Wanadai hii app yao iliyopo google play inaweza kuhack mawasiliano ya mtu. Ila ukisha install wanadai uingize namba unayotaka kufuatilia na kusema wamekamata mawasiliano yake. baada ya hapo wanakudai activation code kwa kulipa 56,000/- kwa tigo pesa. Baada ya hapo unatuma tigopesa message kwenye namba fulani ya Whatsapp ili utumiwe activation code. Wakiisha kutumia hiyo code wanadai ni lazima iunganishwe na kuunganishwa ni 45 elfu. Hivyo, wanadai utume tena hiyo fedha kwa tigo pesa.
Jamaa yangu kawatumia baada ya hapo wamekaa kimya wiki ya 3. Simu zao haziiti na whatsapp hawapo tena.
hebu tusaidiane kuhusu hawa watu inakuwaje.
Katufu
Jamaa yangu kawatumia baada ya hapo wamekaa kimya wiki ya 3. Simu zao haziiti na whatsapp hawapo tena.
hebu tusaidiane kuhusu hawa watu inakuwaje.
Katufu