Hivi ni kweli kabisa US na N.K wanataka kupigana vita?

Freyzem

JF-Expert Member
Jun 29, 2013
10,113
24,642
Kumekuwa na mijadala mbalimbali kwenye mitandao na vyombo vya habari kuhusu suala la kupigana kati ya Marekani na Korea Kaskazini!
Mataifa haya yamekuwa yakijidai na kuonyesha jinsi yalivyojiandaa kwa chochote na wakati wowote!
Sasa hivi ni kweli kabisa haya mataifa yanataka kudundana? Au ni mikwara tu? Na sababu kubwa hasa ya kutaka kudundana ni ipi au kupigana mikwara ni ipi,? Kwani mataifa haya kama yana mgogoro hauwezi kumalizika kwa njia za kidiplomasia?!!
 
Duniani kuna aina 27 za vita pia Duniani kuna sababu kuu mbili
1 Kulinda Maslai ya kiuchumi au kisiasa
2 Kujilinda dhidi ya uvamizi kutoka nje au ndani

KOREA atapigana kwa ajili ya kujilinda dhidi ya uvamizi kutoka nje ambao ni USA

USA anapigana kwa ajili ya kulinda Maslai yake ya uwekezaji na kiuchumi ndani ya Japan na Korea ya kusini ambapo wamekuwa na hofu juu ya harakati za Korea Kaskazini
 
Hakutakuwa na vita hapo kwa hivi karibuni. Trump amehamishia upepo kuwasahaulisha watu huko kwake mambo hayapo vizuri kuna madudu mengi yamemkalia tenge kuhusu yeye na wasaidizi wake kuna maskandali kibao.
 
Kwa hiyo uonavyo watapigana kweli hawa manjemba?
 
Hakutakuwa na vita hapo kwa hivi karibuni. Trump amehamishia upepo kuwasahaulisha watu huko kwake mambo hayapo vizuri kuna madudu mengi yamemkalia tenge kuhusu yeye na wasaidizi wake kuna maskandali kibao.
Ikiwa huu upepo sababu ndio hiyo basi Trump ni genius!
 
Wachapane kidogo mana vita navyovikumbuka nikiwa na akili timamu ni vita ya Kuwait mwaka 1991 hebu Wachapane hawa tushuhudie tukiwa na akili timamu nini kitaikumba dunia
 
Back
Top Bottom