulikuwa na maeneo ya viwanda.

Mheshimiwa Spika, sio busara kupigana kugundua tairi ambalo wenzetu walishagundua. Aidha, Kambi ya Upinzani Bungeni inaishauri Serikali kufanya mapitio upya ya uwekezaji uliofanyika katika msingi wa ujenzi wa viwanda hapa nchini ili kuja na hatua za makusudi katika Maendeleo ya sekta ya viwanda hapa nchini. Msukumo uwekwe zaidi kwenye mazao ya chakula, misitu, mifugo na biashara kama Kahawa, Korosho, Mpira, Pamba, Mchikichi, Katani, Mawese, alizeti n.k Mageuzi ya viwanda duniani hutegemea Maendeleo ya watu, hasa wakulima wa mazao ya chakula na biashara, wafugaji na wavuvi.

Mheshimiwa Spika, Kwa muda mrefu wananchi wa Tanzania wanaolima mazao wameshindwa kuinua hali zao za maisha kutokana na sera ya uwezeshaji wa kimitaji na mazingira magumu ya biashara kuwabana katika uanzishaji wa viwanda vidogo vidogo kuweza kuyaongezea mazao yao thamani kama vile vya kukamua mafuta ya alizeti nk.

Mheshimiwa Spika, changamoto kubwa inayovikabili viwanda nchini ni pamoja na ukosefu wa mitaji, teknolojia ya uzalishaji kupitwa na wakati (vilivyobinafsishwa), malighafi isiyokuwa na uhakika, umeme, maji, urasimu katika kupata huduma mbalimbali zinazotolewa na Serikali, mlolongo wa kodi na kutoshirikishwa katika kufikia maamuzi yenye athari kwa viwanda.
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, inaona kwamba changamoto hizi bado zipo na zitaendelea kuwepo kwa kuwa Serikali haina mkakati wowote maalumu wa kibajeti wa kuondoa changamoto hizi ila ni nyimbo zile zile (Business as usual).

*2.2 Utekelezaji wa Bajeti Usioridhisha katika miradi ya kimkakati*
Mheshimiwa Spika, si rahisi kuamini lakini ni ukweli kuwa maelezo ya Serikali katika utekelezaji wa bajeti na miradi mbalimbali yamejengwa katika misingi ya ujanja ujanja unaolenga kufunika ukweli halisi ili mambo yapite tu.
Mheshimiwa Spika, nitarejea mifano michache inayoweza kuthibitisha ninachoeleza. Fidia ya maeneo ya EPZ na SEZ: Hili ni jambo la kisera na kisheria ambalo limekuwepo kwa muda mrefu na kila mwaka limekuwa likipewa fedha chini ya wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji japo hazilingani kabisa na mahitaji. Aidha ni wajibu wa Serikali kisheria kujenga miundombinu ili kuweka mazingira wezeshi na rafiki kwa wawekezaji katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya SEZ.

Mheshimiwa Spika, mwaka huu wa fedha 2017/2018 jambo hili limetoweka kabisa katika bajeti halitajwi popote pamoja na ukweli kwamba Wananchi katika maeneo kadhaa nchini walishapisha maeneo yao na wamenyimwa kabisa kufanya maendelezo yoyote wakisubiri fidia za maeneo yao. Maeneo yaliyotengwa yana jumla ya hekta 31,000 lakini ambayo yamefidiwa ni takriban hekta 10,000 tu.

Mheshimiwa Spika, nitarejea mifano michache ili kuonyesha hali ilivyo kama Bagamoyo SEZ mchakato wa kutwaa maeneo ya Wananchi ulianza toka 2007 na kukamilika mwaka 2010 kwa uthamini wa hekta 5,742.5 ambapo kilihitajika kiasi cha shilingi bilioni 50.2 kama fidia lakini mpaka leo ni hekta 2,560.8 tu sawa na shilingi.bilioni 28.36 tu ndizo zilizokwisha tolewa kama fidia mpaka sasa.

Mheshimiwa Spika, kwa maelezo ya randama ya Wizara yenyewe kiasi kinachohitajika kufanya fidia katika eneo hili kwa sasa ni shilingi bilioni 51.3 zikijumisha na riba ya ucheleweshaji. Ninajua kuwa Mh Waziri amekuwa akisema fidia ya eneo hili itafanywa na mwekezaji binafsi. Kambi Rasmi Bungeni itataka kujua ni lini mwekezaji huyo atalipa fidia na ni kiasi gani na kwa masharti yapi.

Mheshimiwa Spika, jukumu hili kwa maamuzi ya Baraza la Mawaziri la Serikali ya Mh Rais John Pombe Magufuli limepelekwa kwa sekta binafsi jambo ambalo linakosa uhakika wa kufanyika na halina tena ukomo wa muda wa kutekelezwa.

Mheshimiwa Spika, aidha, hatua hii ni ushahidi dhahiri wa Serikali ya awamu ya tano kukwepa jukumu lake la kisera na kisheria na kuendeleza tabia yake ya kutojali athari mbaya zinazoweza kusababishwa na maamuzi yake kwa Wananchi.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa sheria ya maeneo maalumu ya uwekezaji (SEZ Act Nos 2 of 2006 & 2011) uendelezaji wa miundombinu katika maeneo hayo kwa mujibu wa sheria hii ni jukumu la Serikali lakini maeneo hayo kwa asilimia kubwa yameishia kuambulia visingizio kama ufinyu wa bajeti hivyo maeneo karibu yote yaliyokwisha fidiwa hayajafanyiwa maendelezo yoyote mfano Bagamoyo special economic zone hekta 2,399.6, Kigoma, Tanga ekari 1,363, Bunda ekari 3,255, Mererani hekta 530.87, na Ruvuma.
*2.3. Kupata Mwekezaji atakayejenga Miundombinu ni ndoto ya mchana*

Mheshimiwa Spika, eneo jingine ni mradi wa makaa ya mawe ya mchuchuma na chuma cha liganga. Huu ni mradi wa muda mrefu ambao umetajwa na Serikali kuwa ni mradi wa kimkakati kwa kuwa utachochea maendeleo ya viwanda. Mradi huu una faida zifuatazo:-
a. Mradi wa Mchuchuma na Liganga utahusisha ujenzi wa Kinu cha Umeme chenye uwezo wa Megawati 600 ambapo 250 zitatumika katika Kiwanda cha Chuma na nyingine 350 zitapelekwa kwenye Gridi ya Taifa kwa ajili ya kuongeza nguvu katika nishati ya umeme.
b. Tanzania kwa sasa itakuwa na umeme wa gesi, maji na umeme wa makaa ya mawe ambapo umeme wa makaa ya mawe utakuwa msaada mkubwa kwa nchi kwani hautegemei tabianchi kama ilivyo vyanzo vingine vya umeme.

Mheshimiwa Spika, Pamoja na faida zote hizo bado mradi huu haujapewa uzito unaostahili kila siku kuna hadithi mpya katika utekeleza ji wa mradi huu. Licha ya maagizo mengi ya Bunge lako tukufu.
Mheshimiwa Spika, moja ya maagizo ya kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira ya Bunge la kumi ni kuharakisha utekelezaji wa mradi huu muhimu na wa lazima kwa maendeleo endelevu ya Viwanda. Mwaka jana Bunge lilirudia tena agizo hilo na maelezo ya Serikali yalikuwa kila hatua imeshachukuliwa na mradi huo utaanza robo ya kwanza ya mwaka 2017.

Mheshimiwa Spika, maelezo ya leo ya Serikali yaliyopo katika randama yanasema Baraza la Mawaziri lililokaa tarehe 7 Desemba 2016 na kuelekeza mkataba wa mradi wa mchuchuma na liganga upitiwe upya. Kufuatia maelekezo hayo kamati ya makatibu wakuu iliundwa na kupitia mkataba huo na kutoa mapendekezo ya vivutio vitakavyozingatia maslahi ya Taifa. Kulinda maslahi ya Taifa ni muhimu sana lakini kwanini maelezo yote ya awali hayajawahi kueleza mapungufu hayo na hivi kweli hii ndiyo sababu ya mradi huo kutokuanza muda wote? Hatua hii ni kana kwamba huu mradi ndio unabuniwa kwa mara ya kwanza na sasa ni vigumu kuamini kama mbia aliyekwishatambuliwa ataendelea au la.
Mheshimiwa Spika, majibu mengi ya Serikali katika wizara hii ni ya kupigishana “sound” au blaa blaa!! tu, huo ni ushahidi tosha kuwa Serikali ya CCM ikiwa ni pamoja na hii ya awamu ya tano ni kusema ili mradi muda upite kwa kuwa haingii akilini kuwa mradi huu maelezo yake ndiyo hayo.

Mheshimiwa Spika, maelezo ya Serikali yamekuwa yakibadilika kila siku kutegemea ni nani anapewa taarifa hiyo kama ilivyojidhihirisha hapo juu. Mh Spika mwenendo wa aina hii hauwezi kuifikisha nchi kwenye uchumi wa viwanda kama inavyohubiriwa.
Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi Bungeni inaitaka Serikali kusema ukweli katika mizania hii ambayo inahusu uchumi sekta ambayo inahitaji kuaminiwa na wadau wengine.

*2.4. Ufufuaji wa kiwanda cha General tyre Arusha*
Mheshimiwa Spika, Mh Spika, katika mwaka wa fedha 2016/17 utaona kuwa mradi wa kufufua kiwanda cha General tyre kasma (1210) zilitengwa shilingi milioni 150 kwa ajili ya mradi huo kuandaa andiko la mradi, kuendeleza mashamba ya mpira na kutafuta mbia mpya.
Mheshimiwa Spika, mwaka huu wa fedha 2017/2018 wizara inaomba jumla ya sh 70,000,000 kutafuta mbia lakini utafiti uliofanywa na wataalamu wa ndani inaonyesha kuwa mitambo iliyopo katika kiwanda hicho haifai kabisa kulingana na technolojia ya sasa, kiwanda hicho kinahitaji kupanuliwe ili kiweze kuzalisha kwa wingi kuweza kushindana na soko la kimataifa na imeshauri kiendeshwe na sekta binafsi na Serikali iwe mbia kwa thamani ambazo zipo hapo.

Mheshimiwa Spika, maelezo mengine yaliyo katika kitabu cha mpango wa maendeleo wa Taifa 2017/2018 uk. 20 yanasema baada ya taarifa ya awali ya wataalam hao Serikali inatafakari nini yatakuwa matumizi sahihi zaidi ya eneo la kiwanda hicho, mwekezaji aliyekuwa ameomba kuwa mbia katika kufufua kiwanda ameomba kupatiwa eneo la kuweka kiwanda kipya cha matairi eneo la TAMCO Kibaha, kwa sasa kiwanda hicho kinamilikiwa na Serikali kwa asilimia 100.

Mheshimiwa Spika, kwa maelezo hayo hakuna kitu kinachoitwa kiwanda cha matairi cha General tyre kwa maana ya mitambo ila kuna eneo ambalo palikuwepo na kiwanda cha matairi cha General tyre na mabaki ya kiwanda hicho ambayo kwa lugha fasaha na ya uwazi zinapaswa kuondolewa kupisha uwekezaji sahihi.

Mheshimiwa Spika, bila kuweka jambo hili wazi mbele ya Bunge lako tukufu na maamuzi yakafanyika hicho kinachoitwa kiwanda cha matairi cha General tyre Arusha kitaendelea kuwa kama mfereji wa kutumia fedha za umma kama zilivyokwishatumika huko nyuma bila matokeo. Mh Spika, ni vema tukajiuliza katika kutenga fedha hizi sh. 70,000,000 zinazoombwa, taarifa ya wataalamu imezingatiwa?

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali itoe maelezo kuwa ni kwanini katika Mpango wa Maendeleo wa Miaka mitano (National Five Year Development Plan, 2016/17 – 2020/21, kiwanda cha General Trye kwa mwaka wa fedha 2017/2018 kilipaswa kutengewa jumla ya Shilingi bilioni 22 na sio milioni 70. Kiasi hicho kilichotengwa ni kidogo mno kuweza kufanya kazi zilizokusudiwa na kuwezesha kiwanda hicho kuanzishwa tena upya kwa tija.

*2.5. Kiwanda cha Viuadudu kibaha na kiwanda cha TANALEC Arusha*
Mheshimiwa Spika, Hiki ni kiwanda kilichotajwa na Serikali kama ni cha kimkakati kimekabidhiwa shirika la maendeleo la Taifa (NDC) baada ya ujenzi wake kukamilika kwa mkopo wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 22.307 na wenye riba ya aslimia 11 utakaorejeshwa kwa miaka 10.

Mheshimiwa Spika, ili kiwanda hicho kianze kuzalisha kimepewa na Serikali jumla ya sh 2,100,000,000 na pia kimekopa jumla ya sh. 4,553,010,000 na kimeanza kuzalisha na hadi February 2017 kimezalisha dawa kiasi cha lita 100,000 ambazo zimeuzwa nchini Niger kwa kiasi cha sh 1,012,000,000 tu. Nchi yetu ambayo inatumia fedha nyingi sana kupambana na malaria na ndio ugonjwa unaoongoza kwa kuua haijanunua hata lita moja. Wizara ya afya imeshapitishiwa bajeti yake ya 2017/2018 na hakuna fedha yoyote iliyotengwa kwa ajili ya dawa toka Viaududu Kibaha. Kiwanda hiki hakiwezi kuwa endelevu kama Serikali yetu haitaweza kujipanga na kuwa na soko la uhakika la ndani ambalo ni dhahiri lipo lakini hakuna uratibu ndani ya Serikali (coordination).

Mheshimiwa Spika, Leo kiwanda hicho ambacho kina uwezo wa kuzalisha lita milioni 6 kwa mwaka na kujiendesha hakizalishi kwa kuwa hakina soko la bidhaa zake na kinaendelea kulipa gharama mbalimbali za uendeshaji kama wafanyakazi, umeme nk. Kwa maneno mengine kiwanda hicho kwa sasa kina endeshwa kwa hasara ukiachilia mbali uwekezaji uliokwishafanywa katika kiwanda hicho.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi Bungeni inataka maelezo ya kina juu ya jambo hili ambalo kwa mtazamo wake linafanana na hujuma kwa azma ya Taifa letu kuelekea uchumi wa Viwanda.

Mheshimiwa Spika, aidha, Kambi Rasmi Bungeni inataka pia kujua ni jitihada gani zimefanywa na wizara ya Viwanda, Biashara na uwekezaji ndani ya Serikali katika kupata Soko la Bidhaa za Viuadudu Kibaha kwa kuwa ni jukumu lake kisera na ni nini kikwazo hasa inapozingatiwa katika andiko la mradi huu la mwaka 2010 linaonyesha umuhimu wa kiwanda hiki ni haja kubwa ya kukabiliana na tatizo la ugonjwa wa malaria nchini

Mheshimiwa Spika, tatizo la Viuadudu linafanana kwa kiasi kikubwa na lililopo katika kiwanda cha TANALEC Arusha ambacho mtumiaji mkubwa wa bidhaa zake ingepaswa kuwa TANESCO lakini kwa visingizio mbalimbali vilivyopo ndani ya uwezo wa Serikali kama ikiamua kujiratibu. TANESCO imekuwa ikinunua bidhaa zinazopatikana TANALEC toka nje ya Nchi na kukiacha kiwanda hicho taabani.

Mheshimiwa Spika, wakati TANESCO wameshindwa kununua Transformer zinazotengenezwa na TANALEC kwa sababu ya taratibu za manunuzi, wateja wakubwa wa TANALEC ni majirani zetu wa Kenya, Uganda, Zambia na Msumbiji ambao mazingira yao yanafanana sana hata taratibu zao za manunuzi. Hii ni changamoto kwetu kama Taifa lazima Serikali ikubali kutatua changamoto hizi na kuwezesha viwanda vyetu kwenda mbele.

Mheshimiwa Spika ni wakati mwafaka sasa Serikali kuacha visingizio na kuchukua hatua za maksudi kuona kuwa viwanda vya ndani vinapata fursa katika soko la ndani kwani faida zake ni nyingi kwa uchumi wetu ukilinganisha na visingizio vinavyotolewa eti bei ni kubwa na taratibu za manunuzi haziruhusu lakini moja ya sababu ya bei kuwa juu ni kodi zinazotozwa na Serikali yenyewe na kwa kiasi fulani urasimu unaozalishwa na vyombo vyetu wenyewe vya udhibiti kwa kuongeza gharama za uendeshaji, nyingi ya taasisi hizi hukinzana katika utendaji wake na hufanya jambo ambalo linaweza kufanywa na taasisi moja na kupata matokeo yaliyokusudiwa.

Mheshimiwa Spika, masuala haya ya urasimu, mwingiliano wa vyombo vyetu vya udhibiti, mlolongo wa kodi na taratibu mbaya za manunuzi zinazopewa nguvu na sheria zetu wenyewe zimekuwa kama nyimbo tu au misahafu isiyoweza kurekebishwa.

Mheshimiwa Spika, haingii akilini ni kwanini Serikali haioni ukweli huu na kuchukua hatua au ndio maana kuna msemo unaosema sikio la kufa halisikii dawa?

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inasema sasa ni muda mwafaka masuala yote haya ya bei na taratibu zetu za manunuzi kuangaliwa upya na kuweka utaratibu unaokubalika kisheria unaohami viwanda vyetu vya ndani kwani utakuwa na tija kubwa zaidi kuanzia kwenye ajira ambazo nazo huzalisha kodi nyingine nyingi kama mapato kwa Serikali, kukuza utaalamu wa ndani, urahisi wa kukarabati (after sales service) bidhaa zinazozalishwa hapa nchini na kukuza matumizi ya malighafi zinazopatikana hapa nchini.

Mheshimiwa Spika, mataifa yaliyoendelea kiviwanda hayakuendelea nakufikia yalipo kwa bahati mbaya yalifikia hatua hiyo kwa kujenga uwezo wake wa ndani, kwa kujenga mazingira ya kutumia bidhaa zake na kuwapa wataalamu wake wa ndani fursa ya kujenga uzoefu na uwezo hata kwa kutoa ruzuku inapobidi.


Mheshimiwa Spika, Wakati Mhe Mary Nagu akiwa Waziri kwa wizara hii, alianzisha kampeni ya “buy Tanzania use Tanzania”, hii ni kauli mbiu yenye maana kubwa sana kiviwanda. Hiyo kaulimbiu imeishia wapi?, countinuity ya mambo haipo katika nchi yetu kila waziri akiondoka anaondoka na mafaili yake na anayekuja anakuja na mafaili yake. Hii ndiyo Serikali ya CCM.

*2.6. Kila siku nchi inaanza upya*.

Mheshimiwa Spika; mwenendo huu unaifanya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni irudie maneno yake ya mwaka jana na ni nayanuku “…Miaka mitano ijayo ya Mhe. Rais Magufuli inayotumia ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015, haina jambo jipya katika Maendeleo ya Sekta ya Viwanda hapa nchini. Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 inazungumzia Maendeleo ya sekta ya viwanda katika muktadha ule ule ulioshindwa kuzaa matunda kwa zaidi ya miaka 50 iliyopita. Ilani hiyo ya CCM inasema kuwa;
“Katika kipindi cha utekelezaji wa Ilani hii ya 2015–2020, Chama Cha Mapinduzi kitaielekeza Serikali kuweka nguvu kubwa katika kukamilisha utekelezaji wa Sera ya Maendeleo Endelevu ya Viwanda Awamu ya Tatu (2010–2020) ambayo malengo yake ni kuiwezesha Sekta ya Viwanda kuchangia katika kufikia malengo ya maendeleo ya muda mrefu kama ilivyoanishwa katika Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025...” Mheshimiwa Spika, Mh Rais wa awamu ya tano alishaweka wazi msimamo wake kuwa anajitambua na haelekezwi na mtu yeyote cha kufanya, ni imani ya kambi rasmi ua upinzani Bungeni kuwa sasa Nchi inaendeshwa kwa mawazo na utashi wa Mh Rais John Pombe Magofuli na ndio maana ametamka mara kadhaa kuwa anayo kazi ya kunyoosha nchi kwanza; maana yake ni kuwa watangulizi wake waliipinda nchi sana. Msimamo huu kwa kiasi kikubwa siyo sahihi kwa kuwa huo ni uimla jambo ambalo limeanza kuvuruga uchumi wetu na kuondoka katika vipaumbele tulivyojipangia na kuanza mtindo wa kubahatisha. Ushauri wetu ni kama ule wa Rais mstaafu wa awamu ya nne kuwa yafanyike mapya ya kutupeleka mbele siyo mapya ya kubomoa.

*3.0 SERIKALI KUPOTEZA DIRA KATIKA SERA ZA BIASHARA NCHINI*
*3.1. Mkanganyiko wa Mwelekeo wa Sera Kitaifa*

Mheshimiwa Spika, katika miaka ya 1990 Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ilianza kutekeleza mageuzi makubwa ya kiuchumi (Economic reforms) kwa kubinafsisha mashirika na viwanda vyote vilivyokuwa vinamilikiwa na Serikali na vilivyokuwa havifanyi vizuri.

Mheshimiwa Spika, lengo kuu la kufanya hivyo ni kuiondoa Serikali katika uendeshaji wa moja kwa moja wa shughuli za uzalishaji na Biashara na kuipa nafasi zaidi ya kutoa huduma za jamii, kujenga miundo mbinu, kutunga sera na kujenga mazingira wezeshi na rafiki kwa sekta binafsi na kuwekeza katika mashirika na viwanda vya kimkakati vinavyoweza kuchochea mageuzi ya kiviwanda katika Taifa letu.

Mheshimiwa Spika, baada ya takriabani miaka 27 toka sera hii ianze kutekelezwa, sasa, Serikali ya awamu ya tano ya CCM imeamua kurudi nyuma na kuanza tena kushiriki moja kwa moja katika shughuli za uzalishaji/kiuchumi na Biashara. Mfano mzuri na hai ni tangazo la Serikali kuwa nyumba zote za Serikali zitajengwa na TBA na inasemekana pia ipo nia ya kutaka SUMA JKT ipewe kandarasi zote za ujenzi wa Barabara za Serikali jambo ambalo limeleta hofu kubwa katika sekta hii ya ujenzi ambayo ina mchango mkubwa katika mafanikio tunayojivunia leo.

Mheshimiwa Spika, katika hotuba ya Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Mh Prof. Makame Mbarawa (MB) alilieleza Bunge lako tukufu kuwa makandarasi waliosajiliwa ni 8,475 na alieleza mipango mbalimbali ya kuwa endeleza makandarasi hao. Aidha alieleza kazi nyingi sana zinazofanywa na TBA ambaye ni wakala wa majengo wa Serikali na na ukweli si Mkandarasi lakini yeye sasa ndiye anayetakiwa kufanya kazi zote za ujenzi wa majengo ya Serikali. Swali la msingi hapa, hivi hawa wakandarasi anaowazungumzia Mhe Mbarawa watafanya nini na wapi? Ikumbukwe kuwa hawa wanaajiri wataalamu wetu na wanalipa kodi mbalimbali kwa mujibu wa sheria.

Mheshimiwa Spika, mfano mwingine ni uamuzi wa Serikali kuamua kuingia katika biashara ya Ndege kwa yenyewe kununua ndege 2 na tayari imeshaagiza nyingine nne (4) kwa gharama ya dola za marekani 231.2 tena kwa fedhaa taslimu kinyume kabisa na utamaduni uliozoeleka Duniani kote kibiashara.

Mheshimiwa Spika, maamuzi yote haya siyo sahihi kiuchumi kwa kuwa sekta binafsi ni mdau mkubwa na muhimu kwa uchumi wa Taifa lolote.

Mheshimiwa Spika, Mahali pengi Duniani/kiulimwengu sera za aina hii zimeshindwa na Serikali nyingi zimeamua kuchukua mkondo wa Serikali kujenga mazingira mazuri kwa sekta binafsi kuendesha uchumi.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali iliachie soko lifanye kazi yake, Serikali ijenge mazingira wezishi na rafiki kwa kutunga sera safi, sheria na kuzisimamia kikamilifu , kuondoa urasimu usio na tija, kulinda wawekezaji wa ndani kwa wivu mkubwa na kwa uangalifu wa hali ya juu kwa kuzingatia sheria, kanuni na mikataba ya kimataifa. Ni kwa kufanya hivi ndio tunaweza kupata akina; Ali Mufuruki, Dr Reginald Mengi, Mohamed Dewji, Said Salim Bakhressa na wengi zaidi kama wawekezaji wazawa na kuingia katika uchumi wa kipato cha kati.

Mheshimiwa Spika, katika randama ya Wizara yenyewe imekiri kuwepo na changamoto nyingi katika mazingira ya uwekezaji katika sekta ya viwanda na biashara kama “…uwepo wa kanuni nyingi, uwepo wa wakusanyaji ushuru wengi wa ada mbalimbali, uwepo wa taasisi nyingi za udhibiti (karibu 18), uwepo tozo nyingi za kibiashara (takribani 40) ambazo zinaweza kushawishi rushwa, na uwepo wa gharama kubwa za wadhibiti hususani kupata usajili wa biashara, VAT, ushuru wa ndani na uthibitishwaji wa ubora wa bidhaa…”

*3.2 Matamko ya Viongozi yasiyoendana na Sera za Biashara*

Mheshimiwa Spika, Kumekuwa na viongozi wa Kitaifa ambao hutoa matamko holela yasiyoendana na sera zilizopo, matamko ambayo kimsingi yanayumbisha utulivu wa mazingira ya biashara nchini na kuathiri pato la Taifa kwa ujumla.

Mheshimiwa Spika, matamko hayo yameonyesha mtazamo hasi kwa sekta binafsi kwa kuwa hayazingatii sheria zilizopo, sera, uwekezaji uliokwisha fanywa na mdau katika sekta mbalimbali. Mfano uamuzi/ agizo la Mh. Rais la kufuta leseni ya Mtafiti wa madini katika eneo la Geita eti kwasababu tu alilalamikiwa na Wananchi kwenye mkutano wa hadhara. Serikali kuzuia kusafirisha mchanga ghafla tena tayari makontena yakiwa yameshafika bandarini kana kwamba yalikuwa yanatoroshwa.

Mheshimiwa Spika, matamko mengine ni pamoja na marufuku ya Serikali juu ya matumizi ya pombe ya Konyagi inayopatikana katika vifungashio vinavyojulikana kama viroba kuanzia tarehe 01/03/2017 jambo ambalo limewagharimu Watu wengi uchumi wao hadi kujiua nimkumbuke mwananchi wa jimbo langu Ndg Peter John Mselia aliyepoteza maisha katika sekeseke hili, Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi. Matamko yote niliyoorodhesha hapo juu ni maamuzi yasiyo shirikishi na pia hukiuka mkataba na kuendelea kuleta hofu na maswali mengi kwa wawekezaji katika Nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, Uwazi katika Uendeshaji wa Biashara nchini ndio msingi wa kukusanya mapato halisi bila kudanganywa na wawekezaji. Uwazi hauanzii kwenye usafirishaji wa bidhaa nje ya nchi bali uwazi huanzia katika Mikataba ya Kibiashara, lakini Serikali hii ya CCM bila kuzingatia ushauri wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni uliotolewa mara kwa mara kuhusu kuweka wazi mikataba tata baina ya Serikali na Makampuni ya Uchimbaji madini. Kwa mfano wakati dhahabu ndio inaongoza kibiashara na kunachangia asilimia 21 ya mauzo ya bidhaa zote nje ya nchi kwa takribani dola bilioni $1.42, Serikali inarukia ejenda ya kuzuia mchanga wa madini kuuzwa nje ya nchi, kuikosesha nchi mapato bila kwanza kuweka wazi mikataba ya uchimbaji, ambayo ndio chanzo cha nchi kupoteza mapato mengi.

*3.3 Kushuka kwa mauzo nje ya nchi (Exports) kinyume na malengo ya Sera ya Taifa ya Biashara*

Mheshimiwa Spika, Sekta ya Biashara nchini inaongozwa na Sera ya Taifa ya Biashara ya mwaka 2003 iliyobuniwa na Serikali ya CCM, ambayo dalili za kisayansi zinaonesha kuwa imechoka kiakili katika kuisimamia Sera yake yenyewe. Tafiti mbalimbali duniani na nchini zinaonesha kuwa Sera hii pamoja na utekelezaji wake haifanyi vizuri katika Maendeleo ya Sekta nzima kwa ujumla.

Mheshimiwa Spika, Sera hii ya Taifa ya Biashara katika dira yake inaweka mkazo kwa Sekta nzima ya biashara kuwa ni kuugeuza uchumi kuwa wa uuzaji wa bidhaa nje ya nchi (export-led); Dira ya Sera hiyo inasema, nitanukuu:-
“... to transform the economy from a supply constrained one into a competitive export-led entity responsive to enhanced domestic integration and wider participation in the global economy through national trade liberalisation”
Tafsiri yake ya Kiswahili ni kuwa:-
“…kubadilisha uchumi kutoka katika vikwazo vya usambazaji kwenda kwenye ushindani wa mauzo ya bidhaa nje ya nchi yatakayowezesha maingiliano ya ndani na ushiriki mkubwa wa uchumi wa dunia kupitia biashara huria kitaifa”

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imebaini kuwa msingi mkuu wa Sera ya Biashara ya Taifa ni “mauzo ya bidhaa nje ya nchi” yaani “exports”. Msingi ambao ujenzi wake kwa vitendo umekuwa ni kitendawili kikubwa kutokana na Serikali hii ya CCM kushindwa kwa vitendo kuimarisha uzalishaji wa bidhaa na huduma ndani ya nchi ili hatimaye kuongeza mauzo ya bidhaa nje ya nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, Ripoti ya Shirika la Trading Economics iliyochapwa mwaka 2017 katika takwimu zake zimeonesha kuwa mauzo ya bidhaa nje ya nchi (Exports) yameshuka kutoka Dola milioni 932.90 mwezi Januari, 2016 mpaka Dola milioni 854 mwezi Disemba, 2016. Wastani wa mauzo ya bidhaa nje ya nchi uliendelea kubakia kuwa dola milioni 549.16 kutoka mwaka 2006 mpaka mwaka 2017.

Mheshimiwa Spika, Ripoti ya Benki ya Dunia ya mwaka 2017 iitwayo “Ease of Doing Business Tanzania” (Wepesi wa Kufanya Biashara Tanzania) imeripoti kuwa Tanzania imeshika nafasi ya 180 kati ya 190 (nafasi 10 kutoka mkiani) katika wepesi wa kufanya biashara baina ya mipaka ya nchi na nchi (Trading Across Borders)
Mheshimiwa Spika, kukamilisha nyaraka za mauzo ya bidhaa nje ya nchi hapa kwetu Tanzania inachukua saa 96 (karibuni siku 4) wakati Botswana huchukua takribani saa 8 tu, na Kenya majirani zetu huchukua muda wa saa 21. Kushuka kwa mauzo ya bidhaa nje ya nchi kumeendelea kushika kasi hasa katika kipindi amacho Serikali ya awamu ya tano ipo madarakani.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali kutoa taarifa mbele ya Bunge lako tukufu juu ya hatua inazozichukua kuhakikisha inaongeza kiwango cha mauzo ya bidhaa nje ya nchi (Exports). Tunaitaka Serikali kuhakikisha kuwa inaboresha mazingira ya biashara katika mipaka ya nchi na nchi (Trading Across Borders). ili nchi yetu iendelee kuaminiwa na wawekezaji wa ndani na nje ni lazima sera na sheria zetu za biashara ziaminike, ziheshimiwe na ziwe shirikishi (Predictable and participatory).

*3.4 Uratibu Mbovu wa Sekta ya Viwanda na Biashara*
Mheshimiwa Spika, Serikali imeshindwa kwa kiwango kikubwa kuratibu vyombo vyake vinavyotoa huduma mbalimbali katika wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji hususani vile vya udhibiti na uratibu. Yapo malalamiko mengi yanayoonyesha kuwa vyombo/ wakala wa Serikali wamekuwa wakiongeza urasimu na gharama zisizo na tija na hata kusababisha kufa kwa miradi kadhaa au kushindikana kwa miradi kadhaa nchini mfano mzuri ni mgogoro unaokinyemelea kiwanda cha Tanga Cement PLC

Mheshimiwa Spika, baada ya kiwanda cha Tanga Cement PLC kukidhi vigezo vyote vya kisheria kama vilivyowekwa na TIC kiwanda hiki kilitambuliwa kama mradi wa kimkakati na hivyo Serikali kupitia TIC ikatoa vivutio kadhaa vikiwemo msamaha wa kodi kwa wataalamu washauri toka nje ya nchi, kodi ya zuio (withhold tax) kwa manunuzi ya mitambo na vipuri vyake na mwaka 2009 mkataba ukaingiwa kati ya Serikali (TIC) na mwekezaji. Kiwanda hiki kilipata mkopo wa kujenga mradi huu toka taasisi za fedha za Afrika Kusini na mikataba yote iliingiwa kwa kuzingatia unafuu uliotolewa na Serikali kupitia TIC lakini taasisi nyingine ya Serikali (TRA) ilikuja kufanya ukaguzi na kutaka kodi zote zilipwe ikiwa ni jumla ya Shilingi. Bilioni 17. Madai ya TRA ni kwamba makubaliano ya Tanga Cement PLC na TIC hayakuwekwa kwenye gazeti la Serikali (GN) hivyo kisheria hayatambuliki jukumu ambalo lilipaswa kufanywa chini ya Wizara ya Fedha.

Mheshimiwa Spika Kiwanda hicho kwa sasa kipo kwenye mkanganyiko mkubwa kutokana na msimmo huo wa TRA kwani fedha hizo zinazodaiwa hazipo na wataalamu washauri waliojenga walishalipwa na wanaoendelea na ushauri wanao mkataba wenye punguzo la Kodi hizo na ni jambo la kisheria ambalo kulivunja lina athari zake kubwa.

Mheshimiwa Spika huu ni mfano unaotokana na Serikali kutokuwa na uratibu miongoni mwa vyombo vyake. Kiwanda hiki hakina kosa ila kinabebeshwa mzigo na matokeo yake kitayumba na malengo yaliyokusidiwa kupotea kabisa kwa uzembe wa Serikali yenyewe ambayo ina jigamba kujenga mazingira rafiki na wezishi kwa ustawi wa kauli yake mbiu ya Tanzania ya Viwanda.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali ichukue hatua za haraka na za makusudi kutatua tatizo hili kukinusuru kiwanda hiki muhimu. Itakuwa fedheha sana kwa Serikali inayojitanabaisha kwa kauli mbiu ya Tanzania ya Viwanda kuongeza gofu jingine jijini Tanga ambalo tayari limeshaelemewa na magofu ya viwanda vingi vilivyouawa na Serikali za CCM awamu zilizotangulia.

Mheshimiwa Spika kana kwamba haitoshi kiwanda hiki kinaandamwa na tatizo lingine linalosababishwa na Serikali pia. Tanga cement PLC kilitambuliwa kama kiwanda cha kimkakati kwa lengo la kutengeneza Clinker ambayo ni malighafi kwa ajili ya viwanda vya cement nchini hasa vile vidogo vidogo

Mheshimiwa Spika, kutekeleza jukumu hilo mahitaji ya nishati ya umeme ni makubwa sana yanaweza kuchukua asilimia 70 ya uendeshaji wa kiwanda hicho. Umeme unaweza kuwa unaotokana na Maji (TANESCO) au Gesi au makaa ya mawe. Umeme wa makaa ya mawe kutoka nje ya nchi ndiyo nishati ya umeme wa uhakika na nafuu kwa kiwanda hicho lakini bila kujali ustawi wa kiwanda hiki Serikali imepiga marufuku uagizaji wa makaa ya mawe toka nje jambo ambalo limekiacha kiwanda hicho na chaguo la kutumia umeme wa Tanesco ambao hauaminiki na ni ghali sana au kununua makaa ya mawe hapa nchini ambayo nayo hayapatikani kwa kadiri ya mahitaji na kwa wakati lakini pia ni ghali sana kutokana na gharama za usafirishaji kutokana na miundombinu ya inayotumiwa.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali kukaa na wadau wa viwanda vya cement nchini na kukubaliana namna yenye tija ya kututua mikanganyiko hii ambayo kimsingi inaweza kuua baadhi ya viwanda vyetu vingi vya cement hapa nchini na dhamira safi ya Serikali ya awamu ya tano ya kujenga viwanda na kupunguza uhaba wa cement nchini jambo litakalosababisha bei ya bidhaa hii kuwa ya juu kinyume na matarajio.
*4.0 SEKTA YA BIASHARA*

*4.1 Mazingira Magumu ya kufanya Biashara nchini*
Mheshimiwa Spika, Ripoti ya Ease of Doing Business Tanzania 2017 imeonesha kuwa Tanzania imeongeza ugumu zaidi katika hatua za kuanzisha bishara kwa kuongeza tozo za usajili. Jambo hili linaathiri juhudi za kuongeza ajira kwa vijana wetu. Tanzania imeshika nafasi ya 135 kati ya 190 katika wepesi wa kuanzisha biashara mpya. Unapokuwa na ugumu wa kuanzisha biashara, unawafanya wajasiriamali wasifanye shughuli rasmi ya kuingiza mapato yao na mapato ya Serikali, na hivyo kupunguza kiasi cha ajira zitokanazo na biashara rasmi.

Mheshimiwa Spika, ili mjasiriamali aanzishe biashara Tanzania anatakiwa kuruka vihunzi 9 vya utaratibu wa usajili ndani ya siku 26 na gharama ya asilimia 21.5 ya mapato ya Mtu mmoja kwa mwaka (per capital income). Biashara za ujenzi wa majengo ikiwemo uuzaji wa vifaa vya ujenzi unakabiliwa na changamoto kubwa ya muda mrefu unaotumiwa kutoa Kibali cha Ujenzi (Construction Permit). Utafiti wa Ease of Doing Business 2017 unaonesha kuwa inachukua takribani siku 205 na taratibu 18 ili mfanyabishara apate kibali cha ujenzi. Kuingiza umeme kwenye biashara mpya kama vile kiwandani inachukua siku 109 na hatua 4 za ukamilishaji wa nyaraka mbalimbali. Kupata hati ya nyumba kwa ajili ya biashara mbalimbali inachukua hatua 8 ndani ya siku 67 kukamilisha mchakato wa kupata hati hizo.

Mheshimiwa Spika, nchini Rwanda, ambako ndiko Serikali ya awamu ya tano inapendelea sana kwenda kuchukua ushauri wa masuala mbalimbali ikiwemo jinsi ya kukusanya kodi, inachukua muda wa siku 1 tu kufungua Kampuni bila kulipia gharama zozote zile. Hapa nchini inachukua siku 4 kufungua kampuni na ada inayotozwa ni kati ya Shilingi 20,000 na 440,000 jambo linazuia biashara nyingi kurasimishwa, ajira kupotea na sekta binafsi kuendelea kudumaa.

Mheshimiwa Spika, kutokana na mazingira magumu ya kuanzisha na kuendeleza biashara nchini, utafiti uliofanywa na Wizara ya Viwanda na Biashara mwaka 2012, (National Baseline Survey Report – Micro, Small and Medium Enterprises in Tanzania) unaonesha kuwa asilimia 96.4 ya biashara za chini (Micro-Entprises) hazijasajiliwa na BRELA, na asilimai 84.4 ya biashara ndogo (Small Enterprises) hazijasajiliwa na BRELA, huku asilimia 63 ya wafanyabishara waliohojiwa wakisema hawajui chochote juu ya masuala ya usajili wa biashara.

Mheshimiwa Spika, hii ni ishara kuwa mazingira ya kuanzisha biashara nchini sio rafiki kiasi cha kuwa na kiwango kikubwa cha biashara zinazoanzishwa bila kusajiliwa rasmi. Ni ishara pia kuwa mipango ya Serikali haiwezi kuwafikia kundi hilo kubwa la wafanyabiashara nchini ili kuboresha mazingira yao ya biashara na kuongeza mapato ya Serikali kwa namna itakayofaa.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali kuboresha mazingira ya kuanzisha biashara kwa kupunguza idadi ya siku mpaka kufikia siku moja (saa 24) na kuondoa tozo za usajili wa makampuni ili kuchochea wajasiriamali kufungua makampuni kwa wingi na kuongeza ajira kwa Watanzania. Aidha, tunaitaka Serikali kuweka mazingira rafiki na yanayovutia wafanyabisahara wa kada zote kusajili biashara zao kwa namna itakayoiwezesha Serikali kubaini wafanyabishara walipo ili kuwapelekea Maendeleo kwa wepesi na haraka zaidi, tofauti na ilivyo hivi sasa, ambapo ni vigumu mipango ya Serikali kuzifika biashara ndogo ndogo zaidi ya asilimia 90 ambazo hazijasajiliwa na kutambuliwa.

*4.2 Kufungwa kwa Biashara zaidi ya 2,000 nchini*

Mheshimiwa Spika, Waziri Uchumi na Mipango, Mhe. Dr. Philip Mpango alinukuliwa na gazeti la Mwananchi, tarehe 3 Januari, 2017 akikubali kuwa Serikali imebaini kuwa karibu wafanyabiashara 2,000 wamefunga biashara zao. Gazeti hilo hilo la Mwananchi, lilimnukuu mwenyekiti wa Wafanyabiashara nchini, Bw. Johnson Minja akidai kuwa kufungwa kwa biashara hizo kunatokana na Serikali kutosikiliza kilio cha muda mrefu cha wafanyabiashara, na kuwa Serikali imeweka mazingira magumu sana ya kufanya biashara hapa nchini.

Mheshimiwa Spika, Suala hili la kufungwa kwa biashara nchini limetolewa angalizo na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF). Ripoti ya IMF kuhusu utekelezaji wa Sera Tanzania (Policy Support Instrument for Tanzania) iliyotolewa tarehe 9 Januari, 2017 imeionya Tanzania kuwa moja ya masuala yanayohatarisha ukuaji wa uchumi ni pamoja na “kuyumba kwa sekta binafasi kutokana na mikakati mipya ya Serikali ya awamu ya tano” (private sector uncertainty about the government’s new economic strategies.)

Mheshimiwa Spika, kama biashara 2,000 zilizofungwa wastani kila biashara inaajiri watu 5, inamaanisha kuwa ajira 10,000 za Watanzania zimepotea kutokana na sera mbovu za uratibu wa biashara nchini zinazosimamiwa na Serikali ya awamu ya tano. Serikali imevuruga mazingira ya biashara nchini na hivyo kupelekea wananchi wengi kuishi maisha ya dhiki na taabu.

Mheshimiwa Spika, muendelezo wa sera hizi zinagharimu ajira na biashara nchini ni kinyume cha ushauri uliotolewa na Shirika la Fedha la Kimataifa – IMF tarehe 14 Aprili, 2017 Tanzania kuifikia malengo ya uchumi wa kati sharti iwe na sekta binafsi yenye nguvu na yenye mazingira bora ya biashara. Ni wazi kuwa kudorora huku kwa biashara na kuendelea kufungwa kwa biashara nchini ni ishara kuwa Serikali ya awamu ya tano haielewi inataka kulipeleka wapi Taifa letu kwa kuendelea kuharibu mazingira ya biashara nchini.

Mheshimiwa Spika,Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, inaitaka Serikali kutoa taarifa za kina kwanini biashara zaidi ya 2,000 zimefungwa nchini. Aidha, tunaitaka Serikali iseme kuwa ni hatua zipi inazozichukua ili kuondoa mdororo wa biashara nchini na hatua zilizochukuliwa kuzuia kuendelea kufungwa kwa biashara nyingine nchini.

*4.3 Hali duni ya Wafanyabiashara wadogo pamoja na Machinga*
Mheshimiwa Spika, Taifa letu limekosa dira muafaka (a right vision) juu ya kuendeleza watu wake kupitia sekta isiyo rasmi iliyojaa wafanyabiashara wengi wa biashara ndogo ndogo maarufu kama wamachinga. Kwa ufupi, Tanzania kwenye sekta ya Biashara ni Taifa la wachuuzi, ambao kwa muda mrefu biashara zao imekuwa ikiathiriwa na ukosefu wa dira muafaka ya Serikali kuhusu biashara ndogo ndogo.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni bado inaendelea kusisitiza kuwa ‘Maendeleo ni ya watu na sio ya vitu’ hivyo ni jukumu la Serikali kuangalia Maendeleo ya kila mtu mmoja mmoja kwa makundi yao kama vile ilivyo kwa kundi la wafanyabiashara ndogondogo.

Mheshimiwa Spika, Serikali pamoja na kufanya tafiti mbalimbali kupitia mashirika yake mbalimbali lakini inashindwa kuzitumia tafiti hizo kwa umakini wakati wa kupanga vipaumbele kwenye sekta ya ukuzaji wa biashara kwa ajili ya Maendeleo ya watu nchini.

Mheshimiwa Spika, Moja ya tafiti ambazo hazitumiki ipasavyo na kwa kiwango cha kuridhisha katika kupanga Maendeleo ya wafanyabiashara ndogo ndogo ni pamoja na utafiti uliofanywa na Wizara ya Viwanda na Biashara mwaka 2012 juu ya Sekta ya Biashara za Chini, Ndogo, na Biashara za Kati (National Baseline Survey Report – Micro, Small and Medium Enterprises in Tanzania).

Mheshimiwa Spika, Utafiti huo ulibaini kuwa vijana wa Kitanzania wenye umri kati ya miaka 25 na 34 ndio kundi kubwa kwa asilimia 36 linalojihusisha na biashara ndogo ndogo nchini, wakati kwa ujumla wake asilimia 14.6 hawajawahi kumaliza elimu ya shule ya msingi, na asilimia 73.5 ndio wamemaliza elimu ya shule ya msingi na asilimia 72.1 katika maisha yao yote hawajawahi kabisa kupata mafunzo yoyote kabla hawajaanza biashara. Bila kuwa na ‘picha kubwa’ yaani maono makubwa ya kuliangalia taifa letu miaka 100 mbele, taifa haliwezi kupiga hatua za Maendeleo ya kibiashara kwa haraka, bali tutaenda kwa kusuasua kama ilivyo hivi sasa.

Mheshimiwa Spika, Ukisoma kitabu cha randama ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa mwaka wa fedha 2017/2018 fungu namba 60 hakuna malengo ya kushughulikia masuala ya wafanyabishara ndogo ndogo. Katika hali kama hii, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ilitarajia Wizara ya Viwanda na Biashara katika malengo yake kwenye sekta ya biashara katika mpango wa taifa na katika bajeti ya mwaka 2017/2018 itoe kipaumbele kuboresha mazingira ya wafanyabiashara ndogo ndogo kulingana na tafiti zilizofanywa huko nyuma, jambo ambalo halijapewa umuhimu na Serikali.

*5.0 SEKTA YA MASOKO*

Mheshimiwa Spika, dhana ya masoko ina uhusiano wa moja kwa moja na aina na ubora wa bidhaa zinazozalishwa na uwezo wa mtu kufanya mahusiano ya kibiashara. Kwa muktadha huo, masoko hayatafutwi kwa kuangalia siasa za washirika wako tu.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inasema ili kupata masoko kama ni ya bidhaa zako haina maana kwamba uzuie bidhaa za mshindani wako. Unachotakiwa kufanya ni kuzalisha kwa ubora uliozaidi na pia bei yake iwe ni shindani kwa kulinganisha na bidhaa kama hizo za mshindani wako.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Taifa letu halizalishi vya kutosha bidhaa za ndani hivyo manunuzi ya bidhaa nje ya nchi (imports) ni makubwa zaidi ya mauzo ya bidhaa nje ya nchi (exports). Takwimu zinaonesha kuwa mauzo yetu ya bidhaa nje ya nchi yameshuka kwa asilimia 5.0 ambayo ni sawa na shilingi Trilioni 8.22 wakati uagizaji wa bidhaa nje ya nchi ukiongezeka kwa asilimia 8.9 ambayo ni sawa na Shilingi Trilioni 19.90.

Mheshimiwa Spika; Sera mbovu za biashara zilizo asisiwa na Serikali hii ya CCM hazijaweza kumudu kuiondoa nchi katika hali mbaya kama hiyo. Nchi yetu imekuwa tegemezi na haizalishi vya kutosha kiasi cha kuagiza kutoka nje ya nchi hata chakula kama sukari, mchele, ngano na mahindi, samaki, matunda mazao ambayo yalipaswa kupatikana kwa wingi hapa nchini na hata ziada ya kuuza nje.

Mheshimiwa Spika; Kwa sasa Tanzania inanunua mchele kutoka katika mataifa ya China, India, Indonesia, Pakistan na Vietnam, wakati uzalishaji wa ndani ukiwa mdogo ambapo asilimia 18 ya familia zinazojihusisha na kilimo ndio hulima zao la mchele. Jiji la Dar es Salaam pekee hutumia asilimia 60 ya mchele unaozalishwa ndani wakati asilimia 30 huliwa na wakulima wenyewe na asilimia 10 inayobakia huingia katika soko la ndani hasa maeneo ya mikoani. Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya Global Agricultural information Network iliyotolewa tarehe 21 Machi 2016 kama ilivyoandaliwa na Benjamin Mtaki na kuidhinishwa na Kate Snipes.

Mheshimiwa Spika; ni aibu kubwa kwa nchi yetu kuagiza mchele kutoka mataifa mengine wakati tuna mito inayotiririka maji mwaka mzima, tuna ardhi kubwa yenye rutuba, na vijana wetu wana nguvu za kuzalisha ila Serikali haijatilia maanani aibu hii mbele ya uso wa ulimwengu. Taifa linashindwa kuzalisha ngano na badala yake thamani ya manunuzi ya ngano nje ya nchi yaani “imports of wheat” yamefikia dola milioni 225 kwa mwaka kwa mujibu wa Global Agricultural information Network.

Mheshimiwa Spika; Ununuzi wa bidhaa nje ya nchi (imports) unachangia katika kuporomosha thamani ya Shilingi ya Tanzania kiasi cha kulifanya taifa letu kupoteza hazina yake ya fedha za kigeni na kuongezeka kwa pengo kubwa katika urari wa biashara. Thamani ya Shilingi ya Tanzania dhidi ya dola ya Marekani imeporomoka kutoka shilingi 1,754.7 Januari 2015 mpaka kufikia Shilingi 2,335 mwezi May 2017. Sababu zinazotajwa na Serikali kuchangia uporomokaji huo ni pamoja na kupungua kwa mauzo ya nje ya nchi. Hapa Serikali imeendelea kukiri udhaifu wake kuwa inashindwa kabisa kusimamia thamani ya Shilingi dhidi ya dola ya Marekani katika soko la dunia

Mheshimiwa Spika, “nchi yoyote inayotaka kujitegemea kibajeti lazima iimarishwe na bidhaa zake zilizoongezewa thamani na kuuzwa nje ya nchi” hii ni kauli ya mtendaji mkuu wa TPSF

*6.0 SEKTA YA UWEKEZAJI NA UWEZESHAJI

Mheshimiwa Spika, Kwa mujibu wa Sera ya Uwezeshaji ya Taifa ya mwaka 2004 pamoja na sheria ya usimamizi wa sheria hiyo ya mwaka 2004 vililenga kuhakikisha kwamba watanzania waliowengi wanapata fursa ya kushiriki katika shughuli za kiuchumi kwenye sekta mbalimbali. Mataifa mengine yamefanya hivyo, mfano; Afrika Kusini mwaka 1994 baada ya kumalizika kwa Ubaguzi wa Rangi walianzisha sera ya kuwawezesha Waafrika wazawa Kiuchumi (Broad-Based Black Economic Empowerment (B-BBEE)),

Mheshimiwa Spika, Kwa upande wetu, Sheria na Sera za Uwezeshaji na Uwekezaji ni dhahiri vimeshindwa kukidhi matakwa tarajiwa, imebaki makabatini badala yake Serikali ya awamu ya tano ni kama imetangaza vita na watanzania wazawa pale walipojaribu kutafuta fursa za kuwekeza kwa kuwaona kama maadui wa uchumi wetu na haya yanajidhihirisha jinsi wafanyabiashara wanavyosumbuliwa na kutengwa katika shughuli ambazo wameandikishwa kihalali.
Mheshimiwa Spika, Serikali inawachukulia wafanyabiashara kama mahasimu wake nasio kama wadau muhimu, hata uamuzi wa Serikali wa kuondoa pesa zake na za mashirika katika benki za biashara ni katika mtazamo huo hasi ambao unawanyonya wafanyabiashara na na mazingira ya biashara kwa ujumla.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inauliza katika mazingira kama hayo, Sera na sheria za uwezeshaji zinawasaidia vipi watanzania katika kushiriki na kumiliki sekta mbalimbali za uchumi wa nchi yetu? Ni dhahiri kuwa Serikali imeshindwa kuwasaidia Watanzania kuingia katika biashara kubwa kwa makusudi au kwa kukosa uwezo wa kujenga mazingira wezeshi kwa Watanzania kuwekeza na kuwa sehemu ya wamiliki wa uchumi wao. Serikali za CCM zimeshindwa kabisa kutumia ardhi na raslimali asilia za nchi yetu kama mtaji kwa watanzania katika ubia na wawekezaji wa nje.


*6.1. TIC NA UWEKEZAJI WA KUSUASUA NCHINI*
Mheshimiwa Spika, Hali ya uwekezaji nchini hairidhishi hata kidogo hii ni kutokana na marekebisho ya mara kwa mara ya sheria zinazosimamia vivutio vya uwekezaji, urasimu, rushwa, ukosefu wa uratibu wa kiSerikali n.k

Mheshimiwa Spika, Sababu nyingine zinatokana na utawala mbovu kama ucheleweshaji wa vibali mbalimbali vya kuwasaidia wawekezaji kuendeleza miradi yao, umeme usiokuwa wa uhakika, ubovu na urasimu wa usafirishaji na bandari ya Dar es salaam kuwa na urasimu uliokithiri, migogoro ya ardhi isiyotatuliwa, mlolongo wa kodi na ufanisi duni wa wakala wa Serikali, bodi za mazao na riba kubwa zinazotozwa na taasisi za fedha na raslimali fedha zisizokidhi mahitaji ya TIC mfano 2017/2018 TIC haikutengewa hata senti moja kama OC.

*7.0. HITIMISHO*
Mheshimiwa Spika; Msimamo wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na Ilani ya Uchaguzi ya CHADEMA/UKAWA iliyouzwa na Mgombea Urais wa CHADEMA/UKAWA Mheshimiwa Edward Lowassa tuliwaahidi Watanzania kuwa katika kipindi cha miaka mitano yaani 2015 – 2020 naomba kunukuu tamko la Ilani, alisema kuwa “Tutainua mchango huu wa sekta hii muhimu (ya viwanda) ufikie siyo chini ya asilimia kumi na tano (15%) katika miaka yetu mitano ya kwanza”. Tutafanya hivyo kwa:

1) Kuimarisha sekta ya viwanda kuwa mhimili wa uchumi kwa uzalishaji wa bidhaa na ajira endelevu;
3) kuingia mikataba ya kuleta technolojia ya kutengeneza bidhaa badala ya kuleta bidhaa;
4) Kuhakikisha kuwa ndani ya miaka mitano asilimia (75%) ya mali ghafi zote za Tanzania zinasindikwa kabla ya kusafirishwa nje ili kuongeza mapato na ajira ya mamilioni ya vijana;
5) Kutoa kipaumbele na vishawishi maalum kwa viwanda vya kuendeleza kilimo. Kwa mfano, tutaendeleza viwanda vya mbolea kulingana na mahitaji ya taifa na uuzaji wa ziada ya bidhaa hiyo nje ya nchi; pili viwanda vya kutengeneza mbegu bora na madawa ya kilimo;
6) Kufufua na kuongeza viwanda vyetu vya nguo ili tuweze kusindika kiwango kitakachofikia asilimia sabini na tano (75%) ya pamba inayozalishwa Tanzania.
7) Kuimarisha na kukuza usindikaji wa mazao ya katani, kahawa, tumbaku na chai ili kuhakikisha ongezeko kubwa la thamani katika mazao haya na ongezek kubwa la bidhaa zinazotokana na mazao haya.

Mheshimiwa Spika, Serikali za CCM kwa utamaduni wake wa kutaka kuonekana inafanya imekuwa ikijiwekea vipaumbele vingi na wasivyoweza kutekeleza au visivyo na mchango mkibwa katika mageuzi ya kiviwanda yanayoelezwa na dira ya Taifa au kutokana na kujaribu kushika kila kitu na mwishowe kushindwa vyote. Tunataka utamaduni huu sasa ukome kwani unaliingizia taifa hasara kwa kutenga fedha kidogo kidogo kwenye miradi na hatimaye kushindwa kukamilisha miradi husika kwa wakati na huku gharama za miradi zikikua maradufu kutokana na mabadiliko mbalimbali na kwa wakati mwingine kulipa watumishi wasiokuwa na kazi ya kufanya kutokana na kutokuwepo kwa fedha za kutekeleza majukumu yao. Haya ni malipo hewa yanayotokana na mipango hewa. Tanzania kwa sasa itakuwa na umeme wa gesi, maji na umeme wa makaa ya mawe ambapo umeme wa makaa ya mawe utakuwa msaada mkubwa kwa nchi kwani hautegemei tabianchi kama ilivyo vyanzo vingine vya umeme.

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, inasisitiza na kuendelea kuishauri Serikali kuwa bado inaweza kubadilisha mwelekeo wake kwa kuzingatia msimamo wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni kuhusu Maendeleo ya Sekta ya viwanda.
Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani naomba kuwasilisha.


*………………………..*
*ANTHONY CALIST KOMU (MB) *
*MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI*-
*WIZARA YA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI*
*17.05.2017*
 
Back
Top Bottom