Kutoka kwenye rushwa itakuwa ngumu sana, japo inawezekana. Hii ni kwa sababu rushwa imekuwa sehemu ya maisha ya watu kiasi kwamba mtu ikitokea (ambayo ni mara chache) akapata huduma bila kudaiwa rushwa na wahusika anashangaa. Kwani kupata huduma bila rushwa imekuwa ni jambo geni. Kumbe utakuta mara nyingine mtu anatoa rushwa yeye mwenyewe hata kabla hajatakiwa kufanya hivyo. Kwa hiyo, kunahitajika mapinduzi ya fikra sambamba na kuwachulia hatua za kisheria wala-rushwa.