Habari za jioni wakuu? Shalom!
Rejea kichwa hapo juu, kwa Hakika hakuna kijana anaejielewa anayependa kuingia katika taasisi nyeti ya ndoa kwa njia isiyoeleweka namanisha isiyo rasmi yaani bila kupata baraka za kanisa na wazazi.
Siku za karibuni tumeshuhudia sherehe za kufunga ndoa zikiwa za kufuru unaweza kuta harusi moja inagharimu Tsh. 45 milioni huku bibi harusi akirukaruka na shela lake na kupamba mitandao ya kijamii ili mashoga wajue rasmi kuwa ameshapata mwenza .
Jambo la kushangaza bajeti nzima ya harusi inategemea michango ya kuomba unaweza kuta Bwana harusi na familia yake wanachangia Tsh. 4 millioni kati ya Tsh 45 millioni zinazohitajika.
Binafsi kufanya harusi kwa michango ya kuomba naona kama roho yangu haiafiki natamani mfano nikitaka kuuoa namchukua mwanawali akiwa amevaa nguo zake nzuri sio shela tunaenda zetu kanisani tunafungishwa ndoa iliyopata kibali cha Mungu wa mbinguni baadaye tunaondoka zetu tunaenda kuishi pamoja.
Sasa swali langu, je Mdada unaweza kubali kuingia ndoani bila shela wala 'party' za kuwalingishia mashoga lakini tunaenda kanisani kama kawaida bila kujisikia mnyonge?
NB
Binafsi sipendi mambo ya kusumbua watu kuchangishana.
Naomba kuwasilisha!