Somoe
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 754
- 282
Somoe, unaweza kutoa point bila kukandamiza waafrika. Si kila mzungu umuonae ni "interigent".
Anyways, C programming, kwanza si wazungu wote wanaoweza kuenda Harvard wala Oxford. Kwa asilimia kubwa ya population hiyo ni ndoto tu.
Vyuo vingi ughaibuni vina exchange program, yaani unachukua semester moja unaenda nchi ya nje kusomea huku ukijipatia credit kwenye somo fulani. Hii inasaidia kukupa exposure na nchi/utamaduni wa watu wengine, na pia inakupa kitu cha kukutofautisha na wengine kupitia CV.
Mfano classmates wooote mgekuwa na qualifications sawa kwenye CV lakini wewe ukawa una semester moja angalau Kenya, Uganda au Msumbiji kidogo inakufanya u-stand out. Kwahiyo kama una uwezo wa kusafiri au kusomea nje, japo kwa semester moja ningekushauri ufanye.
Samahani, sikuandika kila nzungu umuonae ni interigent.
Ila nimeandika wazungu wanaokuja Afrika wapo very interigent.
Swala la kuponda waafrika kwangu lipo bado pale pale kwa kweli.
Muafika ambao wapo interigent wanakuwa waaribifu, na wanyanyasaji kwa wananchi wenzao.
Na mzungu akija kutoa unyanyasaji, waafrika haipendagi sababu mamlaka yao yatapungua.
Mara nyingi exchange student wa kizungu, wanakuja kufanya observation for research"
Upelelezi kwa mtu flan,au watu flan, kitu flan au vitu flan.
Report watakazo zirudisha zitafanyiwa kazi na wakubwa wao,
Nimesomea nchi moja ya ulaya,
Nakumbuka exchange student wa kizungu walipelekwa India, wakarudisha report ya kusikitisha sana, hadi waziri wa elim wa kizungu aliitwa kuja kusikiliza.
Waziri wa elim wa kizungu alipiga kilio kusikia manyanyaso ya wanafunzi wa kimaskini ya huko India, tena na serikali yao.
Discussion ikaendelea na utaratibu wa kusaidia hao wanafunzi kutoka family masikini ukaanza.
Wakaenda kuwachukua wanafuzi kama 15 waliofukuzwa shuleni, wakamaliza shule vizuri na organization wakaianzisha hapo hapo. Na ilikuwa kila mwaka exchange student wakirudi basi utasikia jipya kutoka nchi furani, na teyari utaratibu wa kuasaidia unaanza, kama si ki pesa, basi hata madawati, au mawazo.
Siku hizi ndio wanapelekaga maloptop na mfumo wa ki IT.
Fikiria unatoka nchi ilio endelea na technologia poa, kila kitu mwananchi umerahisishiwa, unaenda nchi ipo nyuma kimaendeleo.
Ni kama vile unaishi masaki maisha yako yote, alafu unambiwa ili uweze kufaulu mtiani wa mwisho unalazimika ukaishi na watu masikini, kijijini kwenye nyumba za nyasi, mvua inakunyeshea, mbu, maji ya matope, chakula kila siku hiko hiko, usalama barabarani mbovu, watu ufa hovyo kwa magonjwa na ajari, yaani vitu vinavoweza kuzuilika visitoke. Na inabidi ulete report na uelezee njinsi gani unaweza kuwasaidia watu kama hawa ukiwa, mkubwa wa nchi!!!!
Uwezi kuona hata siku moja mtanzania alie ishi masaki maisha yake yote au mtoto wa waziri, akapelekwa vijijini kwa mda kusoma mazingira.
Akili za kiafrika,alie juu hataki kwenda chini. Hivo wakimuona mzungu alie juu anakuja chini wanamshangaa.