Hivi nyie kina dada mna nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi nyie kina dada mna nini?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by TAITUZA, May 7, 2011.

 1. T

  TAITUZA Member

  #1
  May 7, 2011
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 94
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani inanishangaza, hii si mara ya kwanza kuliona na leo nimeamua kulivalia njuga. Jamani hebu liangalieni hili, utakuta mwanamke, mdada bado hakubahatika kuolewa na ukimfuatilia kwa undani utagundua ana kazi yake nzuuuuuuri tuu,ila hana cha boyfriend wala fiancee. Cha ajabu kila cku anajivalia pete ya ndoa tena ya gharama kubwa,tena wakati akitembea anaurusha ule mkono wenye pete kwa maringo makubwa ili kila apishanaye aione. Hivi hamuoni kama hii ni kutaka kujipotezea bahati ya kuolewa au? Au wana jf mnalizungumziaje hili?
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  May 7, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Unaposema anajipotezea bahati ya kuolewa kwani anakua amekwambia anataka kuolewa??Unajuaje kama havai kwasababu hiyo hiyo kwamba hataki ndoa hivyo anavaa ili wamtambue kama mke /mchumba wa mtu??Au unajuaje kama havai ili awavutie wale wanaopenda wake za watu??Hapo anapata mahusiano yasiyo na ulikua wapi au kwanini simu unazima usiku!!Kabla hujajua kwanini mtu anafanya kitu ambacho sio uasi wa aina yoyote ile chunguza sababu kabla ya kumhukumu!
   
 3. daughter

  daughter JF-Expert Member

  #3
  May 7, 2011
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 1,275
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ngoja wanaovaa hizo pete waje watwambie. As for me naona sababu inaweza kuwa, 1.Desperation 2. Kujikatia tamaa 3. Hapendi kuolewa so hataki usumbufu and so on and on
   
 4. daughter

  daughter JF-Expert Member

  #4
  May 7, 2011
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 1,275
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  kweli Lizzy,kuna mwingine hapendi kumilikiwa,kuwa under control ya m2 so bora awarushe tu kwa pete ili ata ukiwanae ujione mwizi which means utakuwa na limit kwenye mipango/ratiba or maamuzi yake
   
 5. Wit

  Wit JF-Expert Member

  #5
  May 7, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 417
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu umeuliza kwa ukali kweli,sasa umejuaje kuwa hao dada zetu wako hivyo au ulitafiti? na kama ulitafiti kwanini hukuwauliza sababu za wao kufanya hivyo?
   
 6. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #6
  May 7, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,476
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Kwani kuolewa ni kumilikiwa?
   
 7. daughter

  daughter JF-Expert Member

  #7
  May 7, 2011
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 1,275
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  obvious, how else can u explain it? Unaweza kutuoa watatu lakini siwezi kuolewa na wawili. Which means kuoa ni kumiliki na kuolewa ni kumilikiwa.
   
 8. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #8
  May 7, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Kuepuka usumbufu. Unajua kuna baadhi ya wanaume wakiona mdada ana pete ya ndoa wanamwogopa na kumpa heshima kama mke wa mtu.
   
 9. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #9
  May 7, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  nimejaribu kutafuta kwenye biblia andiko linalohusu pete za ndoa au engagement rings kama muitavyo lkn cjafanikiwa kuona!!!

  hivyo basi kwangu mimi hata kama nikivaa nikama urembo tu!!! kama vile nivaavyo hereni, mkufu au urembo mwingine.

  mambo mengine ni maandaliyo ya moyo tu ya mwanadamu!! kwani nyie mnavyotoga masikio na kusuka mnataka nini lakini??
   
 10. MUREFU

  MUREFU JF-Expert Member

  #10
  May 7, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 1,230
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  kuvaa pete co tatzo asilimia kubwa ya watu wa namna hii huwa hawapend kufuatiliwa kimaisha na wanapenda kuwa huru muda wowote hvyo kuvaa pete ya ndoa inawapa mwanya wa wao kufanya kile wanachokiweza au kukipenda so haina tatzo ila tatzo linakuja kujua ni nan mke watu na nan cye. Dah! Kwel wanaume kaz 2nayo
   
 11. Wit

  Wit JF-Expert Member

  #11
  May 7, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 417
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Well stated super dear,hizi pete tumejiwekea sisi wanadamu kama alama ya utambulisho au pambo.....kwani watawa wanapovaa pete na hawana commitment za ndoa mwenye thread anawaelewa vipi?
  Twende kule kwenye colour reflection tukatete
   
 12. CPU

  CPU JF Gold Member

  #12
  May 7, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Una mtazamo na mawazo hasi sana dhidi ya ndoa.
  Kama unahisi au unaona kuna tatizo fulani ktk muundo wa ndoa, elimisha jamii iyafanyie kazi na iondokane nayo kuliko kudhalilisha wanandoa namna hii.
  Achana na mawazo ya kudidimiza ndoa, tubuni njia za kuboresha na sio kubomoa
  Sawa dada angu???
   
 13. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #13
  May 7, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  hapo mwanzo MUNGU alimuumba ADAM , kicha hakamuona ni mpweke ndipo HAWA akaumbwa, Kama HAWA hataki kuolewa huo ni ukatiri kwa ADAMU na kwake na nikinyme cha yeye kuendelea kuishi maana hana faida ya kuumbwa kwake


   
 14. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #14
  May 7, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  sio wote wanaishi kwa kufuata bible , wengi tunaishi kwa kuiga western culture kwa hiyo mimi nadhani unachimba kwenye wrong source.
  JE HUKO TULIKO HIGA HIZO PETE WANAMAANA GANI?

  lakini pia kumbuka kwamba bible ina heshimu tamaduni zetu.

   
 15. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #15
  May 7, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Umenifuharisha kweli ila ukweli ni kwamba kina HAWA wako wengi kwahiyo ni kiasi tu cha ADAMU kuchagua kati ya wale walio tayari kutimiza wajibu wao hapa duniani!!
   
 16. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #16
  May 7, 2011
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ukimfuatilia huyo dada utagundua mengi sana kwake,nijuavyo hiyo ni gear yake ya kupata mabwana kwa mfano ukinikuta naye mimi utakaa mbali ukidhani yule ndo mwenyewe kumbe wapi, na ukijua unaiba huwa na mvuto wake tofauti,huyo ni mtu anapenda kuwa na wanaume tofauti tofauti
   
 17. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #17
  May 7, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  hapo kwenye pink hapo,kuolewa ni bahati? na kuoa je?
   
 18. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #18
  May 7, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,062
  Likes Received: 3,089
  Trophy Points: 280
  Nadhani anayesema pete ya (NDOA) ni urembo yeyote anaweza kuvaa hajui uhalisia wa maana ya ndoa yenyewe na hli nadhani ndo linafanya ndoa za leo zisidumu,maana unapoanza kuhoji na kuidharau taasisi ya ndoa sitegemei kama utakuja kuiheshimu mda wote,siku nyingne pia utahoji kwani ndoa nini bwana?

  hao watawa wenye kuvaa pete halisi za ndoa umewaona wapi?kwahyo kama ulimwona leo ndo role mode wako siyo,

  nachoelewa mie wasichana wamekuwa na vidole ambavyo kila kmoja hutoa tafsiri yake pale knapovalishwa pete,mfano natafuta mchumba,nimeolewa,sina mme/mchumba,sihitaji n.k lakini pia huwa ni pete tofauti kabisa

  Nachokiona kwa sasa,wanawake hawataki tena ndoa,tuseme ukweli,ila pia wanachokichagua ni balaa zaidi maana kwenye magonjwa haya,umaskini huu sie wajomba tuna kibarua,maana anaranda tu,ksho anatoswa na mimba,mtoto akizaliwa anaelekezwa kwa mjomba,mjomba anakuwa baba,akiugua mjomba,daftari mjomba,viatu mjomba,WANAWAKE TAMBUENI NYINYI NI HAWA na kama hamtaki hili maana hata bible inasema naamini katu hamtobaki salama
   
 19. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #19
  May 7, 2011
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Mnazungumzia Biblia pekee, kwani kwenye Quran suala la pete ya ndoa halizungumziwi?
   
 20. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #20
  May 7, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Sasa sindio anaejua atufungue macho!
   
Loading...