Hawa wadudu wanapatikana katika mwambao wa ziwa victoria, huko ndiko humea, wanapokuwa na mabawa husambaa kimakundimakundi pembezoni mwa ziwa, radi ikipiga huruka juu sana kwahofu na husafiri umbali mrefu ili kutafuta sehemu iliyo salama, basi ikitokea wakaona mwezi unaangaza, huruka kuufuata na hatimaye baada ya kufika juu sana, huona mwangaza mwingine kwa chini ambao ni human made, hubadili uelekeo badala ya kwenda katika mwezi huruka hadi katika taa zinazoangaza chini nasi ndo tunapata wasaa wa kuwaokota na kuwatafuna. Kula nyuma wanakuwa wameacha Mayai na tunutu ambavyo navyo baadae huwa ni senene kamili. Kama hakuna kitu chakuwashtua huwa wanatulia tu ndo maana huwa tunawaona misimu ya masika ikikaribia.