Naungana na Rais Magufuli watoto wanaopata ujauzito wasimamishwe masomo

MJ Ryoba

Member
Jun 11, 2017
47
61
1. Mwanafunzi wa kike ukiacha aendelee na masomo vipi kuhusu huyu wa kiume aliempa mimba kwanini yeye asimamishe masomo na ikiwezekana afungwe? Labda tukubaliane kuwa wote wawili wasifanywe chochote inamaana hapo tumeruhusu ngono mashuleni, shule zitakuwa kiwanda cha kutotolesha watoto, ukimpeleka binti yako shule umempelekea mke mvulana flani hapo shuleni je tutaiweza hali hii?

2. Majukumu ya kulea au kutunza mtoto pia tuyatungie sheria itakuwa kazi ya nani? Babu au huyohuyo binti? Kumbuka baba wa mtoto atakuwa jela akitumikia miaka yake 30, kama ni kazi ya binti ataweza kusoma na kutunza mtoto? Kwa wazazi tunajua malezi ya mtoto yalivyo gharama hivi mwanafunzi ataweza na bado afanye vizuri kwenye masomo yake? Babu na bibi ndio watunze mtoto? Watawezea wapi kama karo ya 20, 000 tu kwa mwaka iliwashinda? Na kwanini wabebe mzigo wa makosa ya mtu mwingine? Haya elimu yetu unaijua ilivyo ndefu inamaana mtoto atamkuta mzazi shule nani atamsomesha huyu mtoto babu au binti mwenyewe? Anatoa wapi pesa ilihali yeye bado mwanafunzi? Au babu aache kusomesha wanawe asomeshe wajukuu na wajukuu wakipata mimba wazae pia? Mnatania nyie.

3. Mzazi anahitaji kwa siku masaa kadhaa kwa ajili ya kunyonyesha mtoto hili ni jukumu la mama pekee hawezi kumwachia mtu mwingine, je mama akienda kunyonyesha masomo yasimame yamsubiri au masomo yaendelee? Tutaongeza miezi ya kukaa shule ili kufidia muda wa mzazi kunyonyesha? Au mzazi akoswe baadhi ya vipindi? Atadai haki ya kusoma vipindi sawa na wengine na akivikosa ufaulu wake utakuwa sawa na huyu asiekuwa mzazi? Haya akirudi jioni nyumbani atakaa kuangalia mtoto atajisomea sangapi?

4. Wanajificha kwenye hoja ya ubakaji eti ooh! Wanabakwa jamani ubakaji ni uharifu kama uharifu mwingine hatuwezi kuharalisha dhambi sababu ya dhambi nyingine. Acha kesi ya ubakaji ishughulikiwe kama kesi ya ubakaji, mbakakaji nje ya mimba anaweza kumuambukiza binti UKIMWI pia basi tuhalalishe na ubakaji ili mubakaji atumie kondom asimuambukize UKIMWI mhanga wa kubakwa! Acheni unafiki in the name of utetezi wa wanawake na watoto mnawaingiza kwenye janga kubwa zaidi ya hili walilonalo sasa.

5. Oooh! Wanatembea mwendo mrefu umbali wa kilomita 7 kwenda shule ndio maana wanapewa mimba na makondakta shame sasa akiruhusiwa kuendelea na masomo ndio umbali utapungua? Kumbuka sasa utaongezeka mara mbili zaidi maana atarudi kunyonyesha sasa hapo ndipo atapata mimba ya mapacha kabisa, hivi mnatumia nini kuwaza jamani ili kuwa 7x2 sasa itakuwa 7x4 umemsaidia au umemuongezea mzigo. Na nikumbushe akifikisha watoto wawili hata umruhusu kusoma hiyo shule itamshinda tu.

Mimi kwa hili naungana na Rais bila wasiwasi kumbuka mimi ni mzazi nina binti wangu pia, nina dadazangu pia, so usijifanye wewe ndio mwenye uchungu sana.

Angalau mtupe mfano wa nchi iliyokuwa hairuhusu baadae ikaruhusu je walifanikiwa au walididimia zaidi? Watoto wetu wasiwe wa majaribio.
 
Raha ya JF kuna uhuru mkubwa wa kutoa maoni haijalishi ya kijinga kiasi gani
 
kwel kabisa mkuu hata wakiendelea na shule hakuna kitu ambacho kitabadilia bora amlee tu mtoto wake afundishe vzur il asirudie makosa kama ya mama ake
 
Kabisa watu wanataka kutumia aliyosema kupiga siasa za kidhaifu, ila hawajui madhara ya haya.

Uamuzi mzuri wa Raisi kuisukuma, ambaye hajamsikia akale raha au iuachia watoto wao wayajue wakiwa wadogo ni wao kwa wao watajiju
 
UMEANDIKA VITU VYA MAANA MKUU.
Inabidi Shule za Msingi na secondary ziwe na Maternity Leave...!!!!!:eek::eek:
Wakimaliza hapo watahamia kwenye ushoga, kwa kigezo hicho hicho kuwa maumbile yalimsababishia.
JPM kaona Mbali...
Utamaduni wetu ni kuhubiri maadili ya mtoto kutokupata Mimba utotoni Huku Vijana wanaowamendea wakishughulikiwa kwa sheria kali.
 
Kuonyesha mmeunga mkono vya kutosha watoto wenu wakipata janga hili msiwasomeshe tena, sawa?
 
Wakae nyumban hawa kwanz mim nasapot tuwe na ule mfumo wazamani wanawake hamna elimu bas,,kwasabab unakuta unampa lecturer ya kutosha bint elimu ya mazingira na elimu ya kuhusu ngono zembe na kufocus ahead ili kutimiza ndoto,,anakwambia kaelewa af within a short period of time anapewa mimba.sasa apo utasema ni mtoto wa under18?au kabakwa na konda wakt anaenda shule??wakae tu nyumban mana ata ada ya serikali ni kod zetu wananchi sas kama tunatoa kod afu wanapata mimba inamana tunasomesha wazaz nasio wanafunzi tena,,asante
 
Hata mm naungana nae sababu akiruhusu wanafunzi watazaa sana...... Na utakuwa upotovu wa maadili zamani binti ukipata mimba anakimbia nyumbani. Na akirudi lazima apeleke wazee wakamwombee msamaha
 
Binti akipata mimba aachishwe shule.

Alaf aliyempa mimba afungwe miaka 30.

Je, huyo mtoto anaezaliwa atalelewa na nani na kwa mazingira gani?

Bila shaka, kama na yeye ni wa kike bas atabeba mimba mapema tu.

Sababu mama yupo tu mtaani baada ya kufukuzwa shule kisa mimba.

Na baba yupo jela kwa kumpa mama mimba!

SOMETHING IS WRONG SOME WHERE!
 
Hili linamlenga nani? Masikini au tajiri?
Likimpata tajiri hali itakuwaje? Na je likimpata masikini khali itakuwaje?
Tutafakari.
 
Wadau wasalamu. Saa zingine tunakosoa lakini kwenye la wanafunzi kupata mimba mlitaka mkuu wa nchi awambie pateni mimba mtazaa na mtarudi shule. Hivi kweli akiwa mtoto wako wa kike utamwambia ukipata mimba mwanangu utajifungua, na utarudi shuleni. Huoni hapo umeruhusu apate mimba? Nyie mnaokosoa mlitaka asemeje?
 
Misingi ya kimaadili na dini yeyoteee ile ni kusubiri na kutopata mimba nje ya ndoa... Magu ktk hili amenyoosha taifa...
Kutwa unakuta mwanaume anaponda single mothers afu yuko hapa anampinga tena Magu....kuna vitu lazma ukweli wake na Misingi iwekwe wazi...mzazi gani anataka mwanae AZAE akiwa under 18???..tujitathmini...ikitokea bahati mbaya basi tudeal nayo...uzazu isiwe fungulia mbwa...uko shule utamlea vipi uyo mtoto na wengi wanatokea familia duni utajikomboa vipi kama hutawekeza ktk elimu kwanza??.
 
1. Mwanafunzi wa kike ukiacha aendelee na masomo vipi kuhusu huyu wa kiume aliempa mimba kwanini yeye asimamishe masomo na ikiwezekana afungwe? Labda tukubaliane kuwa wote wawili wasifanywe chochote inamaana hapo tumeruhusu ngono mashuleni, shule zitakuwa kiwanda cha kutotolesha watoto, ukimpeleka binti yako shule umempelekea mke mvulana flani hapo shuleni je tutaiweza hali hii?

2. Majukumu ya kulea au kutunza mtoto pia tuyatungie sheria itakuwa kazi ya nani? Babu au huyohuyo binti? Kumbuka baba wa mtoto atakuwa jela akitumikia miaka yake 30, kama ni kazi ya binti ataweza kusoma na kutunza mtoto? Kwa wazazi tunajua malezi ya mtoto yalivyo gharama hivi mwanafunzi ataweza na bado afanye vizuri kwenye masomo yake? Babu na bibi ndio watunze mtoto? Watawezea wapi kama karo ya 20, 000 tu kwa mwaka iliwashinda? Na kwanini wabebe mzigo wa makosa ya mtu mwingine? Haya elimu yetu unaijua ilivyo ndefu inamaana mtoto atamkuta mzazi shule nani atamsomesha huyu mtoto babu au binti mwenyewe? Anatoa wapi pesa ilihali yeye bado mwanafunzi? Au babu aache kusomesha wanawe asomeshe wajukuu na wajukuu wakipata mimba wazae pia? Mnatania nyie.

3. Mzazi anahitaji kwa siku masaa kadhaa kwa ajili ya kunyonyesha mtoto hili ni jukumu la mama pekee hawezi kumwachia mtu mwingine, je mama akienda kunyonyesha masomo yasimame yamsubiri au masomo yaendelee? Tutaongeza miezi ya kukaa shule ili kufidia muda wa mzazi kunyonyesha? Au mzazi akoswe baadhi ya vipindi? Atadai haki ya kusoma vipindi sawa na wengine na akivikosa ufaulu wake utakuwa sawa na huyu asiekuwa mzazi? Haya akirudi jioni nyumbani atakaa kuangalia mtoto atajisomea sangapi?

4. Wanajificha kwenye hoja ya ubakaji eti ooh! Wanabakwa jamani ubakaji ni uharifu kama uharifu mwingine hatuwezi kuharalisha dhambi sababu ya dhambi nyingine. Acha kesi ya ubakaji ishughulikiwe kama kesi ya ubakaji, mbakakaji nje ya mimba anaweza kumuambukiza binti UKIMWI pia basi tuhalalishe na ubakaji ili mubakaji atumie kondom asimuambukize UKIMWI mhanga wa kubakwa! Acheni unafiki in the name of utetezi wa wanawake na watoto mnawaingiza kwenye janga kubwa zaidi ya hili walilonalo sasa.

5. Oooh! Wanatembea mwendo mrefu umbali wa kilomita 7 kwenda shule ndio maana wanapewa mimba na makondakta shame sasa akiruhusiwa kuendelea na masomo ndio umbali utapungua? Kumbuka sasa utaongezeka mara mbili zaidi maana atarudi kunyonyesha sasa hapo ndipo atapata mimba ya mapacha kabisa, hivi mnatumia nini kuwaza jamani ili kuwa 7x2 sasa itakuwa 7x4 umemsaidia au umemuongezea mzigo. Na nikumbushe akifikisha watoto wawili hata umruhusu kusoma hiyo shule itamshinda tu.

Mimi kwa hili naungana na Rais bila wasiwasi kumbuka mimi ni mzazi nina binti wangu pia, nina dadazangu pia, so usijifanye wewe ndio mwenye uchungu sana.

Angalau mtupe mfano wa nchi iliyokuwa hairuhusu baadae ikaruhusu je walifanikiwa au walididimia zaidi? Watoto wetu wasiwe wa majaribio.
Hivi umedondoshwa jana hapa nchini? Ipo sheria inayozuia wanafunzi wanaopewa ujauzito kuendelea na masomo na inatekelezwa. Pamoja na kutekelezwa kwake hebu nenda wizara ya elimu ukaone takwimu za wanafunzi wanaopewa ujauzito kwa mwaka! Hili jambo halihitaji mhemko kulishughulikia, bali linahitaji akili iliyotulia!
 
Sikubaliani 100%, hapa naona adhabu kwa binti haiendani na kosa walilofanya, na tunaongelea mabinti ambao umri wao ni mdogo sana ambao mimba sio chaguo lao ila ni bahati mbaya tuu kwa ujumla wanahitaji msaada wa kila hali katika maisha yao sio kuendelea kuwaumiza kwa kuwakosesha elimu , discussing issue hii eti binti apewe elimu au asipewe inaonyesha jinsi society inayoongozwa na Magufuli ilivyo nyuma na katili na watu lazima walipinge hili kwa nguvu zote na huyu zero lazima aambiwe ukweli na sio kila kitu anachosema yeye ni sheria na sio mungu yeye anapita tuu
 
Wadau wasalamu. Saa zingine tunakosoa lakini kwenye la wanafunzi kupata mimba mlitaka mkuu wa nchi awambie pateni mimba mtazaa na mtarudi shule. Hivi kweli akiwa mtoto wako wa kike utamwambia ukipata mimba mwanangu utajifungua, na utarudi shuleni. Huoni hapo umeruhusu apate mimba? Nyie mnaokosoa mlitaka asemeje?
Kwa hiyo mwanao akipata mimba ndio itakuwa mwisho wa haki yake ya kupata Elimu? mambo mengine ya kipuuzi sana
 
Hivi umedondoshwa jana hapa nchini? Ipo sheria inayozuia wanafunzi wanaopewa ujauzito kuendelea na masomo na inatekelezwa. Pamoja na kutekelezwa kwake hebu nenda wizara ya elimu ukaone takwimu za wanafunzi wanaopewa ujauzito kwa mwaka! Hili jambo halihitaji mhemko kulishughulikia, bali linahitaji akili iliyotulia!
Sidhani kama mimba mashuleni ndio sababu pekee watoto wakike kukatusha masomo wengi sana wanafeli masomo na wengine kuolewa, nimesoma sekondari pia wanafunzi walioshindwa kufika advance kwa sababu ya mimba ni wawili tu lkn zaidi ya nusu ya dalasa walifeli kidato cha nne kwenda advance, kangalie takwimu waliopata mimba ni wangapi na waliofeli mtihani ni wangapi? Utagundua mimba si tatizo kubwa kama tunavyojidanganya, tushughulikie kwanza kinachosababisha wanafeli sana.
 
Back
Top Bottom