Hivi ni nyie hawa hawa wanandoa au ni wengine?

hakiba

Member
Jun 1, 2021
19
33
Salaam.

Happy saba saba day, Twende kwenye topic, Nimekuwa nikikutana na clips nyingi kwenye youtube channels za ma MC's wa shughuli za harusi na kushudia vile watu wanakiwa wanasherehekea kuingia katika ndoa, promises kibao na mambo kedekede, inshort huonesha kwamba kwamba wako smart couple and etc kitu ambacho kinaweza kukushawishi kwamba na wewe uoe sasa utulie na mmoja😀.

Sasa kutokana na nyuzi nyingi za wanandoa humu hasa kuchepuka wote waume kwa wake imenifanya nikawa najiuliza ni hawa hawa wanandoa tunaowaona kwenye hizi shughuli au ni wa nchi jirani?😕

Yani huwa nikitazama zile speech za wanandoa kwenye sherehe hasa wadada maneno kibao wakichanganya na lile neno lao maarufu kwamba"tukamtumainie mungu katika ndoa yetu " dah napata ukakasi kidogo,ni nyie hawa hawa au ni vivuli vyenu asee?
 
Raha, karaha, utamu usio na mfano, mapenzi ya mwendokasi, vurugu, kutibuana, kusameheana kupendana tena....vyote vinapatikana itategemea wewe unachagua nini katika hayo, karibu sana.
Hata kutengana kwa muda kupo....mnalazana adi lock up afu kesho mnashikana mikono mkitembea, wanashauri achana naye, lakini waaapi siku mbili tu na Mimba juu🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Hata kutengana kwa muda kupo....mnalazana adi lock up afu kesho mnashikana mikono mkitembea, wanashauri achana naye, lakini waaapi siku mbili tu na Mimba juu🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Ewaaaaaaa.....😁
 
Ndoa ni taasisi nyeti zaidi duniani,kila kitu kinaanzia hapo.Familia,ukoo,jamii,taifa na mataifa ni matokeo ya so called ndoa.Tunaoamini kuhusu Adamu na Hawa mpaka kukosea kwao tunaelewa vita kubwa ambayo falme mbili zimekuwa zikitenda kazi duniani, Mwenyezi Mungu anatumia familia kama cell,na shetani ili kutenda kazi kwake kufanikiwe anajua akishika na kuharibu ndoa kila kitu kimeharibika, so he is busy 24/7 akiharibu haijalishi ni ndoa ya Aina gani.shetani kama simba aungurumae hutafuta mtu wa kummeza.Ndoa ni targeted point,sio wote wanaokosea kwenye ndoa wanapenda wafanye makosa,kuna force wakati mwingine nje ya muhusika na kama hakuna stamina ya kimaadili ya Kimungu ni rahisi kukosea.
 
Back
Top Bottom