Daby
JF-Expert Member
- Oct 26, 2014
- 33,648
- 75,741
Wanaume wengi wangapi wewe mdada wataje waliofanikiwa 10 tuwaone.Sasa kwa nini Mtu asisubiri wakat muafaka ndio waoe?
Wanaume wengi wangapi wewe mdada wataje waliofanikiwa 10 tuwaone.Sasa kwa nini Mtu asisubiri wakat muafaka ndio waoe?
Sawa kabisa mkuu.Bora, kuliko ukose yote
Furaha nitajipa mwenyewe.
Bora kuvumilia vituko vya tajiri.Kwakweli, hawa masikini wenzetu ni vichomi kweli kweli.
Hii inatokana kuwa wakati huna hela wazuri wengi tunawaita mashemeji pia wanawake wanatubagua tukiwa hatuna kitu so tukiwa na mpunga huwa tunatafuta wa hadhi yetu.Nimeona hili kwa Wanaume wengi, mambo yakiwa safi..hakuwa na Gari sasa kawa nalo, hakuwa na Nyumba sasa anayo...basi kifuatacho ni Mamaa mwingine atatafutwa.
kuoa mwanamke wakati bado unatafta hua ni sehemu ya kuwa hauna otherwise, ila unapopata pesa ndipo unamtafta yule alie sahihi!!
Sent using Jamii Forums mobile app
Ukiona hivo hawakupendana mwanaume alikuwa anamtumia huyo mwanamke kwa vile hakuwa na kitu sasa kapata anasahau. Mimi ndo mana sipendi mwanaume maskini wakipata hela ni mwanzo wa familia kusambaratika
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwenye mafanikio ya Mwanaume kuna mkono wa Mke wake.
Hii ndio pointi nilyokuwa najaribu kuionyesha hapa.Hii inatokana kuwa wakati huna hela wazuri wengi tunawaita mashemeji pia wanawake wanatubagua tukiwa hatuna kitu so tukiwa na mpunga huwa tunatafuta wa hadhi yetu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Exactly my point.Nadhani hii inachangiwa zaidi na kuwa mara nyingi tunaoa watu ambao sio tunaowapenda ukizingatia unakuwa hujafanikiwa so kumpata yule unaempenda ni vigumu kidogo ukizingatia wanawake wengi pia hupenda wanaume wenye uwezo, so inapokija umefanikiwa ina maana una uwezo wa kumpata mwanamke yeyote unayemtaka ndo hapo unaanza kumuona/ kujua kama huyu uliyenae ulikosea na sio size yako!!!
Exactly my point.
Na pia kama huna pesa unakosa kujiamini (confidence) ya kumtokea Mwanamke wa chaguo lako na utaishia kukamata unachokifikia kwa wakati huo.
Sasa basi kumbe ipo haja Wanaume washauriwe wawe na subira ili wapate watakacho, tuepushe maumivu kwa wasio hatia.
Na pia Wanawake wa aina hiyo hata kama utafanikiwa kumpata na huna chochote atakuweka roho juu muda wote wa ndoa/mahusiano yenu.changamoto ni kwamba mafanikio huja kwa wakati anaotaka Mungu na sio kwa kupanga sisi japo tunatakiwa kuweka juhudi katika utafutaji, ndo maana kuna wengine wana-hustle sana bado wanakuja kufanikiwa katika age ya miaka 60 so ni ngumu kusema usubiri maana hujui utafanikiwa lini.
kuhusu confidence hii inatokana na ukweli kwamba asilimia kubwa ya wanawake wazuri hupenda kuwa na mahusiano na wanaume waliofanikiwa wakiamini uzuri wao haustahili kwenda kuishi maisha ya shida na mara nyingi huwa na nyodo sana.
NB; Kumbuka pia kwamba kuna kifo so unaweza ukafa kabla hujafanikiwa so wazo la kusubiri mafanikio ndo uoe pia sio sahihi sana!!!
Upo na mwanamke miaka mi5 hajawai kuchangia chochote kwenye maendeleo zaidi ya kutengeneza migogoro hizio na sababu mradi tuu akukwamishe kimaendeleo!....alafu siku nifanikiwe niendelee kukaa nae?
Yani niwe na gari bovu kila siku ni spana mkonani alafu siku nipate pesa ya kununua gari jipya bado niendelee kung'ang'ana na kimeo?
Sent using Jamii Forums mobile app