Hivi TTCL hawana kitengo cha marketing?

tutafikatu

JF-Expert Member
Dec 17, 2011
3,307
4,585
Huwa nashindwa kuelewa kampuni kubwa kama hii kila siku inalialia tu. Hakuna marketing kubwa wanayofanya. Hawajajipanga kukamata wananchi wa kawaida. Bundles zao pia ghali ukilinganisha na mitandao mingine. Sijui haya mashirika yamerogwa na nani.
 
Huu ni UGONJWA WA MAJIPU, hapa una wakurugenzi wanaolipwa na serikali kila kitu, wao kazi yao ni kulala tuu na majungu ofisini. MASHIRIKA yetu kama TTCL, NIC, POSTA kutaja machache hayana ufanisi kabisa, wakati potential ya biashara ni kubwa. Mh Rais tumbua haya majipu, na teua watu wenye UPEO kama MCHECHU walete mageuzi. Busness as usual ife.
 
Mkapa alikuwa Sahihi kuuza Mashirika ya Umma. Hapo utakuta TTCL haina hata uwezo hata wa kujiendesha kulipana mishahara inapelekea Hazina wawape mafungu ya ruzuku kila Mwezi. The same case to ATC wakati kama yangeuzwa yasingehitaji ruzuku toka hazina na bado yangelipa kodi. Airtel walitumia resource za TTCL wakati wanaanza leo hii wako mbali kuliko TTCL yenyewe.
 
Back
Top Bottom