Hivi ni kweli tz inasheherekea miaka 50 ya uhuru? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi ni kweli tz inasheherekea miaka 50 ya uhuru?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by NEW NOEL, Nov 1, 2011.

 1. NEW NOEL

  NEW NOEL JF-Expert Member

  #1
  Nov 1, 2011
  Joined: May 21, 2011
  Messages: 837
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 60
  Kwa sasa serikali ya Tz na baadhi ya wananchi wapo katika pilika pilika za kusherekea miaka 50 ya uhuru wa nchi hii. Lakini kwa mtazamo wangu mimi ninaona bado hatujawa huru.
  Kwa sababu ninachoelewa ni kuwa uhuru ni dhana pana sana. Ebu tujiulize mpaka leo hii tunategemea mataifa ya nje kutubeba kiuchumi. Na mataifa hayo yanatumia matatizo yetu kutunyanyasa. Mfano ni kitendo cha Uingereza kutulazimisha tukubali suala la Ushoga na Usagaji. Mimi nadhani bado tunatawaliwa na ukoloni uliopo sasa ni ule ujulikanao kama 'Ukoloni Mamboleo'.
  Na tazama leo hii Afrika tunapojiona kama wamoja,ili hali hakuna umoja wa kweli katika Afrika. Mfano tazama suala la uvamizi wa Libya. Ni sisi mataifa ya Afrika tulioungana kupinga uvamizi wa mataifa ya nje katika taifa la Libya. Lakini hapo baadae tukasalitiana na kuunga mkono uvamizi ule. Laba tu,nisiende mbali,umeshawahi kujiuliza hivi umoja huu wa nchi za Afrika mashariki ni umoja wa kweli na wa dhati au ni umoja ulioundwa ili kunyonyana? Ninaposema kunyonyana ninamaanisha kuwa,ni umoja ambao upo kwa ajili ya maslahi ya kiuchumi tu na sio kusaidiana na hata kuinuana.
   
Loading...