Hivi tukitumia DDT hatuwezi kuondokana kabisa na mbu na hatimae kuagana na Malaria?

N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
6,825
9,533
Nawaza kama Serikali ifanye utafiti juu ya kuangamiza kabisa mazalia ya mbu nchini kwa kutumia DDT ili tuagane kabisa na Malaria. Hili gonjwa linazingua mjue.

Hata kama ilizuiwa mbona nasikia kuna nchi nyingi tu wanaendelea kuitumia na huko India inaendelea kuzalishwa kama kawaida.

"Malaria haikubaliki"
 
Umenikumbusha wimbo wa AFANDE SELE.

nadhani unaitwa MALARIA.

Jamaa anasema amekutana na bosi wake jeshini analia, kafiwa MKE na MTOTO.
Maumivu anayosikia ni kama ANACHINJWA KWA MSUMENO.
 
Nakumbuka gazeti la Ijumaa au Uwazi likiwa na kichwa cha habari 'DDT siyo tiba, ni msiba'
 
DDT is potentially carcinogenic, wacha tu tulale ndani ya vyandarua na kutumia rungu(spray). Long term effects za DDT ni kubwa sana.
Nimesoma bango moja inaonekana kampuni za vyandarua na dawa zimo kwenye hizo conspiracies zinazozuia DDT isitumike kuua mbu. Nawaza kama wachina ndio watakaoweza kututoa hapa...kwanini baadhi ya nchi ziwe zimeweza kutokomeza kabisa Malaria na mbu wa aina yoyote sisi tusiweze tukajifunze kwao tuchukue hatua.

Hivyo vyandarua wananchi wetu wanafugia kuku na walio navyo hawajifuniki na kuna wanaofanya kazi nyakati za usiku...kuna maeneo ya starehe huko kote wananchi wanakuwa exposed kwenye mbu wa Malaria..

Na Malaria bado ni kinara wa kuondoa uhai.

Tchukue hatua. Walioweza kutokomeza kabisa Malaria wamefanyaje?
 
Nawaza kama Serikali ifanye utafiti juu ya kuangamiza kabisa mazalia ya mbu nchini kwa kutumia DDT ili tuagane kabisa na Malaria. Hili gonjwa linazingua mjue.

Hata kama ilizuiwa mbona nasikia kuna nchi nyingi tu wanaendelea kuitumia na huko India inaendelea kuzalishwa kama kawaida.

"Malaria haikubaliki"
Ndio mkuu tunawesa tu hii malaria ni Hofyoooo kabisa
 
DDT Inauwa hadi wale wadudu muhimu kama nyuki manyugwi na sisimizi kabla haijaingia kwenye vyanzo vya Maji na hatimae kwenye chakula na hapo ndio tunakutana na saratani ya kila aina
 
Malaria ni mradi mkubwa pesa, kuna mtu alileta mada kuhusu makampuni ya madawa yanavyonufaika na magonjwa yetu, ddt ilitokomeza malaria Cuba inapigwa vita sababu kama hakuna mbu hakuna malaria kama hakuna malaria hakutakuwa na madawa ya malaria, ajira zitapotea kuanzia viwanda vya madawa mpaka viwanda vinavyouza vyandarua
 
Nawaza serikali basi ingenunua zile dawa za kiwanda cha KIBAHA izigawe kwenye Halmashauri zote nchini kisha itengwe siku moja au siku tatu ya kila mtaa nchini Tanzania kupuliza/Furmigate mazingira yote hatarishi yakiwemo mashimo ya vyoo mitaro nakadhalika...hii malaria itasepa tu
 
Kile kiwanda kilichopo pwani, cha kutengeneza kiwatirifu cha kuua mbu, kilifia wapi??kwani kilizinduliwa kwa mbwembwe, kuwa ni cha kwanza afrika!!
Naomba tafadhali kukazia kwenye hili swali. Awamu hii hakisikiki tena! Na tuliahidiwa makubwa sana kupitia kile kiwanda! Na ilikuwa ni enzi zile za JK bila shaka.
 
Hiyo ni miradi ya watu, ni sawa useme HIV itapatiwa chanjo.

Watu wanaingiza mahela mengi kupitia hizo projects
 
Inashangaza sana , hebu angalia mwenyewe nchi kama south africa , ambayo wazungu wemelowea DDT ni ruhusa kutumika lkn huku kwingine wakitaka kutumia wanazuhiliwa kwa kuambiwa inaua hadi other important species , swali je hao other important species ambao hawatakiwi kuuliwa kwenye nchi nyingine za africa , south Africa hawapaswi kuwepo ?.

Najua wengine watasemaa oohh itapelekea watu kupata saratan , okay fine but DDT has been used for decades in western countries , the question is , are they not aware of these impacts that they are telling us ?.

I think , they know for sure what they have been up with all this time , i totally agree with someone above who said that they never wanted us to use it to proctect their companies that have been running this bussiness and enjoying the super normal profit out of us .
 
Nawaza serikali basi ingenunua zile dawa za kiwanda cha KIBAHA izigawe kwenye Halmashauri zote nchini kisha itengwe siku moja au siku tatu ya kila mtaa nchini Tanzania kupuliza/Furmigate mazingira yote hatarishi yakiwemo mashimo ya vyoo mitaro nakadhalika...hii malaria itasepa tu
Walishapewa maagizo ila kama unavyojua hakuna utekelezaji wala ufuatiliaji
 
DDT Inauwa hadi wale wadudu muhimu kama nyuki manyugwi na sisimizi kabla haijaingia kwenye vyanzo vya Maji na hatimae kwenye chakula na hapo ndio tunakutana na saratani ya kila aina

The food chain! Maana ikiingia kwenye maji ikaingia baharini ikaliwa na samaki na samaki akaja kuliwa huku kwetu inakua hatari sana. Halafu DDT ni non biodegradable kwa hiyo inafanya accumulation kwenye food chain. Hata kwenye udongo pia mmea utafyonza halafu sisi tunakuja kula zile kemikali
 
DDT is potentially carcinogenic, wacha tu tulale ndani ya vyandarua na kutumia rungu(spray). Long term effects za DDT ni kubwa sana.
Hizo ni hadithi tu zilizotungwa na watu wa Eugenics baada ya kuona population growth ya Africa na Asia inaongezeka kwa kasi baada ya mbu kuangamizwa, wakashtuka kwamba kumbe malaria ilikuwa inasaidia kucontrol population, ndio wakamlipa mwanasayansi mmoja aandike kitabu kinachoitwa ‘Silent spring’, ambacho kimejaa porojo na hisia tu bila basis yoyote ya kisayansi
 
DDT Inauwa hadi wale wadudu muhimu kama nyuki manyugwi na sisimizi kabla haijaingia kwenye vyanzo vya Maji na hatimae kwenye chakula na hapo ndio tunakutana na saratani ya kila aina
Kwani unapulizia kwenye mizinga ya nyuki, si unafanya selective fummigation, acheni visababu vya ajabu ajabu
 
The food chain! Maana ikiingia kwenye maji ikaingia baharini ikaliwa na samaki na samaki akaja kuliwa huku kwetu inakua hatari sana. Halafu DDT ni non biodegradable kwa hiyo inafanya accumulation kwenye food chain. Hata kwenye udongo pia mmea utafyonza halafu sisi tunakuja kula zile kemikali
Ila kwa South Africa na nchi zingine zilizoruhusiwa hakuna samaki? 😂😂😂😂, hivi mnapata faida gani mnapotoa ubongo kichwani na kujaza funza?
 
Back
Top Bottom