Hivi ni kwanini CHADEMA mnalaumu sana Polisi?

Hivi ni kwanini CHADEMA mnalaumu sana Polisi?

Jibu ni wazi, polis wetu hawatendi haki kwa vyama vya upinzani. Hili sio kosa Lao Bali ni kosa la mfumo.

Polis nikama m...wa wakiambiwa " kamata" wanakamata
 
ukinitaji katika jeshi la polisi kuanzia ngazi ya juu mwenye division 1 form four au 3dvs ntakuelewa kweli huenda polisi wanalaumiwa bure na cdm.uhalisia uko hivi jeshi la polisi linatumikia wanasiasa wa ccm wanasahau wajibu wao kama walinzi wa usalama,wao wakisikia upinzani wanaona wahalifu tu wanatumia nguvu nyingi kwajambo linalo hitaji busara tu..Elimu Elimu Elimu ndio msingi wa taifa hili
 
Ndg subiri yakikukuta hutaamini na utakuwa wa kwanza kufunga kinywa chako.
 
Hapana ndugu yangu unakosea.Ukisema CDM ndio tu wanaolilaumu Jeshi la Polisi sio kweli.Mimi sio CDM na kiukweli sina chama,lakini utendaji wa Jeshi la Polisi unanikera sana.Aisee hawa jamaa noma.Kwanza wanakula rushwa wazi wazi,bila kificho.Yaani ni wote,wala sio traffic tu kama wengi wanavyodhani.Wanatumia shida za watu kujineemesha,mbaya sana na inaudhi sana.

Naomba niwe muwazi, siwasingizii,nimeona mwenyewe first hand.Polisi ambao sio traffic wanaficha tabia yao ya rushwa kwa mtu wasiyemjua kiasi fulani.Wakishakujua na wakawa na uhakika kwamba huwezi kuwafanya lolote hawafichi kabisa.Traffic wao ni mwendo mdundo.Yaani hali ni mbaya sana Jeshi la Polisi.Ni kero kwa wananchi kwa kweli.Jeshi la Polisi Linahitaji mabadiliko makubwa ili kweli liwe jeshi la usalama wa raia.Vinginevyo litabaki kuwa jeshi la kuwapora na kuwaonea raia(JKKR).
Imefikia hata kuwashambulia polisi mmejenga tabia ya mara kwa mara kugombana na polisi kuwatuhumu mnajenga tabia gani au ndio maelekezo ya wafadhili wenu au ndani ya chama kuna watu wana makosa yao ambayo wamawaunganisha na wadau kuwachukia polisi.

Kumbukeni hilo ni jeshi la usalama wa watanzania wote
 
Unatumia njia nzuri sana kufukuzia cheo maana ndio kwanza teuzi hazijaanza. Ila kwa kukujibu swali hili, nakushauri uligeuze uwaulize polisi, wana majibu ya kweli kuliko huu unafiki wako na kujipendekeza
 
Imefikia hata kuwashambulia polisi mmejenga tabia ya mara kwa mara kugombana na polisi kuwatuhumu mnajenga tabia gani au ndio maelekezo ya wafadhili wenu au ndani ya chama kuna watu wana makosa yao ambayo wamawaunganisha na wadau kuwachukia polisi.

Kumbukeni hilo ni jeshi la usalama wa watanzania wote
Mkuu, mtoto wa kambo alipata lini haki?
 
mimi ni askari lakini siwapendi chadema kwa siasa zao za kishamba na vurugu tutawapiga tu.

Kama kweli wewe ni askari basi hufai maana utawezaje kutenda haki kama unamchukia huyu na kumpenda yule
 
Siyo siri hicho chama ni kero na wao wana mtazamo wa ajabu mno,kwamba ukiwa upinzani kila kitu kinachofanywa na serikali ya chama tawala wao watakipinga tu kisa eti hao ni ccm,ipo mifano hai Musoma ikiwa chini ya Chadema miradi mikubwa kama ule wa Maji Bukanga serikali ilitafuta fedha kwa Wafadhili ili kusambaza maji ktk Manispaa pamoja na Musoma Vijijini,siku ya Uzinduzi Chadema waliwakataza watu wao kushiriki sherehe hizo eti hiyo itawapa point CCM,upuuzi Mtupu,haya Sherehe ya Siku ya Wakunga Duniani ilifanyika Kitaifa Musoma Mara,kilichotokea watu waliambiwa hiyo ni Sherehe ya CCM,pamoja na kwamba alikuja rais wa chama hicho duniani,waliojitokeza ni Wakunga peke yao na watoto wa shule,aibu.Wkt wa kampeni za juzi kiongozi wa Baraza la Vijana Chadema aliwajeruhi baadhi ya wafuasi wa CCM akakamatwa na kuwekwa ndani huku majeruhi wakiwa wamelazwa hospitali,Mgombea wa Chadema akakusanya Wafuasi na Wapambe huku akiwaita Makamanda kuwa waende kituoni kumtoa kwa Nguvu kiongozi mwenzao kwa kauli kuwa Polisi wamemuonea,watu zaidi ya elfu wamekwenda kuzingira kituo,mgombea anaulizwa iwapo huyo aliyekamatwa ana Kinga yoyote ya Kisheria ya kutokamatwa,polisi wakachukua nafasi na kukamata wavamizi na pikipiki zaidi ya 30 zilizotelekezwa na hao wahuni,Jee ktk hili watu wangekufa nani angelaumiwa?mgombea kakamatwa na kuswekwa ndani kesho mahakamani,Mgombea bila aibu baada ya kupewa dhamana anaitisha Press Conference ooh polisi wanaonea,polisi wanatumiwa,polisi wametumia nguvu kubwa kuwakamata na kuwabambikizia kesi,kibaya zaidi Waandishi nao hawahoji maswali mazito ili ku-ballance taarifa yao nao wanaingia ktk mkumbo.Hakuna aliye juu ya sheria ndani ya JMT.
 
Imefikia hata kuwashambulia polisi mmejenga tabia ya mara kwa mara kugombana na polisi kuwatuhumu mnajenga tabia gani au ndio maelekezo ya wafadhili wenu au ndani ya chama kuna watu wana makosa yao ambayo wamawaunganisha na wadau kuwachukia polisi.

Kumbukeni hilo ni jeshi la usalama wa watanzania wote

Ndugu ningependa ufahamu jeshi la polisi Tanzania limepoteza ile heshima yake ya kuwa chombo cha kulinda raia na mali zao!.Baada ya polisi kuwa ni chombo cha kisiasa ndio maana unaleta uzi wa kuuliza ni kwa nini CHADEMA wanalaumu polisi.Ukweli ni kwamba polosi sasa ni chombo cha kusimamia maslahi ya chama dola.Mfano mdogo ni pale Ihungo high school .wanafunzi wanapeleka malalamiko yao ya haki polisi wanawapiga mabomu. Hii dhambi kubwa mbele ya Mungu.Sisi wazazi tunalipa kodi ili polisi walipwe mishara na marupurupu; lakini matokeo wananyanyasa raia.
 
Then solution ni kupiga police!!!!!????
 
Back
Top Bottom