Hivi ni hujuma kwa Rais Magufuli ama?

Hivi ni hujuma kwa Rais Magufuli ama?

kunena

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2016
Posts
507
Reaction score
721
Mimi kama mtanzania mzalendo kuna mambo nimekua ninayatizama kwa jicho makini toka awamu hii imeshika hatamu.

Rais Magifuli toka ameingia madarakani amejipambanua kama kiongozi makini, mwenye kasi na maono yake kama kiongozi mkuu wa taifa, hivyo tunategemea wasaidizi wake watakua ni watu wa kumsaidia mzee kutimiza maono yake.

Nina mifano michache ambayo inanifikirisha sana juu ya hawa wateule wa rais kama kweli wanatambua wajibu wao ama hawaelewi wafanye nini bali watembelee ‘kiki’ ya Mhe Rais.

1. Sakata la bandarini
Tumekia tukishuhudia mara nyingi madudu ya bandarini kuibuliwa na Mhe Rais na watendaji wengine kuishia kutoa matamka yasiyo kua na kichwa wala miguu. Sasa kwa jambo kama hili tunabaki kujiuliza hivi hapo bandarini si pana watu wanaolipwa mishahara??...sasa iweje rais awasaidie kufanya kazi yao?

2. Dhana nzima ya Uchumi wa viwanda
Rais Donald Trump wa marekani alipoingia madarakani tu alikuja na sera isemayo ‘buy americans, hire americans’ kwa lugha nyepesi sera hii ina promote bidhaa za ndani kwa kuweka kodi kwenye bidhaa zinazotoka nje na kuhimiza wamarekani kutumia bidhaa zao za ndani yaani America first, vilevile waajiri wazingatie sana suala la kuajiri mmarekani kabla ya kumfikiria mgeni.
Mawazo haya amekuja nayo JPM kwa sera ya kuwa na uchumi wa viwanda....uchumi wa viwanda ndio njia pekee ya kututoa hapa na kutupeleka nchi ya uchumi wa kati.
Viwanda vya ndani vipewe mazingira bora ya kufanya kazi ili bidhaa zao ziweze kushindana na zile za nje, uagizaji wa bidhaa za nje ambazo zinazalishwa ndani usifanyiwe lelemama hata kidogo, tunajua sheria ya soko huria na mikataba ya kikanda kama EAC inatubana ila tunaweza kuwa na miongozo yetu ya ndani na kampeni za kuhamasishana kutumia vya ndani ili tujijengee uwezo sisi wenyewe.
Lakini hali ni tofauti, wizara ya viwanda na biashara imelala usingizi wa pono hawajui waanzie wapi na wala waishie wapi, waziri amebaki kuzunguka na Zari the bosslady katika maduka ya bidhaa pale mlimani city....aibu kubwa sana hii....katika zama hizi za ushindani na makampuni ya kibeberu wizara na wataalam wake wangekua ndio ma lobbyist na ma consultant wa makampuni yetu ya ndani katika kupata kazi mbalimbali.

Mathalani wilayani Longido mkoani Arusha wizara ya maji inatekeleza mradi mkubwa wa zaidi ya bilioni saba lakini ukiangalia katika mradi huo mkandarasi anaagiza na kutumia bomba toka nchi jirani Kenya, na kilometa chache toka wilayani Longido kuna viwanda vya watanzania wenzetu vinavyozalisha bomba zenye viwango vya kimataifa. Hatusemi wazawa wapendelewe laa ila tunapaswa kutengeneza namna ya kusaidiana katika mambo kama haya wenzetu wamekua katika mifumo hii ya kibepari kwa muda mrefu wana misuli na weledi wa mbinu za kutafuta fursa, katika uwanda sawa hatuwawezi....’we dont seek for the equality we seek for the equity’.

Jiji la Arusha linakwenda kutekeleza mradi mkubwa wa maji unaogharimu zaidi ya bilioni 400 za kitanzania, kampuni ya SINOHYDRO ya Korea imeshinda zabuni na kuna tetesi anaanza mchakato wa kufanya international tender.....bila kumung’unya maneno kampuni za uchina zitashinda zabuni hii na sisi tukiwa tunaangalia kwa macho wazi, imagine fedha hii aipate mtanzania mwenzetu aingize pesa hii katika mzunguko wetu kwa kulipa wafanyakazi kiwandani, kulipa kodi na expenditure mbalimbali je haitalegeza vyuma??....ni kweli sheria inataka zabuni zinazozidi kiasi fulani cha pesa zitangazwe kimataifa.

Je katika hali ya sasa hatuoni kwamba tuna haja ya kuwalinda wazalishaji wetu wa ndani hata kwa mbinu za ‘medani’ kwani kwa sheria hizi hakika tunawanyonga??....ni wakati sasa tuziangalie sheria ambazo haziwapi fursa wazawa, ingependeza zaidi kama bidhaa ambayo inapatikana nchini ni marufuku kuitangaza katika zabuni za kimataifa.

Ni matumaini yangu wizara husika ya viwanda na biashara na ile maji itafanya kila namna kuhakikisha zabuni hii ya bomba za Jiji la Arusha itafanywa na mtanzani mwenzetu....

TUMSAIDIE MHE RAIS KUIVUSHA TANZANIA YETU.
Wasalaam
Matokeo Chanya+
Sauti ya Mtu aliaye nyikani
 
Pamoja na mipango na baadhi ya mambo ambayo Rais Magufuli anatekeleza katika utawala wake lakini ana upinzani wa ndani kwa ndani ndani ya Serikali yake mwenyewe na ndiyo maana kila siku analalamika baadhi ya maagizo yake au Makamu wa Rais au Waziri Mkuu kutotekelezwa au kuchelewa kutekelezwa kwa wakati na watendaji wa ngazi za juu.

Na hilo liko wazi kabisa kwa jinsi anavyokwenda mahali na kukuta madudu tupu huku akiwa ameshatoa maagizo huko nyuma.

Hapo ndipo kuna la kujifunza kwanini kunatokea hali kama hiyo?
 
hakuna hujuma.
ika nikionacho ni uvivu wako wa kufikiri na kujalibu kumtetea "mshamba" kwa kauli ya Zitto.
1. SGR
how many times zitti kapiga keleke kuwa heka yote inarudi huko ?

2. bombadier na boein
how many times tumesema ndege azinunuliwi cash ?

3. madeni ya ndani
imebaki porojo na siasa tu. inshort hata mafao watu hawalipwi mwaka sasa.
 
Tuache mahaba na kusingixia watu.
 
Muda unaenda. Kama ana wasaidizi ambao hawawezi kumsaidia vizuri si awapige chini?

Mwisho wa siku mambo yasipoenda tutasema Yeye magufuli kashindwa
 
Diamond amekusikia kumbe Zari anazunguuka madukani mitaa ya Mlimani city kwenye msafara wa Ushomile
 
hakuna hujuma.
ika nikionacho ni uvivu wako wa kufikiri na kujalibu kumtetea "mshamba" kwa kauli ya Zitto.
1. SGR
how many times zitti kapiga keleke kuwa heka yote inarudi huko ?

2. bombadier na boein
how many times tumesema ndege azinunuliwi cash ?

3. madeni ya ndani
imebaki porojo na siasa tu. inshort hata mafao watu hawalipwi mwaka sasa.
Stiglers gorge. Umeme wa maji kwenye nyakati ambazo kuna climate varibility/change huwezi kutegemea na kwenda kuweka the hell of money. Mvua ikigoma 2seasons, viwanda na vyote vilivyotegemea huo umeme vitasimama! Where is our natural gas to generate and hence resolve the power issue as once announced?
 
Mimi kama mtanzania mzalendo kuna mambo nimekua ninayatizama kwa jicho makini toka awamu hii imeshika hatamu.

Rais Magifuli toka ameingia madarakani amejipambanua kama kiongozi makini, mwenye kasi na maono yake kama kiongozi mkuu wa taifa, hivyo tunategemea wasaidizi wake watakua ni watu wa kumsaidia mzee kutimiza maono yake.

Nina mifano michache ambayo inanifikirisha sana juu ya hawa wateule wa rais kama kweli wanatambua wajibu wao ama hawaelewi wafanye nini bali watembelee ‘kiki’ ya Mhe Rais.

1. Sakata la bandarini
Tumekia tukishuhudia mara nyingi madudu ya bandarini kuibuliwa na Mhe Rais na watendaji wengine kuishia kutoa matamka yasiyo kua na kichwa wala miguu. Sasa kwa jambo kama hili tunabaki kujiuliza hivi hapo bandarini si pana watu wanaolipwa mishahara??...sasa iweje rais awasaidie kufanya kazi yao?

2. Dhana nzima ya Uchumi wa viwanda
Rais Donald Trump wa marekani alipoingia madarakani tu alikuja na sera isemayo ‘buy americans, hire americans’ kwa lugha nyepesi sera hii ina promote bidhaa za ndani kwa kuweka kodi kwenye bidhaa zinazotoka nje na kuhimiza wamarekani kutumia bidhaa zao za ndani yaani America first, vilevile waajiri wazingatie sana suala la kuajiri mmarekani kabla ya kumfikiria mgeni.
Mawazo haya amekuja nayo JPM kwa sera ya kuwa na uchumi wa viwanda....uchumi wa viwanda ndio njia pekee ya kututoa hapa na kutupeleka nchi ya uchumi wa kati.
Viwanda vya ndani vipewe mazingira bora ya kufanya kazi ili bidhaa zao ziweze kushindana na zile za nje, uagizaji wa bidhaa za nje ambazo zinazalishwa ndani usifanyiwe lelemama hata kidogo, tunajua sheria ya soko huria na mikataba ya kikanda kama EAC inatubana ila tunaweza kuwa na miongozo yetu ya ndani na kampeni za kuhamasishana kutumia vya ndani ili tujijengee uwezo sisi wenyewe.
Lakini hali ni tofauti, wizara ya viwanda na biashara imelala usingizi wa pono hawajui waanzie wapi na wala waishie wapi, waziri amebaki kuzunguka na Zari the bosslady katika maduka ya bidhaa pale mlimani city....aibu kubwa sana hii....katika zama hizi za ushindani na makampuni ya kibeberu wizara na wataalam wake wangekua ndio ma lobbyist na ma consultant wa makampuni yetu ya ndani katika kupata kazi mbalimbali.

Mathalani wilayani Longido mkoani Arusha wizara ya maji inatekeleza mradi mkubwa wa zaidi ya bilioni saba lakini ukiangalia katika mradi huo mkandarasi anaagiza na kutumia bomba toka nchi jirani Kenya, na kilometa chache toka wilayani Longido kuna viwanda vya watanzania wenzetu vinavyozalisha bomba zenye viwango vya kimataifa. Hatusemi wazawa wapendelewe laa ila tunapaswa kutengeneza namna ya kusaidiana katika mambo kama haya wenzetu wamekua katika mifumo hii ya kibepari kwa muda mrefu wana misuli na weledi wa mbinu za kutafuta fursa, katika uwanda sawa hatuwawezi....’we dont seek for the equality we seek for the equity’.

Jiji la Arusha linakwenda kutekeleza mradi mkubwa wa maji unaogharimu zaidi ya bilioni 400 za kitanzania, kampuni ya SINOHYDRO ya Korea imeshinda zabuni na kuna tetesi anaanza mchakato wa kufanya international tender.....bila kumung’unya maneno kampuni za uchina zitashinda zabuni hii na sisi tukiwa tunaangalia kwa macho wazi, imagine fedha hii aipate mtanzania mwenzetu aingize pesa hii katika mzunguko wetu kwa kulipa wafanyakazi kiwandani, kulipa kodi na expenditure mbalimbali je haitalegeza vyuma??....ni kweli sheria inataka zabuni zinazozidi kiasi fulani cha pesa zitangazwe kimataifa.

Je katika hali ya sasa hatuoni kwamba tuna haja ya kuwalinda wazalishaji wetu wa ndani hata kwa mbinu za ‘medani’ kwani kwa sheria hizi hakika tunawanyonga??....ni wakati sasa tuziangalie sheria ambazo haziwapi fursa wazawa, ingependeza zaidi kama bidhaa ambayo inapatikana nchini ni marufuku kuitangaza katika zabuni za kimataifa.

Ni matumaini yangu wizara husika ya viwanda na biashara na ile maji itafanya kila namna kuhakikisha zabuni hii ya bomba za Jiji la Arusha itafanywa na mtanzani mwenzetu....

TUMSAIDIE MHE RAIS KUIVUSHA TANZANIA YETU.
Wasalaam
Matokeo Chanya+
Sauti ya Mtu aliaye nyikani
Nani aliahadi kuendeleza uchumi labda awamu ijayo .sasa hivi nituna nyoosha nchi na chama tuu .mpaka walioishi kimalaika waishi kishetani ,[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Stiglers gorge. Umeme wa maji kwenye nyakati ambazo kuna climate varibility/change huwezi kutegemea na kwenda kuweka the hell of money. Mvua ikigoma 2seasons, viwanda na vyote vilivyotegemea huo umeme vitasimama! Where is our natural gas to generate and hence resolve the power issue as once announced?

Umeme wa gesi ni very expensive hatuwezi kuuendesha wala wananchi kuununua per unit....umeme wa maji ni rahisi kuuendesha na hata kuuza kwa wananchi....stieglers gorge ni suluhisho. Umeme wa gesi ubaki kama back up plan
 
Hee!! Kunena we ufikiri wako ni mfupi sana! Umeme wa maji ni very un reliable kutoka na hali ya Dunia ya sasa na climate change hii, mataifa yaliyoendelea hayategemei huo umeme aisee
 
Go
Nani aliahadi kuendeleza uchumi labda awamu ijayo .sasa hivi nituna nyoosha nchi na chama tuu .mpaka walioishi kimalaika waishi kishetani ,[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23][/QUO
Good thinking
 
Hee!! Kunena we ufikiri wako ni mfupi sana! Umeme wa maji ni very un reliable kutoka na hali ya Dunia ya sasa na climate change hii, mataifa yaliyoendelea hayategemei huo umeme aisee

Hebu soma post yangu vizuri uielewe acha kukurupuka
 
Back
Top Bottom