Hivi ni haki kuziba barabara ya mtaa kwa kifusi kwa zaidi ya wiki tatu

PgSoft2008

JF-Expert Member
May 15, 2008
264
73
Wapendwa,

Kufuatia shughuri zangu sasa niko Iringa na ninakaa mitaa furahi maeneo ya Wilolesi. Ni zaidi ya Wiki tatu sasa tangu lundo la kufusi kumwagwa katika barabara ya mtaa wetu kwa kisingizio cha mwenge na kutuzuia kabisa kufika nyumbani kwetu. tunalazimika kulaza magari mbali sana na kulipia gharama za ziada wakati tuna walinzi nyumbani na parking ya kutosha.

kwa jinsi kifusi kilivyomwagwa completely huwezi pitisha gari wala pikipiki nitaweka picha, mbaya zaidi hata upitaji kwa miguu pia ni mgumu na hakuna dalili ya kusambazwa leo wala kesho. watendaji wa mtaa wala hawana mpango wa kutoa taarifa na kwa nini wanakiacha hicho kifusi mpaka leo.

SIJUI KWA SABABU HUKU NI KIJIJINI.

nisaidieni kuwaambia wahusika wakumbuke labda hawajui kama ni kero.
 
Hao halmashauri wanafanya kazi kwa kusukumwa sukumwa labda watakuwa wametegeshea atakapo kuja mkubwa hapo IR waanze kazi si unajua tena viongozi wetu.Itapidi kuwasiliana na TANROADS kabisa wakichemka tuwekee picha kabisa.
 
Ni mtindo uliojitokeza sehemu mbalimbali hapa nchini. Mimi ni mkazi wa Manzese uzuri. Kuna barabara ya lami ipitayo Tandale Uzuri. Barabara hii ilikuwa na mashimo mengi sana. Kitu kilichofanyika ni kupanua yale mashimo lengo likiwa ni kuweka lami ili kuyaziba. Mpaka sasa karibu mwezi hakuna kilichofanyika. Tatizo kama lako la kuweka kifusi zaidi y awiki ni la kawaida sehemu nyingi nchini. Tatizo ni viongozi au watendaji wetu hawafanyi kazi kwa malengo. Badala ya kutatua tatizo wanaongeza ukubwa wa tatizo.
 
na huku dar walitufanyia mtindo huo huo huku mitaani kwetu ... tena walimwaga udongo wa mfinyanzi .. worst still kulikuwa na nvua ... tulikoma ... maana watu waliteleza mpaka .. halafu katika hali hiyo usilewe kabisa ...
 
Back
Top Bottom