Hivi ni lazima kila Mikutano ya Mheshimiwa Rais na Wadau mbalimbali iwe inaonyeshwa Mubashara kwa Umma?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,542
108,877
Nalia sana na Watu walio karibu na Mheshimiwa Rais kwani kuna nchi zingine hapa duniani ukisikia kuwa leo Rais wao anaonekana katika Vyombo vya Habari au anazungumza na Umma ( Wananchi ) wake basi jua ya kwamba kuna Kitu Kizito au Jambo zito linakuja.

Sidhani kama ni sahihi na inaleta Tija kwa Mheshimiwa Rais kila mara au kila Siku tu kusikika au kuonekana hovyo wakati Watendaji wake wa chini wanaweza wakawa wanatekeleza hayo mambo mengine. Hofu yangu tu ni kwamba kuna Siku wa Kuzungumza nao atawakosa na huenda hao Wasaidizi wake sasa wakampangia Kukutana kama Kikao na Makahaba wote wa nchini au hata na Wapiga Punyeto wote ili kuweza Kuwatatulia matatizo yao.

Hebu rudisheni Hadhi ya Taasisi ya Urais tafadhali.

Tujadili.
 
sio lazima ikioneshwa utazame au usikilize kama hupendi kusikiliza au kutazama lakini ni lazima kupata taarifa ya nini serikali inafanya, nini imepanga kufanya na nini imefanya
Kwa Hiyo kujua serikali inafanya nini ni kwa kuonyesha kila siku akiapisha watu?
KARLO MWILAPWA umekuja kasi sana kusifia uvundo na utakuwa wewe ndio uvundo. Take care kijana!
 
Kinachoudhi ni kwamba huwa kuna matukio mazito huwa yanatokea lkn hata siku moja Magufuli hajawahi kujianika kwenye TV kutoa tamko kama rais, watu wengi wamekuwa mapanga, wameuwawa, wametekwa na kupigwa risasi hadharani lin kama rais hajawahi hata kuitisha conference na kuongea na wananchi wake. Anachopenda ni hizi za kujisifia na kutukana watendaji wake hadharani wakati ni yeye ndie anaetoa maelekezo TRA hawawezi kuwabambikia watu kodi kama siyo kwa kupata pressure kutoka kwake. Ni yeye Magufuli ndio anavurunda kwa kutumia pesa za wananchi pacpo kufuata utaratibu halafu lawama anapeleka TRA na baadhi ya watanzania wasiojielewa wanashangalia anapofukuzwa au kushushwa cheo kwa afisa wa TRA. Tatizo siyo watendaji wa TRA, tatizo ni Magufuli pmj na mfumo
 
Akikaa mwezi bila kuonekana utakuja hapa na uzi wa propaganda oooh Magufuli Maji ya shingo, anaona aibu kuonekana kwenye TV,Nchi imemshinda nk.So muache Rais afanye kile anachoona kinafaa imradi havunji sheria au katiba na mambo yake hayaongezi wala kupunguza unga nyumbani kwako.
 
Personally nilishauri Ikulu iwe na station yake ili kuruhusu vipindi vingine kuendelea kama kawaida, kwamfano leo kuna ugeni wa Rais wa DRC, wakati huohuo kuna usomaji wa budget ya serikali, hivyo Ikulu TV ingeendelea kutangaza habari za mgeni na mwenyeji wake na huku TBC ikiendelea na Bunge
 
Kwa Hiyo kujua serikali inafanya nini ni kwa kuonyesha kila siku akiapisha watu?
KARLO MWILAPWA umekuja kasi sana kusifia uvundo na utakuwa wewe ndio uvundo. Take care kijana!
Jaribu kusoma taratibu nilichoandika. kwani zoezi la kuapisha linafanyika lenyewe? si linaambatana na matukio mengine kama kutoa taarifa za serikali yaliyofanyika, yanayohitijika na yatakayofanyika. Jenga hoja katika msingi wa kueleweka, sio huu
 
Akikaa mwezi bila kuonekana utakuja hapa na uzi wa propaganda oooh Magufuli Maji ya shingo, anaona aibu kuonekana kwenye TV,Nchi imemshinda nk.So muache Rais afanye kile anachoona kinafaa imradi havunji sheria au katiba na mambo yake hayaongezi wala kupunguza unga nyumbani kwako.

Sawa Kiongozi.
 
Swali gani hili?, siku hizi mmeanza kuangalia na TBC?

Kama huna cha maana kuleta jukwaani ni bora ukaendelea kuangalia pornography kama kawaida yako
 
TBC wamejua jamaa anapenda kiki hivyo kila mkutano wanarusha live, TV zingine kwa hofu ya kutomuonesha mkuu wanaingia faster kujiunga kuonesha, huoni leo mkuu ameisifia sana TBC kuwa wanafanya kazi nzuri na waendelee hivyo hivyo, kuna mama wa TBC pale ametoa tabasamu kubwa anajua hakuna wa kutumbuliwa. Sasa hivi ni kumfurahisha tu..
 
..... Wasaidizi wake sasa wakampangia Kukutana kama Kikao na Makahaba wote wa nchini au hata na Wapiga Punyeto wote ili kuweza Kuwatatulia matatizo yao.
MASHOGA mtapiga kelele weee lakini sio kwa nchi kama Tanzania!
 
Personally nilishauri Ikulu iwe na station yake ili kuruhusu vipindi vingine kuendelea kama kawaida, kwamfano leo kuna ugeni wa Rais wa DRC, wakati huohuo kuna usomaji wa budget ya serikali, hivyo Ikulu TV ingeendelea kutangaza habari za mgeni na mwenyeji wake na huku TBC ikiendelea na Bunge
Budget utaelezwa na mwakilishi wako!
 
Back
Top Bottom