Hivi ni nani hasa aliyoleta vyama vyingi nchi tanzania?

lendila

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
5,806
4,370
Hivi ni nani hasa aliyoleta vyama vyingi nchi tanzania?

Nauliza swali hili kwa kuwa,kuna baadhi ya wananchi wanatembea wakiwa wazima lkn ndani ya miyoyo yao mioyo yao imekufa na inavuja damu,mashabiki wa ukawa wanaumizwa sana roho zao, roho zao zinavunja damu ndani kwa ndani,mashabiki wa ukawa ni kama vile tumeshauliwa tukiwa hai tunatembea

Nani hasa alileta mfumo huu wa vyama vyingi vya siasa nchini tanzania?
Mfumo huu wa vyama vyingi unatufanya baadhi ya watanzania tuwe tunaumizwa na washindani wetu kisiasa kila siku kwa washindani wetu kutumia nguvu za kijeshi zaidi kuliko ushawishi kwa wananchi

Nani hasa aliyoleta mfumo wa vyama vyingi nchini kwetu tanzania? kufanya siasa ukiwa upinzani kwa sasa unachukuliwa kama mhalifu kwa taifa?

Kwanini tumekubali mfumo ambao hatuhuwezi?
 
Acheni mambo ya siasa chapeni kazi mpaka wakati uchaguzi utakapofika.
 
Mfumo wa vyama vingi katika nchi za kiafrica umeletwa kwa lazima na wazungu , hakuna kiongozi yeyote mwafrica aliyeutaka .
 
Mungu-maana aliwapa wazungu akili za kuweza kututawala toka dunia ilipoumbwa kiuchumi,kisiasa,kijeshi n.k
 
Watu wanatembea wakiwa maiti,vidonda vya uchaguzi bado havijapona vizuri wanazidi tena kuvitonesha
 
Bila Baba wa Taifa si ajabu Tanzania hadi hii leo ingekuwa ni nchi ya chama kimoja. Iliteuliwa Tume na kupita sehemu mbali mbali nchini ili kukusanya maoni ya Watanzania kuhusu nchi kuruhusu mfumo wa vyama vingi. Hitimisho la maoni yaliyokusanywa na tume ile lilionyesha kwamba Watanzania kwa silimia kubwa hawataki mfumo wa vyama vingi kwa sababu vitaleta mfarakano nchini na hata kutugawa Watanzania.

Baba wa Taifa akasema kwamba kwa maoni yake Tanzania ilikuwa imefikia umri ambao inaweza kuukaribisha mfumo wa vyama vingi bila matatizo yoyote an hivyo hitimisho lile la ile tume likatiwa kapuni na kuanza mkakati wa kuruhusu vyama vingi nchini. Kosa kubwa lililofanyika ni kwamba pamoja na nchi kuruhusu mfumo wa vyama vingi lakini katiba ya nchi iliendelea kuwa ya chama kimoja, katiba ambayo sasa inatumika kuvinyanyasa, kuvionea na hata kuvinyima vyama vya upinzani haki yao stahili ya kufanya shughuli za kisiasa nchini.

CCM haina haki ya wao kujiona kama ndiyo wanastahili kuviamualia vyama vya upinzani lini vikutane na wanachama wao, lini vifanye maandamano na lini vifanye shughuli zao za kisiasa.

Na ukiangalia hali ya nchi kwa sasa wanaoleta vurumai nchini si vyama vya upinzani bali ni MACCM kwa kuhofia kupoteza dola na hivyo kufanya kila aina ya uharamia ili kuvikandamiza vyama vya upinzani.
 
Back
Top Bottom