Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,486
- 30,166
Nianze mada yangu kwa kunukuu Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ya mwaka 1977, ibara ya 18, ambayo inasema hivi "Kila mwanachi atakuwa huru kutoa mawazo yake na maoni hayo hayapaswi kuingiliwa na chombo kingine chochote" mwisho wa kunukuu.
Pili niseme kila mwananchi yuko huru kuihoji serikali yetu kwa kuwa sisi wananchi ndiyo WAAJIRI wa serikali iliyopo madarakani.
Sasa nije kwenye mada yangu ya leo, ni kuwa Rais wetu amekuwa akisisitiza kuwa serikali yake imapiga vita ya rushwa na vita hiyo haitamwangalia mtu aliyetoa rushwa hiyo.
Sasa cha ajabu ni kuwa kauli hiyo ya Rais haionyeshi uhalisia wake kwa kuwa sisi wananchi tunaona kuwa sheria hiyo inawahusu watu wengine peke yake na siyo wateule wa Rais, kwa kuwa ukiwa mteule wa Rais ni RUKSA kutoa rushwa!
Nitaeleza ni kwanini nasema wateule wa Rais ni RUKSA kutoa rushwa.
Wabunge wa upinzani Godbless Lema na Joshua Nassari walitoa picha za video zinazoonyesha namna mkuu wa wilaya ya Arumeru, Alexander Mnyeti, namna alivyohonga madiwani wa Chadema ambao walidaiwa kuwa wamehamia CCM kutokana na kuunga mkono utendaji mkono wa Rais!
Wakati kashfa hiyo ikiwa "mbichi" watanzania walishikwa na bumbuwazi pale mkuu huyo wa wilaya akipandishwa cheo na mamlaka ya uteizi na kuwa mkuu wa mkoa wa Manyara!
Sasa inaonekana wazi kuwa sheria ya rushwa ina "macho" na inaangalia nani kufanya, kama aliyefanya ni mteule wa Rais, RUKSA kufanya na ndicho kilichotokea kwa DC Mnyeti pamoja na kukiri kwake kuwa kweli alitoa rushwa na akaongea kuonyesha kiburi cha madaraka kuwa kama na wao Chadema wanataka kuhonga Ruksa iwahonga madiwani wa CCM!
Sasa kwa watu waliolewa madaraka yao kama CCM hivi sasa dawa yao ni moja tu kuwakataa katika chaguzi ndogo za udiwani zilakazofanyika November 26 mwaka huu.