magode
JF-Expert Member
- Oct 2, 2014
- 2,204
- 3,337
Wanajamvi,
Heri ya mwaka mpya 2017.
Kuna jambo limekuwa likinisumbua sana akilini mwangu. Kwenye suala la mapenzi na ndoa, kuna hili jambo la fumanizi linapotokea kati ya mwanaume na mwanamke na uamzi unaochukuliwa kwa pande zote mbili.
-Wanawake: Mwanamke anaweza kuwa na mume, mchumba au mpenzi. Katika uhusiano wao anaweza kuwa anashuhudia dalili za kusalitiwa kwa hata 80%, anaweza kukuta sms za wapenzi kwa mwenza wake, au mazingira mengine. Akijaribu kuhoji atapewa uongo wawazi kabisa lakini atauamini na kuendelea na penzi lake.
Anaweza kufumania kabisa mtu wake akiwa kitandani na mtu wake tena kitanda kilekile anacholala yeye anapokuwepo. Atalia hata kuzimia lakini baadae ataanza kujipendekeza na hata kuapa kupigania penzi lake hata kama dalili zote zinaonyesha yeye hatakiwi. Hapa ndo najiuliza huwa kuna nini kichwani mwa wanawake?
-Wanaume: Mwanaume akiwa katika uhusiano na mke, mchumba au mpenzi na ikatokea kafumania hata sms tu ya mwenza wake ikionyesha akijihusisha na mtu mwingine hali huwa ni mbaya sana.
Mwanamke atajitahidi kujieleza lakini kueleweka huwa ni ngumu sana na mara nyingi uhusiano hufikia tamati. Hata ikitokea wakaendelea lakini hilo hubakia tusi kwa mwanamke. Atatukanwa kila aina ya tusi kuonyesha jinsi alivyo malaya.
Wanajamvi kwanini kunakuwa na hii mitizamo isiyolingana? Hivi ni vigumu sana kwa wadada kuwaacha wapenzi wao hata wakiwa na idadi kubwa ya michepuko? Na kwanini wanaume hawana uwezo wa kusamehe wakifumania hata kama na yeye alishafumaniwa akasamehewa?
Nawasilisha.