Wana JF naomba mnisaidie kujua hili kwa uwazi pasipo matusi na kejeli.
Najua wazi kuwa Mengi kuwa mwanachama fulani cha Siasa siyo dhambi wsla kosa, lakini hoja yangu ni pale anapotumia fursa aliyo nayo kutumia vyombo vya habari kukashfu chama tawala, anatoa fursa kwa viongozi wa Chadema kutoa kashfa kwa vyama vingine na kuyapa muda mwingi sana matukano na kejeli hizo, mfano ITV hutangaza habari nyinngi sana za Chadema hususan ni zile za maneno ya wabunge wanaozungumza mambo ya kuiponda Serikali, Pia kuna tukio jingine nalo lilitushangaza Watanzania, Kwanini Mtei alizindua kitabu chake cha "gother to governor" kwenye Hotel ya Mtei? Je tuamini kwamba ni kwa vile wote wanatoka ukanda mmoja? Naomba majibu ya hoja siyo kejeli na matusi.
Sasa wewe ulitakaje?
Inachofanya ITV ndiyo ethics za taaluma ya habari, ya kubalance habari. Kwa maana ya kutangaza habari za CCM, na vile vile kuzipa pia nafasi, habari toka vyama vya upinzani.
Pengine wewe ulichokuwa unataka, kwa kuwa Mengi ana kadi ya CCM, basi hata vyombo vyake, unataka viwe biased, wazi wazi kwa kupendelea CCM.
Taaluma ya habari hailikubali hilo, na ndiyo maana hata Star TV, ingawa mmiliki wake, Anthony Dialo, ni kada mkubwa sana wa CCM na pia ndiye mwenyekiti wa CCM, mkoa wa Mwanza, lakini bado Star TV, angalau inajitahidi tahidi, kubalance habari.
Mtu peke yake ambaye anaushangaza umma wa watanzania, ni Clement Mshana, mkurugenzi wa TBC, ingawa yeye Mshana anajua wazi kuwa TBC ni steshani ya umma, na inaendeshwa na kodi za watanzania wote, wanaccm na wale wa vyama vya upinzani, lakini TBC. inaonyesha upendeleo wa wazi wazi kwa CCM, kiasi cha kudhani pengine chombo hicho kinaendeshwa kwa pesa ya michango, ya wanaCCM peke yake!!