Hivi serikali hela wanapeleka wapi?

Naja naja

JF-Expert Member
Sep 13, 2016
747
1,454
Wakuu nimekuwa nikijiuliza hili swali mara kwa mara lakini nakosa jawabu kwa kweli

Serikali imekataza safari za nje na taarifa zimetoka kuwa wameokoa zaid ya bilioni900,pia kuna sehemu mbalimbali wamebana matumizi kama vile kupunguza posho za wabunge,kushusha mishahara ,kutoajiri watu ,kupunguza wanafunzi hewa na wafanyakazi hewa,kupandisha kodi nk

Sasa kama wamebana kwa kiasi hiki nilitarajia huduma muhimu kama vile mikopo ya wanafunzi wa vyuo vikuu isingesumbua kabisa lakini hali ni tofauti kabisa wanafunzi wengi tumekosa mikopo hata baada ya kuappeal ikizingatiwa mfano kama mimi nasoma kozi yenye kipaumbele pia nina ufaulu mzuri wa kidato cha sita na kidato cha nne pia lakini nimekosa mkopo

Hivi nikisema bwana yule naye ni fisadi nitakuwa nimekosea??

Maana hela hatujui zinapoelekea
 
Huyu bwana hata simwelewi kbsa. Ameingia kaiharibu hii nchi sasa hiv gharama za maisha zipo juu.
Debe la 23,000 sasa kwa wajinga wataendelea kuimba hapa kazi tu. Huyu bwana kanichafua roho sana. Pesa anatunza za kizazi chake.
Debeb1 la mahindi kwa ng'ombe 3
Twafaaaaaaa
 
Enzi za JK tuliishi kwa kukopa kopa, sasa ni zamu ya kulipa tulichokopa. Acha tulipe madeni, lakini katika kumi, mbili tunaweka akiba kwa ajiri ya viwanda na kampeni.
 
IMG_20170212_063718_032.jpg
baby....

Na bado
 
Enzi za JK tuliishi kwa kukopa kopa, sasa ni zamu ya kulipa tulichokopa. Acha tulipe madeni, lakini katika kumi, mbili tunaweka akiba kwa ajiri ya viwanda na kampeni.
Haswa ngoja tupunguze deni LA taifa hata wazungu wanatusimanga kwa nini sisi kila Siku deni linaongezeka!
 
Wakuu nimekuwa nikijiuliza hili swali mara kwa mara lakini nakosa jawabu kwa kweli

Serikali imekataza safari za nje na taarifa zimetoka kuwa wameokoa zaid ya bilioni900,pia kuna sehemu mbalimbali wamebana matumizi kama vile kupunguza posho za wabunge,kushusha mishahara ,kutoajiri watu ,kupunguza wanafunzi hewa na wafanyakazi hewa,kupandisha kodi nk

Sasa kama wamebana kwa kiasi hiki nilitarajia huduma muhimu kama vile mikopo ya wanafunzi wa vyuo vikuu isingesumbua kabisa lakini hali ni tofauti kabisa wanafunzi wengi tumekosa mikopo hata baada ya kuappeal ikizingatiwa mfano kama mimi nasoma kozi yenye kipaumbele pia nina ufaulu mzuri wa kidato cha sita na kidato cha nne pia lakini nimekosa mkopo

Hivi nikisema bwana yule naye ni fisadi nitakuwa nimekosea??

Maana hela hatujui zinapoelekea
Mfate alipo umulize huku JF hayupo.
 
Back
Top Bottom