Hivi ni harali kwa mbunge kuongea na simu bungeni huku kikao kikiendelea | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi ni harali kwa mbunge kuongea na simu bungeni huku kikao kikiendelea

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ptz, Jun 18, 2012.

 1. P

  Ptz JF-Expert Member

  #1
  Jun 18, 2012
  Joined: Aug 23, 2011
  Messages: 466
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 60
  Nimekuwa nikifuatilia kwa ukaribu sana vikao vya bunge letu la Tanzania live kwa kupitia tv. Nimeshuhudia baadhi ya wabunge na mawaziri wakiongea na simu bungeni huku kikao cha bunge likiendelea, ni mara kadhaa nimemshuhudia Mkuchika akiongea na simu na gazeti la mwanachi lilishamtoa kwenye front page picha yake huku akiongea na simu.

  Leo hii nimemshudia Davide Kafulia (mbunge Kigoma Kusini) akiongea na simu huku mzee Cheyo akitoa mchango wake, zaidi ya yote punde baada ya mzee Cheyo(Mbunge wa Bariadi) kumalizia mchango wake, kuna Mbunge wa Mbalali mh Kilufi akichangia kuna mbunge mmoja alikuwa kaketi kushoto kwake ghafla msg iliingia kwenye simu yake, niliisikia msg kwa ringtone ya Nokia, mbunge huyo alichukua simu na kuisoma msg na mara tu baada ya kusoma alionesha tabasamu zito (Source TBC leo saa 11 hadi moja jioni). Kwangu mimi nauita upumbavu. Nimekuwa pia nikifuatilia bunge la Kenya na Uganda, sijawahiona upumbavu huu.

  Ni bunge hili hili kuna mbunge mmoja alishathubutu kughushi hati na saini ya waziri mkuu Mizengo Pinda na kuachwa bila hatua yoyote ile. Je, ni harali kwa tabia kufanywa na hawa watu tunawaita waheshimiwa kuzitumia simu zao wakati wa kikao kikiendelea katika jengo tunaloliita tukufu kwani hata huku uraiani kuna vikao tumekuwa tukivifanya ni kulazimika kuzizima au kutoingia na simu kabisa,

  Kwa mifano ya mabunge ya wenzetu niliyoitaja mfano bunge la Kenya naona kwa Yule spika"sir Kenneth Marende, naibu wake "sir Farah Macalin" upumbavu ninaouona huukwa bunge letu Tanzania si rahisi kuuvumilia kwa bunge la Kenya, nilishashudia waziri akitolewa nje na kupigwa Ban ya vikao vitatu kwa kutojibu swali ipasavyo kwa ushahidi nilionao Bunge la Kenya ni Bunge la Kenya kweli "It's a really Kenyans Parliament" ni vigumu kumjua hata mpinzani au mtawala ni ninani! Nawasilisha.
   
 2. B

  Bob G JF Bronze Member

  #2
  Jun 18, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Haya tumeyataka wenyewe kama hatutaki mambo ya ovyo basi ikatae ccm kwa kuichagua CDM
   
 3. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #3
  Jun 18, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Hiko ni KIJIWE MDAU
   
 4. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #4
  Jun 18, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,127
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Wabunge na viongozi wetu wamejaa mzaha katika utendaji wao. Mtu makini anayetambua umuhimu wake bungeni hawezi kutumia simu. Ni aibu yao na yetu wapiga kura tunaoshindwa kuwawajibisha wabunge wetu. Upuuzi unaofanyika Tanzania katika uongozi haupo mahali popote DUNIANI. Hapa hawara anahongwa cheo na wote tunaishia kuchangia kwa kodi zetu. Mhalifu anapata uteuzi wa Raisi. Ni ajabu na kweli.
   
 5. M

  Moony JF-Expert Member

  #5
  Jun 18, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 1,593
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  halali
   
 6. webondo

  webondo JF-Expert Member

  #6
  Jun 18, 2012
  Joined: Apr 29, 2012
  Messages: 1,724
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 160
  Kwani hakukuwa na kiranja wa kuandika majina???
   
 7. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #7
  Jun 18, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  bunge la kariakoo
   
 8. g

  gati Member

  #8
  Jun 19, 2012
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  naona hujaelewa vizuri hoja ya mtoa mada. Amefafanua vizuri na kutoa mfano hata wa David kafulila( ni CCM?!). Hapa hakuna hoja ya CCM wala CDM.
   
 9. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #9
  Jun 19, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  sio HARALI
   
 10. d

  decruca JF-Expert Member

  #10
  Jun 19, 2012
  Joined: Jun 18, 2012
  Messages: 295
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hapa mi sioni cha ajabu, hata wasipoongea na cm huwa wanapiga stori wenyewe kwa wenyewe huku hoja ikiendelea. na stori zinanoga hadi mtu anahama kiti chake anasogea kwa mwingine. wengine wanapiga usingizi tu kule mjengoni kipengele muhimu ni wakati wa kuandika majina kwa ajili ya sitting allowance,
   
Loading...