Hivi ni siasa au ni weledi mdogo wa Jeshi la Polisi na wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama?

Apr 20, 2017
76
150
Nimesikia kwa mara ya kwanza baada ya ajali ya basi la watoto wa lucky vicent kuwa sasa magari yanayobeba watoto yatakuwa yanakaguliwa haswaa! Hilo lilikuwa agizo la bwana Gambo.

Leo tena nimeskia morogoro nako juhudi hizohizo zinafanyika!

Tatizo ni nini haswa?
Ni siasa ya ulimbukeni wa kufuata matukio au ni kukosa weledi kwa viongozi husika?

Je ni kutaka kutuaminisha kuwa walikuwa hawafanyi ukaguzi kabla ya hiyo ajali?

Trafic police wako kila sku barabarani kumbe walikuwa wanakagua malori tu bila kugusa mabasi ama aina zingine za magari?

Ama leo mabasi yanayobeba watoto yanathamani mara ishirini kuliko mabasi mengne yanayobeba "mbwa" wengne... Au kwenye hayo mabasi ama magari mengne hakuna watoto ikiwa watu wazima hawana thamani sana?

Kwa yanayoendelea nashindwa kujua shida ni nini kwa wahusika... Sasa siliamiamin jeshi la polisi/trafic pamoja na wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama maana inaonekana hawajui wajibu wao bali ni watu wa kufuata matukio tu!
 
MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,729
2,000
Hatupo siriazi hata kwenye elimu bure mpaka tuambiwe fyatueni watoto wengi kwa sababu sasa ni elimu bure ndiyo tunaanza kufyatuana
 
DON

JF-Expert Member
May 6, 2008
910
1,000
Nimesikia kwa mara ya kwanza baada ya ajali ya basi la watoto wa lucky vicent kuwa sasa magari yanayobeba watoto yatakuwa yanakaguliwa haswaa! Hilo lilikuwa agizo la bwana Gambo.

Leo tena nimeskia morogoro nako juhudi hizohizo zinafanyika!

Tatizo ni nini haswa?
Ni siasa ya ulimbukeni wa kufuata matukio au ni kukosa weledi kwa viongozi husika?

Je ni kutaka kutuaminisha kuwa walikuwa hawafanyi ukaguzi kabla ya hiyo ajali?

Trafic police wako kila sku barabarani kumbe walikuwa wanakagua malori tu bila kugusa mabasi ama aina zingine za magari?

Ama leo mabasi yanayobeba watoto yanathamani mara ishirini kuliko mabasi mengne yanayobeba "mbwa" wengne... Au kwenye hayo mabasi ama magari mengne hakuna watoto ikiwa watu wazima hawana thamani sana?

Kwa yanayoendelea nashindwa kujua shida ni nini kwa wahusika... Sasa siliamiamin jeshi la polisi/trafic pamoja na wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama maana inaonekana hawajui wajibu wao bali ni watu wa kufuata matukio tu!
Daladala zote zichekiwe na mikanda itumike inabidi usafiri wote wa umma ufanyiwe uhakiki. Tusikurupuke
 
panda lee

Member
Apr 28, 2017
85
125
Kwahyo mtoa mada ulitaka isikaguliwe,,,,,wew nawe popo kweli ukikosa cha kuposti utaandika ata ujinga kama huu
 
Aleyn

JF-Expert Member
Nov 12, 2011
13,384
2,000
Tatizo shule ya kiaskari, hawa maaskari wetu hawapewi mafundisho mazuri ya nidhamu na weledi wao. Hata akitukanwa tusi askari hapaswi kuonesha hisia zake kiraia kwasababu yeye tayari ameshapewa mafunzo ya kukabiliana na hayo mambo.

Maaskari wa Waafrika wanaona wakishika bunduki basi ndio wapo juu zaidi, mtu pekee ambaye yeye anaamini ataweza kumtuliza ni askari mwenzio ila sio mtu aliyevaa kiraia.

Tukubali tu kuwa Jeshi letu la polisi lina mapungufu ktk utendaji.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom