Hivi ni sawa kumficha mpenzi wako baadhi ya mali unazomiliki?

C Programming

JF-Expert Member
Nov 11, 2011
2,939
2,000
Habari za leo wana JF,

Humu ndani jamani katika pita pita zangu kipindi hiki kuna sehemu nilikutana na mjadala watu wakijadili hili jambo washikaji.

Hivi ni kweli kwa sisi ni sahihi kumficha mpenzi wako baadhi ya vitu unavyomiliki mfano vitu kama nyumba, mashamba, kumficha mshahara wako na vitu vingine vingi ili kuweza kumpima aina upendo aliokuwa kwako wewe.

Kuna wengine wanasema ukiwa na tabia ya kumweleza mpenzi wako kuhusu kila kitu ulichonacho anaweza kukufanyia kitu kibaya au akakufanyia mchezo mchafu akafilisika.

Kuna wengine wanasema ni bora ukawa muwazi maana kuna leo na kesho siku ikitokea wewe haupo unadhani nini kitatokea.

Sasa katika hili lipi bora uwe msiri kwa mpenzi wako au uwe muwazi kwa mpenzi kipi bora.
 

Kyambambembe

JF-Expert Member
Jan 19, 2015
322
500
Inategemea na mtu husika wa kuambiwa lkn sio vizuri saana especially kwa vijana lkn mkiwa watu wazima na mnafamilia nivyema zaidi kwa manufaa ya wototo. NB; Usimwambie mpenzi wako awe wa kiume au wakike utajuta over.
 

Swenailie

JF-Expert Member
Feb 15, 2016
240
250
Mpenzi tu Au mmeshaoana mkawa mke Na mume. Naona kama mmeoana si vyema kumficha Ila kama bado wapenzi hata uchumba bado Ni sahii asilimia Mia kumficha
 

munisijo

JF-Expert Member
Apr 10, 2012
996
1,000
Ndio ni sahihi kabisa kumficha 'mpenzi' lakini usithubu kujaribu kumficha mke/mume ... ni dalili ya tatizo kubwa sana ndani ya NDOA yenu na lazima mwisho ile kwako.
 

ndayilagije

JF-Expert Member
Nov 7, 2016
7,471
2,000
hapa nina maana mpenzi kwanza lakini hata kwa mke pia unaweza zungumzaa
Kama ni wanandoa ambianeni tu,maana kila mmoja ni mrithi wa mwenzake kama akitangulia.kama ni mpenzi tu kujua au kutojua haifanyi tofauti twaweza pendana na malengo yetu yasiwe mamoja.
 

C Programming

JF-Expert Member
Nov 11, 2011
2,939
2,000
Kama ni wanandoa ambianeni tu,maana kila mmoja ni mrithi wa mwenzake kama akitangulia.kama ni mpenzi tu kujua au kutojua haifanyi tofauti twaweza pendana na malengo yetu yasiwe mamoja.
ila unajua shida mpenzi mwengine akishakuona hauko vizuli katika mali na pesa anaweza kukuacha au akagoma kuolewa na wewe hiloo jee
 

C Programming

JF-Expert Member
Nov 11, 2011
2,939
2,000
Kama ni wanandoa ambianeni tu,maana kila mmoja ni mrithi wa mwenzake kama akitangulia.kama ni mpenzi tu kujua au kutojua haifanyi tofauti twaweza pendana na malengo yetu yasiwe mamoja.
lakini pia unajua hata mke pia akijua kama unamiliki mali nyingi anaweza pia kukuondoa duniani
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom