Hivi nyie watu Mpoje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi nyie watu Mpoje?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by ngoshwe, Jan 14, 2010.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  Jan 14, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Nimetoka ofisini, nimechoka na naamua kwenda sehemu ya "kinywaji" kujipumzisha kwa masaa kadhaa kabla sijashika njia ya kurejea nyumbani. Karibu na meza niliyokaa kuna jamaa kama saba hivi. Wanawake watatu na wanaume wanne. Inaonekana wameanza "kupata" muda kabla ya mimi kufika pale. Mara mmoja wa wale wanaume anasimama na kuanza kucheza muziki unaopigwa hapo huku akishangilia na kuwatania wenzake na vicheko vinaendelea.

  Ghafla namwona mmoja kati ya wale wanawake anafungua "kipima joto" chake (kibegi cha kuweka kwapani), anatoa kichupa kidogo cha manukato (perfume) na kujipulizia mikononi kidogo na kumfuata yule mwanaume mchangamfu na kupulizia usoni, mh…nahisi labda ni mwanaume wake, lakini bado sikuona mantiki ya kumpulizia kemikali kama ile usoni...kwa kuwa ni jambo hatari sana, na jamaa ali "stop" ghafla furaha yake....

  Hisia zangu zinakuwa kweli kabisa wanajuana, jamaa anamtizama pasipo kusema kitu lakini mara anaanza kufikicha macho kwa nguvu, na inaonekana alidhulika "ki sawa sawa". Hakika nilimwonea huruma, lakini sikuwa na jinsi kuingilia meza yao. Pamoja na hayo,yule mwanamkea aliefanya kitendo hakuonyesha kujali hata kidogo, akawageukia wenzake na kunong'ona nao huku akiminya midomo kumkebehi yule mwanaume kama haana maumivu yeyote. Waliendelea kunywa na kucheka tu na wenzake huku jamaa hali ikilizidi kuwa mbaya. Na nilimwona mwanaume akitoa machozi kabisa!.

  Wale wanaume waliokuwepo pale wakaanza kumlaumu mwanamke kwa ni ni I kamfanyia vile mwenzie. Yule mwanamke akawafokea kwa sauti akisema wasiwaingilie mambo yao, na muda huyo huo akatoka nje na mmoja wa wanawake wenzake. Baada ya dakika chache walirejea huku wote wakicheka pasipo kuonyesha kumjali jamaa kuhusu macho yake.

  Kwa kweli nilidhani kuna maelewano kati yao, lakini baada ya kama dakika kama kumi hivi, jamaa akaonyesha kujisikia vizuri, yule mwanamke akasimama na kumkumbatia kwa staili ile ya kutaka kupiga picha, lakini jamaa akamsukuma kidogo pembeni, kitendo hicho kinamfanya mwanamke akasirike akitoka nje huku akisema kwa nini jaamaa kamfanyia vile mbele ya wanawake wenzie!.Mmoja wa marafiki za yule mwanamke nae akaanza kumkemea jaama akisema kwa nini amefanya vile kwa jambo dogo tu la utani.

  Jamaa akawa ameghazabika sana na akamuuliza kwa hasira yule mwanamke kama yeye anaona alichokifanya mwenzio cha kumpulizia manukano kwenye macho ni kitendo cha kawaida???. Yule mwanamke akajibu, kijeuri tu kuwa mbona hajapofuka, kama ni mbaya!. Mara ugomvi ukaibuka kati ya yule mwanamke (rafiki) na jamaa , kwa hasira jaama na wanaume wenzake watoondoka kimya kimnya.

  Yule mwanamke aliyefanya kitendo cha hovyo akarejea huku anafurahia na bado hakionyesha sura ya kujali alichofanya, lakini alipoona meza yao imebaki na wanawake wenzake tu, akauliza yupo wapi jamaa yake, na alipojulishwa kuwa amekasirika na ameondoka na wanaume wenzake, yule mwanamke akakimbia tena nje kwa kasi lakini akarudi tena ndani huku analia kilio cha mfiwa aliyepoteza mtu muhimu maishani!.

  Alipoulizwa na wenzake kulikoni, akalalama kwa kilio kikubwa kuwa "Boi friend" (yule aliyempulizia "perfume" usoni) ameondoka na amesema hataki tena kumwona kwa kitendo alichokifanya cha kutaka kumpofua macho!.....wale wenzake wakaanza kumbembeleza wakimweleza kuwa jamaa yake ni mtu safi hana neno ila waliomshawishi ni marafiki zake tu…

  Hata hivyo, bado yule mwanamke hakukubali, akatoka tena mbio huku akilia akisema "eti alikua anamtania tu "boy friend" wake, na kwa nini kamfanyia vile wakati mapenzi yenyewe hayana hata mwezi????? Wale wenzake wakabaki kwenye ile meza ambayo wakati huo haikuwa na kinywaji chochote zaidi ya vibegi vyao huku akikonyezana, na kunitizama mimi kwa tabasamu………
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Jan 14, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Vicheche hao.na pombe hawaziwezi.
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Jan 14, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,485
  Likes Received: 19,881
  Trophy Points: 280
  nimekugonga thanks ila nataka useme kuwa alivyokuchekea ww ulifanya nini ? naona hujamalizia hapo mkuu.
   
 4. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #4
  Jan 14, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145

  Mzee mwenzangu wa pori, sie ni walezi tu (nyoka wa kijani)> niliinua mikono hewa na kusema "utukufu juu mbinguni na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia". Bwana wa majeshi mtenda miujiza....
   
 5. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #5
  Jan 14, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,485
  Likes Received: 19,881
  Trophy Points: 280
  Nimekugongea nyingine kama ni kweli.ni mitaa gani ulikuwa?watu wanatafuta hizi bahati.jokin
   
 6. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #6
  Jan 14, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Chacha nkunong'oneze chomo watu wachichikie, baha!, ni hapo tu kwenye baa ya Ntukufu Raichi, Buguruni kwa Malapa kama unakuja Chalifu chamba!....
   
 7. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #7
  Jan 14, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,485
  Likes Received: 19,881
  Trophy Points: 280
  Eeee! aroo.thanks kubwa. hapo nimeshafika usiku wa manane ile kusimamisha gari wakaja watatu.wakatuambia kwanza mtandao wa simu wanatoa kama kawa then kama unap4a peku bei ni ndogo ukitumia gavana bei ni twice yake.tukatoka nduki.even Bible says"kimbia zinaa"
  mkuu thanks hapo sirudi tena hope hakuna
  mwana JF atakaeopoa kifo hapo.love u guys
   
 8. Annina

  Annina JF-Expert Member

  #8
  Jan 14, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 437
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35

  Nyani kumbe aliyoniambia Lizy ni kweli, mi nilidhani ni mbwembwe za kampeni tu... ngoja nipitie upya proposal yako!

  Annina
   
 9. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #9
  Jan 14, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  mmmh, unafyutwa bha!.....
   
 10. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #10
  Jan 14, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,485
  Likes Received: 19,881
  Trophy Points: 280
  Lizy sio muongo..
   
 11. American lady

  American lady Member

  #11
  Jan 14, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 71
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  siku zote mkuki kwa nguruwe ni mtamu lkn kwa binadamu ni mchungu sn.yule sister aliona yy ndiye aliyeonewa sn mwenzie ile sense ya ku feel maumivu ilishaga paralyze akiwa mdogo may be.du tuwe na tabia ya kujaliana siyo wewe tu uharibu hlf wala huoni.mweeee.
   
 12. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #12
  Jan 14, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,485
  Likes Received: 19,881
  Trophy Points: 280
  Utani PM basi kama vipi
   
 13. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #13
  Jan 14, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,355
  Likes Received: 22,217
  Trophy Points: 280
  Ndio maana mi nasema bora upate msichana mwenye sura mbaya kuliko msichana mwenye sura nzuri halafu ni zuzu magic
   
Loading...