Hivi nyie wanawake mtaolewa na nani!? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi nyie wanawake mtaolewa na nani!?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Tegelezeni, Jan 31, 2012.

 1. Tegelezeni

  Tegelezeni JF-Expert Member

  #1
  Jan 31, 2012
  Joined: Dec 31, 2009
  Messages: 268
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwa mujibu wa Takwimu ya mwaka 2002 Tanzania ina idadi ya watu wapatao Milioni 34, na kwa idadi hiyo, idadi ya wanawake ipo milioni 17 na ile ya wanaume ipo Milioni 16. Mpaka hapo kuna ziada ya idadi ya wanawake inayokadiriwa kufikia milioni 1. Hata hivyo inasemekana hadi kufikia mwaka 2010, Tanzania inakadiriwa kuwa na idadi ya watu milioni 40, ambapo idadi ya wanawake inakadiriwa kufikia milioni 22 na ile ya wanaume inakadiriwa kufikia 18. Na katika idadi hiyo ya wanaume milioni 18, kuna zaidi ya asilimia 20 ya watoto wa kiume ambao wana umri chini ya miaka 15 na bado ni kula kulala, achilia mbali wazee wastaafu ambao hawana nguvu za kufanya kazi tena na bila kuwasahau wale wanaume ambao wameamua kuwa mashoga, na pia wagonjwa ambao nguvu zao za kiume zimekwenda harijojo. Ukitoa idadi hiyo unaweza kupata chini ya wanaume milioni 10 tu wanaoweza kuingia kwenye ndoa leo hii.

  Je kwa upande wa wanawake hali ikoje? Kwa uzoefu tu, hebu tuangalie idadi ya vifo vya utotoni. Idadi ya watoto wa kiume wasiomudu kuvuka umri wa miaka 5 ni kubwa ukilinganisha na watoto wa kike, na hata wazee waliostaafu, wanawake ndio wanaoishi umri mrefu ukilinganisha na wale wa kiume. Hata ukitoa wanawake wasagaji na wamama wazee waliokula chumvi nyingi, bado idadi ya wanawake wanaoweza kuingia kwenye soko la ndoa ni kubwa ukilinganisha na idadi ya wanaume. Hata hivyo kiwango cha ukuaji cha watoto wa kike na wale wa kiume kinatofautiana sana, kwa sababu watoto wa kike huvunja ungo mapema ukilinganisha na wale wa kiume katika kubalehe, na hata kushiriki ngono, watoto wa kike huanza mapema ukilinganisha na wale wa kiume.

  Hivyo basi hata kuolewa wanaowahi kuolewa ni watoto wa kike tofauti na wale wa kiume. Wakati wavulana siku hizi huoa wakiwa na umri wa kati ya miaka 30 mpaka 35, wasichana huanza kuolewa wakiwa na umri wa miaka 15 na kuendelea. Hii inaonesha kwamba soko la wanawake katika kuolewa linazidi kuwa na ushindani mkubwa kutokana na idadi yao kuwa kubwa ukilinganisha na idadi ya wanaume hivi sasa. Leo hii iwapo utamuuliza msichana kama yuko tayari kuolewa uke wenza au mitala atakwambia, "over my dead body" lakini akifikisha umri wa miaka 35, unaweza hata kumsikia akisema, "ngoja nitafute hata mume wa mtu nizae naye" lakini akishazaa na huyu mume wa mtu, kisha akamwambia kuwa angependa amuoe, ombi hilo litakubaliwa haraka sana, kile kiapo cha "over my dead body" hakipo tena. Kiapo kitakuwaje na nafasi wakati ushindani umekuwa ni mkubwa!

  Hili jambo liko complex, na ndio maana nawauliza ninyi wanawake hivi mtaoleana nani, maana kila uchao ukienda mahospitalini wanafyatuliwa watoto wa kike wengi ukilinganisha na wale wa kiume achilia mbali wale wanaozaliwa huko majumbani………………… kazi ipo!
   
 2. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #2
  Jan 31, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  kwani maisha ni kuolewa
  kuolewa ni basic need ya human being?
   
 3. tracy

  tracy JF-Expert Member

  #3
  Jan 31, 2012
  Joined: Sep 22, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Ngoja niseme tu kwamba,.umeongelea Tz peke yake,have you thought of the world as a village,sio lazima niolewe na mtz,or black or asian or etc,the list goes on and on..na pia,kuna wale ambao,they simply do not want to get married,ndo maana kuna the marrying type and not,.na trust me,wakati Mungu anaumba binadam,alijua kueka equilibrium yake,.so pia,hata kama wanawake wako wengi,its a challenge kwa mwanaume kujua nani ni wake!..
   
 4. Tegelezeni

  Tegelezeni JF-Expert Member

  #4
  Jan 31, 2012
  Joined: Dec 31, 2009
  Messages: 268
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Labda tu wewe ndio hutaki kuolewa, lakini hata hivyo na-doubt na msimamo wako. Kuna idadi kubwa ya wenzako wanakimbilia kwa waganga wa kienyeji kutaka kuolewa tena hata huo uke wenza pamoja na kwamba wengine ni wakristo wazuri tu ambapo dini hiyo hairuhusu ndoa za mitala.
   
 5. Asnam

  Asnam JF-Expert Member

  #5
  Jan 31, 2012
  Joined: Jan 18, 2012
  Messages: 4,268
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  mmh kuna wazungu,wachina,wajapan,wahindi,waafrica kibao 2 sio lazima kuolewa bongo kaka habari ndo hiyo:lol::lol::lol:
   
 6. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #6
  Jan 31, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Na kwa wanamke wanaooa?
   
 7. Zabibu

  Zabibu JF-Expert Member

  #7
  Jan 31, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  tutaolewa na wanaume
   
 8. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #8
  Jan 31, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Kweli ushindani kwenye soko la wamama unazidi kuwa stiff siku hadi, cha muhimu ni kwamba wapunguze vigezo ili watu wajichukulie jumla :lol::lol:
   
 9. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #9
  Jan 31, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  teh teh MaNung'aemb....yaanaangaka...tehteh
   
 10. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #10
  Jan 31, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Wanaume sio waTanzania pekee, na hata hiyo asilimia ya waTanzania sio wote waowaji na wanawake sio wote wanaotaka kuolewa.
   
 11. nitonye

  nitonye JF-Expert Member

  #11
  Jan 31, 2012
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 7,167
  Likes Received: 508
  Trophy Points: 280
  Watajioa wenyewe sisi kazi yetu ni kuzalisha tu kama watataka haya kama hawataki haya maisha yanazidi kusonga mbele
   
 12. Tegelezeni

  Tegelezeni JF-Expert Member

  #12
  Jan 31, 2012
  Joined: Dec 31, 2009
  Messages: 268
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Pamoja na hiyo equilibrium unayioizungumzia, hivi huoni jinsi wanaume wanavyowashikisha adabu wanawake na bado wanang'ang'ania tu kuwaganda kama luba! na hao wanaume wa mataifa mengine ulioyataja, kwani kwao hakuna wanawake, kama ingekuwa ni rahisi kiasi hicho basi si mngeolewa. wakati unasema kuwa wapo wanawake ambao hawapendi kuolewa, lakini ukumbuke kuwa wanaumia ndani kwa ndani ni vile tu hawasemi. Kwa taarifa yako wanatamani sana kuolewa ni vile tu hawawezi kusimama hadharani na kupiga mayowe.
  Ukianagalia ndoa nyingi wanaozifanya zidumu ni wanwake na wanaume hawana muda huo, wao wanajua kuoa tu lakini jukumu la kulinda ndoa na kunyenyekea ni kazi ya mwanamke. unajua ni kwa nini? ni kwasababu wanwake wanajua kwamba ndoa ikivunjika ni wao wamepoteza na sio wanaume!
   
 13. Tegelezeni

  Tegelezeni JF-Expert Member

  #13
  Jan 31, 2012
  Joined: Dec 31, 2009
  Messages: 268
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  wanajifanya tu kubisha lakini wenyewe wanajua ni kiasi gani soko lao la kuolewa lilivyo na ushindani. Siku hizi wao wenyewe wanalazimisha kuwa nyumba ndogo unajua sababu? wako wengi na sisi tuko wachache.
   
 14. Digna37

  Digna37 JF-Expert Member

  #14
  Jan 31, 2012
  Joined: May 17, 2010
  Messages: 835
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 60
  chinese-man-with-black-african-women-03-560x530.jpg chinese-man-with-black-african-women-01.jpg chinese-man-with-black-african-women-15.jpg
   
 15. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #15
  Jan 31, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 338
  Trophy Points: 180

  u ar very right tracy
   
 16. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #16
  Jan 31, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 338
  Trophy Points: 180
  sura lako bayaaaaa
   
 17. NYENJENKURU

  NYENJENKURU JF-Expert Member

  #17
  Jan 31, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 1,008
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kweli..Ukiwa na hamu na ile kitu unatangaza kwenye JF au FB unapata wakukupoza then unaendelea na issue nyingine..
   
 18. EBENEZA MT

  EBENEZA MT JF-Expert Member

  #18
  Jan 31, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 264
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
 19. Digna37

  Digna37 JF-Expert Member

  #19
  Jan 31, 2012
  Joined: May 17, 2010
  Messages: 835
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 60
  Chagua tu mwenyewe, dunia duara.

  chinese-man-with-black-african-women-02-560x719.jpg chinese-man-with-black-african-women-04-560x373.jpg chinese-man-with-black-african-women-05-560x419.jpg
   
 20. tracy

  tracy JF-Expert Member

  #20
  Jan 31, 2012
  Joined: Sep 22, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  kwanza,angalia hao wanawake wanaong'ang'ania wanaume ni wa aina gani(hawajaijui thamani yao)regardless the social status...pili,refer to lizzy's thread ya mwanamke kamili,..tatu,refer tena to the thread ya mwanaume kamili,usione unang'anga'niwa na wanawake ukafkiri we kidume kaka,there is more to know than what reaches your eyes,ni sawa na msichana anaefwatwa sana..so,equilibrium ya mungu itabaki pale pale.
   
Loading...