Hivi ni kweli kwamba kwenye ndoa mwanamke kapewa kisu kwa upande wa makali? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi ni kweli kwamba kwenye ndoa mwanamke kapewa kisu kwa upande wa makali?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Aug 11, 2011.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Aug 11, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Je umeshawahi kujiuliza ni kwa nini wanawake ndiyo wanao lalamika sana kuhusu ugumu au matatizo ya ndoa kuliko wanaume? Inawezekana ni kwa sababu wanawake ni wakosoaji na wanaotaka zaidi kwenye uhusiano kuliko wanaume, wakati wanaume ni wagumu kutoa?

  Hakuna anayeweza kusema hasa ni kwa nini wanawake ndiyo wanaolalamika na pengine hata kuomba talaka katika ndoa ukilinganisha na wanaume. Lakini kwa kuangalia sababu kuu ambayo mara nyingi ndizo zenye kutajwa sana kama chanzo cha kuvunjika kwa ndoa tunaweza kupata "ati-ati" ya jambo lenyewe.

  Kabla ya ndoa wanandoa huwa na ndoto tamutamu ambazo siyo rahisi katika ndoa. Kwa kuwa tuna hizi ndoto tamu kuhusu ndoa tunapokuja ingia kwenye ndoa na kugundua kwamba tulichokifikiri hakipo ndipo tunapoanza kuvunjika moyo na kujiuliza kwamba ndoa ina maana. Kwa kawaida tunachotarajia kukipata kabla ya ndoa, tunapoingia kwenye ndoa hatukipati na hili huvuruga kila kitu.

  Inaonekana kama matarajio ya wanaume huwa siyo makubwa sana kama yale ya wanawake kabla ya ndoa. Huenda hili huchangia katika kufanya wanaume wasishangazwe sana na kile wanachopambana nacho baada ya ndoa. Inawezekana pia ni kwa sababu wanaume wameshika "mpini" kwenye masuala mengi ya kiuhusiano wakati wanawake wameshika kwenye "makali".

  Kwenye ndoa tatizo la fedha hukera sana. Kila ndoa ina tatizo linalo husiana na fedha au kipato. Ama hakuna fedha za kutosha au kuna fedha nyingi zinazo sababisha kisirani cha aina moja au nyingine. Kama ilivyo kwa matarajio suala la fedha au kipato pia lina sura ileile ya mwanamke kushika "makali" na mwanamume kushika "mpini". Mwanamke hajaweza kumiliki au kumilikishwa kipato na hili humfanya kuwa mwathirika wa migogoro yote ya kifedha au kipato katika ndoa.

  Inabidi wanandoa kujua kwamba ndoa yao haiunganishwi kwa fedha na wala kuwa au kutokuwa na fedha hakuna maana ya kuwa ya furaha au kukosa furaha. Wanachotakiwa kukijua wanandoa ni kwamba wao wameoana ili kuunda familia kwa njia ambayo kipato hakitakuwa na nafasi ya kuwaathiri. Inabidi wajue kwamba hawakuoa wala kuolewa na kipato bali wapenzi wao na kuwepo kwa fedha hakuwezi kubadili mpenzi kuwa "mbaya" au "mzuri". Kushindwa kuelewa tofauti iliyopo kati ya upendo na kipato kunaweza kuwa chanzo cha mgogoro katika ndoa yoyote.

  Mwanaume anaweza kudhani kuacha shilingi laki moja nyumbani kila siku kunatosha kuimarisha uhusiano. Ndiyo maana wanaume wengi huwa wanasema "nampa kila kitu lakini wapi…." Hiyo "kila kitu" kwao ina maana ya fedha na siyo kauli na kusikiliza au kujali. Katika hali kama hii mwanamke ndiye anayeshika kwenye "makali" wakati mwanaume ameshika kwenye "mpini".

  Matatizo ya ndugu au wazazi kuingilia ndoa ni suala lingine linalotajwa sana katika kuvunjika kwa ndoa nyingi. Bila shaka wengi wetu tunajua kwamba mila na desturi zetu (ni potofu, hata hivyo) ndoa inakuwa ni ya ndugu na wazazi pia, siyo wanandoa peke yao. Lakini kwa bahati mbaya sana katika ndoa nyingi ndugu wa mwanaume ndiyo ambao huingilia ndoa kwa kuwasakama wake katika ndoa hizo wanaume wengi hujikuta wakiwaunga mkono wazazi au ndugu zao dhidi ya wake zao.

   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Aug 11, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  very interesting
   
 3. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #3
  Aug 11, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280
  Inaongea mengi na so nice
   
 4. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #4
  Aug 11, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,139
  Trophy Points: 280
  ndoa nyingi siku hz wanawake ndo tumeshika mpini, tumewaweka wanaume mkono, tunawaburuza tutakavyo.
  Tuna mahela, miradi na kazi nzuri, pia tuna mambinu ya KUWABWEGEZA
   
 5. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #5
  Aug 11, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280
  Kwani Nazjaz umeambiwa mapenzi ni pesa au kazi zako nzuri au maisha mazuri
  Mapenzi ni zaidi ya hayo
   
 6. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #6
  Aug 11, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,300
  Likes Received: 22,089
  Trophy Points: 280
  naona hiyo ndio tafsiri yake nazjaz
   
 7. pangalashaba

  pangalashaba JF-Expert Member

  #7
  Aug 11, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 1,079
  Likes Received: 878
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
  unaweza ukakuta hata hujaolewa best na unataka sana but huwapati..
   
 8. MamaEE

  MamaEE Senior Member

  #8
  Aug 11, 2011
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 103
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Naomba kuongeza observations hizi:
  1.Baada ya ndoa majukumu ya mwanamke huwa yanaongezeka sana hasa kwa mila na desturi zetu juu ya matunzo ya watoto. Wakati labda mlikuwa wawili, mama anajikuta analazimika kuhudumia watoto ambao wanamhitaji yeye physically kuliko baba yao. Wenzetu wa ofisini huwa hili ni tatizo inapobidi kuomba likizo za malezi ambazo madhara yake kwa future ya ajira na kupandishwa cheo ni kubwa.
  2. Wanawake in general ni watu wa kuongelea mambo - communicators. Ukisema wanalalamika sana, sishangai maana hata mambo yanapokuwa mazuri wanawake huwa wanasifia wapenzi/waume zao kuliko wanaume...

  Umesema vizuri kuhusu mtazamo kuwa mapenzi sio pesa etc... Nikijaribu kutathmini naona mapenzi ni urafiki wa kudumu. Penye raha na penye shida, kwenye umaridadi na mapungufu.
   
 9. Shantel

  Shantel JF-Expert Member

  #9
  Aug 11, 2011
  Joined: Feb 7, 2011
  Messages: 2,021
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  thanx mkuu for a usefull post
   
 10. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #10
  Dec 11, 2013
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Tupishe watalaamu wa mambo ya jinsia waje wachangie
   
 11. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #11
  Dec 11, 2013
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,223
  Trophy Points: 280
  Asante kwa kitchen party
   
 12. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #12
  Dec 11, 2013
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Tupishe watalaamu wa mambo ya jinsia waje wachangie
   
Loading...