Hivi nyumbani kwangu KAGERA kuna nini?

KingCobra95

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
2,850
4,850
Nataka niulize, hivi Kagera tuna mizimu ya aina gani? Jimbo langu ni moja ya majimbo masikini sana Tanzania... na mwaka huu cha ajabu tumemrudisha Balozi Kamala bungeni... Assumpta Mshama aliboronga sana tena sanaaaa, ila cha kushangaza mbadala wake Amerudi yuleyule..

Chadema kwanini hamkua serious na hili jimbo? Haya, kule Bukoba Mjini amerudi Lwakatare yuleyule. Kagasheki ni mmoja wa mawaziri wabovu awamu ya nne ila alikua mmoja wa wabunge wazuri sana..

Tibaijuka nae karudi tena, Mwijage nae waziri mzuri mbunge mbovu. 2025 iwe mwisho wabunge kujirudia rudia. Mnatufanya shamba la bibi...

Naweka azma, 2025 naenda kuichukua NKENGE iwe kwa ADC, HATA CCK, LAZIMA HAYO MAJIMBO YARUDI KWA WAZALENDO
 
Tatizo ni elimu elimu elimu mtu anapewa kofia anauza kura yake
 
Wewe ulipiga kura jimbo gani? Nani alishinda? Kagera hawachagui 'wanyamahanga'. Muulize masterwily alikwenda kugombea bukoba mjini akifikia guest. nani akuchague. fikra kuwa jimboni ni site tu ya kuchukulia ubunge haipo tena tz.
 
Mnalia kwa miaka 5 inakuja chance badala muitumie mnapewa kofia na sahani ya mchele mnasahau kila kitu mnagawa mpk vichinjio. Hizo njaa zenu za sku 1 zimewapotezea tena miaka 5 mingine. Endeleeni kupanua midomo.

Na safari hii ndio mtakoma c umeona kule mjengoni jinsi wamekandamiza juzi, mtu hafai kbs sehemu husika lkn wanalazimishia tu. Wanakachukua katoto kachanga kbs wanaacha kwa makusudi kvs watu waliobobea fani. Wanamkoa nani? Hlf wanalia hatusongi mbele tutasonga kwa lipi?
 
Tatizo mnanunulika kwa bei poa, mnauza utu kwa ahadi na chai ya rangi, Tibaijuka alikuwa si wa kurudi bungeni.
 
Back
Top Bottom