Hivi Serikali Haina Watu Wenye Akili Nzuri? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi Serikali Haina Watu Wenye Akili Nzuri?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Haki Yetu, May 13, 2011.

 1. H

  Haki Yetu Senior Member

  #1
  May 13, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 162
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Makosa haya ni mpaka lini? Kwanza tulianza na mabilioni ya kikwete, fedha zikatolewa bila kuweka mfumo mzuri wa kuwafikia walengwa na utoaji wa taarifa za mafanikio ya fedha hizo. Wajinga (kwani sitaki kuwaita wajanja) wakagawana fedha hizo na kuzila, hadi leo hakuna lolote la maana lililofanyika kwa fedha hizo. Tumebaki kimya na hata ukimuuliza aliyezitoa ni watu wangapi wamefaidika nazo nina hakika hata yeye hatakuwa na majibu ya maana.

  Baada ya hapo, tukaja na kilimo kwanza. Hakuna mkakati wowote wa maana uliotayarishwa wa kufanikisha mpango huo. Sana sana ni kelele tu zinazopigwa na wakuu (wanasiasa) kuhusiana na hicho kilimo kwanza. Tunakumbuka zile power tilers kule Kilosa, ni uozo mtupu. Walengwa hawanufaiki na chochote zaidi ya hao wajinga kula kodi za wananchi. Wanasiasa wanakurupuka tu na sera zenye maneno matamu bila ya mpango wowote wa maana kwenye utekelezaji. Hili nalo utaona litakavyoishia........!

  Bado hatujajifunza na wala kusahau tunakuja na mkakati wa kutoa mahindi kwenye maghala ya Taifa na kuwauzia wafanyabiashara kwa bei ya chee ili kupunguza bei ya sembe. Tunarudi pale pale, mahindi yametoka bila ya kuwa na mpango wowote wa maana wa namna ya kuwadhibiti hao wafanyabiashara watakaonunua hayo mahindi. Kwanza wafanyabiashara wameshaanza kutunisha misuli kuwa bei ya sh 500 hailipi. Ni kipi kitawazuia hao wafanyabiashara kununua hayo mahindi na kuyahifadhi kwenye maghala yao? Tunahamisha mahindi kutoka kwenye maghala ya Serikali kwenda kwenye maghala ya wafanyabiashara kwa bei ya kutupa. Tutaona tutayanunua hayo mahindi kwa bei gani sasa!!!!
  HIVI SERIKALI HAINA WATU WENYE AKILI NZURI YA KUPANGA MAMBO KWA UFANISI?????
   
 2. s

  sawabho JF-Expert Member

  #2
  May 13, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,504
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Baadhi ya maeneo Dar es Salaam, kabla ya mahindi haya ya akiba kutolewa bei ya sembe ilikuwa 700/= kwa kilo, sasa hivi ni 800/= hadi 900/= kwa kilo afadhali yasingetolewa!!!
   
Loading...