Hivi ni kwanini Tanzania hatuna board of IT professional kama zilivyo nchi nyingine?

C Programming

JF-Expert Member
Nov 11, 2011
3,011
2,000
Kama zilivyo nchi zingine Africa wataalamu wa fani za computer science, computer engineering, IT software wana association zao ambazo ukimaliza kusoma diploma au degree ni lazima usajiliwe kama mtaalamu ila huku kwetu bongo Tanzania hakuna?

Ila kwa watu wa sheria,accountacy procurement, engineering, doctor na wengine wengi wana bodi zao zinazowatambua lakini pia huweza kuwakutanisha kuzungumza mambo na haki zao kama wataalamu?

Lakini ukienda fani za it na computer science hakuna board wala association of IT PROFFESIONAL ?

IVI NI KWANINI IPO HIVI NI KWANINI IT PROFFESIONALS WASIPEWE HESHIMA ZAO KWA KUWAFANYA WAWE NA BOARD YAO ?
 
Mchizi

JF-Expert Member
Apr 23, 2009
1,934
2,000
Nimesoma Europe nilipo graduate tu nikaingizwa moja kwa moja kwenye Institute of professional engineers.
 
NIMITZ

JF-Expert Member
Aug 19, 2014
287
500
Wazo zuri.fanya kwenda wizara ya sayansi na teknolojia wakupe muongozo wa kuanzisha hicho kitu.
 
Kifaru86

JF-Expert Member
Apr 22, 2017
1,627
2,000
Wataalamu wa IT tatizo bongo wanalala sana wanashidwa kujiongeza.

Kutengeneza madude ya hatari ya hatari nchi kama kenya au nigeria watalaamu wa IT ilivyofikia hatua wakawa wana hack goverment websites, bank accounts, detroying systems ,

Ilifika hatua ilibidi waunde board ya kuwasajili ili watambulike na kuwa monitor maana ilikuwa ni hatari
 
Kifaru86

JF-Expert Member
Apr 22, 2017
1,627
2,000
Wazo zuri.fanya kwenda wizara ya sayansi na teknolojia wakupe muongozo wa kuanzisha hicho kitu.
Ni kweli kabisa mkuu vijana huku wana graduate lakini ndo hivoo

Leo hii wataalamu wa IT hawatambuliki bila kuwa na board yao
 
Joseverest

Verified Member
Sep 25, 2013
44,074
2,000
Nadhani imefikia wakati kwa umoja wenu mpeleke pendekezo lenu mahali husika...itapendeza zaidi
 
kabunguru

JF-Expert Member
Nov 10, 2010
240
250
Sharti Kwanza muanzisha Ka association Ka kuwaunganisha Kwa pamoja;ili kawape negotiation power;pili muweze kudefine nani ni professional,ili asiye na sifa asisajiliwe.Tatu jamii lazima ione umhimu wenu:-[
 
C Programming

JF-Expert Member
Nov 11, 2011
3,011
2,000
Sharti Kwanza muanzisha Ka association Ka kuwaunganisha Kwa pamoja;ili kawape negotiation power;pili muweze kudefine nani ni professional,ili asiye na sifa asisajiliwe.Tatu jamii lazima ione umhimu wenu:-[
Asante sana mkuu nimependa ulivyotambaa ila inabidi hapa muwashilikishe pia na watunga sheria na sera
 
Al-Watan

JF-Expert Member
Apr 16, 2009
11,920
2,000
IT is not hierarchical and it is in many way borderless.

People have their internationally recognized professional certifications.

Bodi ya IT ya Tanzania itafanya nini ambacho hakiwezi kufanyika kimataifa leo?

Unauliza kwanini hatuna printer katika ulimwengu wa email na smartphone?
 
Mkuu issue sio IT wa bongo kutambulika internationally,

Issue IT wa bongo atambulike kwa kazi anazozifanya na kuboresha technologia ndani ya bongo.

Kama ilivyo kwa watu wa phamacy sheria, accounts na procurement mkuuu
 
Kang

JF-Expert Member
Jun 24, 2008
5,290
2,000
Sio kweli kuwa hii kitu ipo nchi nyingi na ambapo ipo mara nyingi sio lazima kwa mfano Marekani ambapo ndo technolojia nyingi zinatoka hakuna.

Hii idea daima nitaipinga inaleta bureaucracy isiyokuwa na ulazima na itawakwamisha watu ambao hawajasome IT kufanya hizi kazi wakati IT ni kitu ambacho unaweza ukajifunza mweneyewe na ukawa bora kuliko aliyesomea.

Na bongo ndo kabisa litaingia tatizo la rushwa na kujuana, hii isiletwe bongo itaangamiza IT kabisa. Kama kuna mtu anahitaji project ifanywe na mtu aliye certified aweke kanununi hizo kwenye project yake mwenyewe.
 
Aliyeshauri jambo hilo sijui kama anaelewa "open system"nature ya IT na umuhimu wa kuwa hivyo ili kuendeleza innovation bila bureaucracy.
 
Al-Watan

JF-Expert Member
Apr 16, 2009
11,920
2,000
Mkuu issue sio IT wa bongo kutambulika internationally,

Issue IT wa bongo atambulike kwa kazi anazozifanya na kuboresha technologia ndani ya bongo.

Kama ilivyo kwa watu wa phamacy sheria, accounts na procurement mkuuu
Nimekuuliza swali hujalijibu. Sifahamu kamahujalielewa au vipi?

Bodi ya IT ya Tanzania itafanya nini ambacho hakiwezi kufanyika kimataifa leo?

Mtu wa IT anajulikana kwa results,sio kwa vyeti vya bodi.

Wewe ukipewa mtu ana cheti cha C Programming lakinihajui ku program,na mwingine hana cheti lakini ni mkali sana wa ku program utachagua yupi?

Pia, mtu ana international certification yake ya CISCO, CISSP etc.

Kashasajiliwa professionally ana international standards.

Unataka asajiliwe na bodi ya kibongo iliiweje?

IT inavunja mipaka ya nchi, mimi niko US, wengine wako Bongo, tunakutana online kwa sababu ya kazi za watu wa IT.

Wewe unataka kurudisha mipaka na kuwapa bureaucrats chance tena!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom