Hivi 'sites' za serikali za kuhakiki na kukusanya V.A.T zinapatikana maeneo gani?

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,704
36,458
Kwenye income tax ama kodi ya mapato sina shida maana sites zake zimesajiliwa na BRELA pamoja na body mbalimbali. Ni kiasi cha kutazama mfumo tu wanaweza kuelewa ingawa ni zile taasisi kubwa kubwa tu. Sasa kwa hivi vi taasisi vidogovidogo napo kuna changamoto ya aina yake maana ni vigumu kupata uhalisia.

Nipo kwenye hii kodi walaji a.k.a consumer tax au V.A.T ambayo kwa nchi yetu inakusanywa kiholela holela kama kinyesi cha kuku!

Niliwahi kutembelea nchi ya China kwa kweli ukienda let say Guangzhou unakuta ni eneo nyeti sana la kukusanya V.A.T maana bidhaa nyingi sana zinatengenezwa kule na hivyo ni rahisi sana kuepuka kitu kilichotapakaa nchini mwetu "multi -taxation. Kodi hii kwa kule China huimarishwa kwenye manufacturing sites sanasana.

Sasa njoo hapa nchini mwetu. Nakumbuka mwaka juzi mwishoni nilienda sehemu moja kununua kifaa kimoja kikubwa ambapo kodi yake ya VAT ilikuwa kiasi cha Tshs 180000 (ingawa sikuilipa na nitaeleza sababu)
Yule muhindi kwakweli nilijikuta nikimuuliza maswali kadhaa kuwa hilo friji yeye amelipia VAT? Akajibu ndiyo. Nikamwambia sasa unaponipa bei ya bila VAT na bei ya na VAT huku ukinishawishi nichague bei niitakayo wakati na kwa vyovyote vile nilichagua bei ya bila VAT hivyo kukwepa kodi ya serikali ya VAT ya Tshs 180000 je wewe hiyo hela uliyolipia VAT unairejeshaje? Yule muhindi akabaki kujiumauma ila mwishoni nikang'amua kuwa hiyo bei aliyonitajia tayari ina VAT ndani (Angekubali kula hasara? ) hivyo nikijichanganya tu kulipa VAT basi nitampa faida mara dufu na mimi nitakuwa nimeliwa (akili inalipa ). Kwa makusudi kabisa nikakwepa kodi ya VAT ya Tshs 180000 ingawa najua niliilipa maana muhindi alishalipa na bei ya awali alishaitundika humo ndani. Kulipa tena VAT hiyo ni kumtajirisha muhindi huyo (asingeweza kunipa friji bila kuweka hiyo 180000 na faida yake juu)

Sasa nchi yetu ina udhaifu mkubwa sana wa ukusanyaji VAT. Vitu vinalipwa mult VAT kwa kwenda mbele na hii ni kumtajirisha yule mfanya biashara wa Kariakoo na mlaji anaumizwa sana. Kwa mfano umetoa kontena la mafriji Dubai kule tayari kuna manufacturing site ambapo mafriji yote yamelipiwa VAT ndipo yakapakiwa. Hapo ni vigumu sana serikali ya Dubai kukosa kodi ya VAT pia ndiyo maana bei ya bidhaa ni nzuri. Lakini ukishafika hapa Dar ni shida sana kudhibiti huu mfumo holela wa ukusanyaji VAT maana vimashine vya TRA vipo mpaka kwa wauza karanga. Wana-control vipi huu uholela? Kwanini wasingekuwa na sites tofautitofauti ambazo zinatambulika za kukusanyia VAT ili kuepusha kusambaza vimashine vya TRA hadi kwa wauza karanga? Mtu mwenyewe anaweza kumaliza mwezi akapata tu shilingi mbili, hamuoni kuwa mtu wa aina hii kumpa kimashine cha malaki ya hela ni kujipa hasara?

Haya twende kwenye faini za magari unakuta matrafiki watano wapo sehemu moja na kila mmoja na cha kwake! Nini hii? Kwanza ile kodi inayotozwa kwenye fine za magari inaitwaje? Kama watu hawatafanya makosa, vile vimashine vitano sehemu moja si ni hasara tupu? Kwanza kutoza kodi ya VAT kwenye faini za adhabu ni dhambi hata kwa Mungu.Ni ukandamizaji juu ya ukandamizaji maana atakachonunua kwa kurekebisha ubovu wa gari lake tayari analipia tena VAT!

Tuwe na sites maalum kuanzia na manufacturing industries zote tuweke pale vituo vya kukusanya just VAT kwanza ili kuepusha kuweka vimashine kila kona kwa hasara. Then kwenye biashara kubwa kubwa tuweke maeneo maalum ambayo mizigo na bidhaa zote za kutoka sehemu tofauti tofauti zitapitia (excluding zile zilizotoka kwenye manufacturing sites maana tayari zilishalipiwa kodi humo )ili kuepuka kufanya mambo kienyeji.

Faida ya jambo hili ni kuwa consumer atapata vitu kwa bei nzuri na rahisi maana tutaepuka tayari multi VAT plus bei za kuepuka risk zinazowekwa kwenye bidhaa moja.

Pia gharama za vimashine kila kona zitaepukwa maana naona kwa sasa ni maigizo tu kwenye kodi hii ya VAT!
 
One of the sensible thread i have lived to read.
Am humbled you know (In the voice of Le Mutuz)
 
Back
Top Bottom