HUU NI UJUMBE NILIOUPOKEA KUTOKA PPF UKINIAMBIA HAWATOI FAO LA KUJITOA(WITHDRAW BENEFIT)
Mfuko wa PPF imezuia malipo ya fao la kujitoa kwa wanachama wa Mfuko kuanzia tarehe 11 Mei 2016. Hatua hiyo ni utekelezwaji wa marekebisho ya Sheria ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na ile ya Mamlaka ya Usimamizi na Uendeshwaji wa Hifadhi ya Jamii nchini(SSRA) iliyopitishwa na Bunge tarehe 13 Aprili, 2012. Kwa sheria hiyo Fao hilo lilifutwa.
Kwa kuwa marekebisho hayo yalisainiwa na Mhe. Rais na kuanza kutumika rasmi kama sheria mwaka 2012 ilikuwa ni lazima kuyasimamisha kwa sababu kuendelea kulipa ni kinyume cha Sheria na ndiyo sababu Mfuko umeyazuia kuanzia tarehe 11 Mei, 2016.
Wanachama wa aina hiyo sasa wanatakiwa kuendeleza uanachama wanapopata ajira au kujiajiri na watapata mafao yao anapostaafu kwa hiari (miaka 55) au kwa lazima (miaka 60) au pale anapopata ulemavu wa kudumu ama ugonjwa.
Kuzuiliwa kwa mafao ya kujitoa kumefanyika ili mwanachama anapostaafu apate mafao bora na yatakayomuwezesha kumudu maisha ya uzeeni jambo ambalo ndiyo dhumuni kuu la Hifadhi ya Jamii.
Aidha, hapo chini ni orodha ya Mafao ya PPF. Tafadhali bonyeza katika Fao husika kwa taarifa zaidi.
Wasalaam