Chapa Nalo Jr
JF-Expert Member
- Dec 8, 2010
- 7,515
- 6,489
Kwa wakazi wa DSM, na pengine hata miji mingine hapa Tz mtakubaliana nami kuwa hali ya usafi na mpangilio wa matumizi wa maeneo mijini umekuwa shang'ala bhang'ala.
Kwa sasa machinga wanapanga biashara kila eneo lililowazi, wamebana upana wa barabara kwani mali zao zinaingia mpaka barabarani na hivyo waenda kwa miguu sehemu zingine wana share barabara na magari. Sehemu za kupita watu kwa miguu zimechukuliwa na machinga. Vituo vya daladala hamna pa kukaa au kusimama ili kusubiri abiria.
Pembezoni mwa barabara mpya za mabasi ya mwendo kazi nako ni aibu tupu. Wauza machungwa, madafu, maembe, mahindi ya kuchoma, vimshikaki vya 50, waliomwaga nyanya chini na viungo mbalimbali wameachwa wakizichafua hizo barabara na kuondoka.
Mbaya sasa hata yale maeneo ya karibu na Ikulu wameshasogea na usikute muda si mrefu watakuwa wamepanga bidhaa zao lango la ikulu.
Naamini mpangalio katika mji ni muhimu kama vile ilivyo muhimu kupanga vema vitu nyumbani kwako.
Hawa machinga wakiachwa hivyo mpaka wakaji-establish ktk maeneo tajwa hapo juu, basi siku utakapoamua kuwatoa hakika litazuka balaa kubwa.
Kuna maneno yanapita pita huko tukiuliza kuwa eti ni amri ya JPM kuwa eti machinga waachwe wafanye watakavyo. Na tetesi zingine ni kuwa eti iliamuliwa hivyo ili UKUTA ukose waungaji mkono. Sijui sijui sijui. Lakini kwa vyovyote ni bomu kubwa hakika kwa huu mwenendo wa machinga.
Ni rai yangu kama ni kweli hizi vurugu za machinga ni ruksa ya JPM basi namuomba asome angalau maoni yangu haya labda anaweza kuamua vinginevyo kwa heshima ya miji yetu. Mgeni akija kwako aone kweli ni mtu uliestarabika. Uchafu ukizidi utakaribisha machizi kuona ni halali kunya popote. Yaani una ugeni muhimu jijini halafu jiji lote linanuka mavi. Hapana hapana hapana aisee!!!!