Hivi ni kweli?

Hivi ni kweli?

LIMANYE

Member
Joined
Nov 16, 2012
Posts
24
Reaction score
1
Nimekuwa nikiona au kusoma post za wana JF mara natafuta mchumba mara natafuta sugar mamii mara natafuta msichana wa kuoa anaejitambua hivi uwa mnapata kabisa na mnafikia malengo ya kuoana nitoeni usingizini mwenzenu bado siamini mapenzi ya kwenye mitandao tena urafiki unaisha mapema nikianzishiwa mada ya mapenzi kwenye mitandao.
 
Mm mbona nimejaribu sikupata...embu waliopata waje hapa
 
Mh mimi najua mapenzi popote humea haijalish ni mtandaoni au niwapi?kuhusu waliopata humu ngoja waje
 
Kweli kuna ugumu kwenye hili. Ugumu unatokana na wasomaji wa hayo matangazo kufikiri kama wewe; kuwa haiwezekani!
Kwenye msafara wa mamba na kenge wapo pia ndio maana humu tupo wenye genuine interest za kupata wenza na wapo vilevile wanaotafuta kukejeli na kuchezea muda wa wengine.
 
Inasemekana zamani kidogo watu walitongozana na kuombana unyumba/uchumba maeneo yafuatayo;-kisimani, ngomani, harusini, machungani, n.k. Maendeleo ya teknolojia yameongeza maeneo ya kukutania, ndiyo kama vile humu JF, facebook, badoo, twitter, n.k.
Ni muhumu kubadilika ili kuendana na matakwa ya dunia. Kalagabaho!!!!!
 
Ukiwa unamaanisha utapata na mutadumu. Maranyingi huwezi kumpata mewnye sifa na vigezo vyako vyote lakini akiwa angalau anaelekeaelekea changamkia fursa mambo mengine mutarekebishana taratibu mwishowe mutakuwa mstari mmoja. Ikishindikana sio lazima. Mbona hata hao wanokutana nyumba za ibada ndoa zingine zinavunjika hukohuko honey moon kabla haijaisha.
 
mh!mwenyewe nataka kupost sasa nimekosa majibu je kweli?hebu tujari tuone kama kweli...
 
Back
Top Bottom