Hivi ni kweli kuwa Bima ya afya (NHIF) ni blank check kwa hospital binafsi?

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,620
1,407
Jamani juzi nilikuwa nimeenda kigoma, nikajisikia vibaya nikaenda kuangalia afya yangu katika kituo cha fya cha Upendo kiko kigoma mjini kwa kutumia kadi yangu ya Bima ya Afya (NHIF)

wakaniambia nina malaria 50 na hivyo niahitaji dawa. daktari aliandika maneno yake akaniambia nipeleke dirisha la dawa.

dirisha la dawa wakaniambia nisaini fomu isiyojazwa gharama za matibabu wanipe dawa.

nikahoji nitasaini vipi wakati haijajazwa gharama za matibabu na kwa mantiki hiyo kopi yangu inakuwa na maana gani?

mtu wa dawa alinijibu hii ni private dawa utapata wasiwasi wako wa kusaini ni nini?

nikamuambia nitasaini vipi wakati fomu haijakamilika?

akamuita mtu mwingine sijui ana cheo gani?

akaja wakanieleza eti utaratibu wa bima ya afya ni usisaini kabla hujapewa dawa lakini wao wenyewe wanaotoa huduma kwa wakati huo hawana idhini ya kujaza fomu hizo na hawazijui bei bali mhasibu ndiye anajaza fomu.

hili swala la hospitali kutojaza fomu za bima za afya kwa wagonjwa na kuwasainisha fomu zisizojazwa nimeliona hospitali nyingi za binafsi.

nilivyokataa kujaza fomu wakaninyima dawa.

baadae nikajiuliza hivi nimekataa kusaini fomu nianyimwa dawa inabidi nikanunue maana nimezunguka kutafuta zahanati ya private inayopokea bima ya fya zijaona.

lakini uzoefu wangu unaonyesha vizahanati vingi vya private vinatumia mtindo huu.

kabla ya hapo nilienda hospitali ya mkoa wa kigoma ya maweni nikapanga foleni masaa matatu bado kuna watu zaidi ya kumi na tano mbele tangu hawajaingia kumuona daktari, mtu mmoja akiingia anatumia kama nusu saa. ingawa watu wa bima ya afya wamepatiwa daktari wao lakini anakuja amechelewa na huduma zinakatisha tamaa.

nikajiuliza hivi hawa wanaotuambia tusisaini sasa baada ya kutosaini nini kinafuata maana rungu wanalolitumia kulazimisha watu kuwapa cheki ambazo nadhani wanakwenda kujaza huduma na gharama wanazotaka wao kwani sahihi mgonjwa kashaweka na hayupo.

hivi NHIF hawajagundua tatizo hili au tunasubiri mpaka mfuko umeshindwa kujiendesha. lakini pia kwa utaratibu huu wenye harufu ya kifisadi utasababisha wateja wa mfuko huu kuendelea kupata huduma mbovu maana watoa huduma wamepewa mwanya wa kujipangia gharama wao wenyewe.

si hoja kwamba mfuko umetoa mwongozo wa gharama bali hoja ni fomu ambayo haijajazwa na kukamilika na kufungwa kwa mtoa huduma kutia sahihi fomu iliyokamilika kunampa nafasi mtoa huduma huyu kujaza huduma ambazo mgonjwa hakuzipata na kuziwekea gharama.

NHIF mtueleze baada ya kukataa kusaini fomu zisizojazwa tukanyimwa huduma tufanyeje maana kiukweli siko tayari kesho kununua dawa eti kwa sababu sitaki kusaini fomu zisizojzwa.
 
mimi sijui ni kwa nini mambo mengi yanayofanywa chini ya serikali yanakuwa supervision ni poor inayopelekea huduma kuwa poor, au taasisi kuendeshwa kwa hasara na kila mara ni kuingiza kodi za wananchi kunusuru au kufilisika kabisa.

kwa nini vitengo vya bima ya afya kwenye government hospitals visiendeshwe kibiashara maana hawa wagonjwa hawalipi fedha zao mfukoni na madaktari waajiriwe na vitengo hivyo, huduma zitolewe kwa ubora na ushindani na sio mfumo wa sasa.

Hilo hata mwananyamala hospital lipo
 
Infact hoja yako ninya msingi sana Ego, na ni haki yako kuwekewa bei ya matibabu kabla huja sign. Sasa ndugu zangu kuna namba ya huduma kwa wateja (unapiga bure) ambayo unapiga na kujibiwa malalamiko yako bure kabisa. Namba hii ni 0800 11 00 63. Mimi pia nimewahi itumia hii number na inafanya kazi na unajibiwa vizuri tuu. Kila la heri waungwana
 
sio NHIF tu bali bima zote za afya imekuwa mkombozi kwa baadhi ya hospitali zimekuwa na uhakika wa mapato,hapo utakuta gharama halisi inazidishwa mara mbili si ajabu kuambiwa umetumia 80000 wakati umekwenda kutibiwa malaria tu
 
Sio kwamba nawatetea watoa huduma ila NHIF hawawezi kulipa kiwango ambacho ni tofauti na makubaliano,,,
So kama unadhan kuwa kule watakapokwenda kujaza gharama watafanya ufisadi, sio kweli
 
Hospitali binafsi wanapenda kutibu wagonjwa wenye BIMA ZA AFYA.wako radhi wadanganye katika kujaza zile form na matibabu waliotoa ili wapige hela
 
Miongoni mwa mbinu chafu za wizi wa mchana kweupe ni pamoja na huo mfuko, imagine mtu anayechangia zaidi ya laki nne kwa mwaka hana mtegemezi mwingine anakwenda hospitali analazimika kutumia dawa walizoziweka wao kwenye mpango wao ikimaanisha kuwa mtu asiye pona kwa dawa hizo basi anatakiwa kwenda kununua kwa gharama yake

Kila siku najiuliza kwanini viongozi wa huu mfuko hawapiti kwenye taasisi wanakotoka wadau wao kusikiliza kero zao?
Kwanini viongozi hao wanatembelea mashangingi ya gharama kubwa huku huduma za afya zikiwa duni?
Hayo mashangingi wanayatumia kwenda wapi kama muda wote hatuwaoni wakija mikoani kujibu kero zetu
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom