Hivi ndivyo USA wanavyokwapua mafuta Syria

MakinikiA

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2017
Messages
2,045
Points
2,000

MakinikiA

JF-Expert Member
Joined Jun 7, 2017
2,045 2,000
Vita vya Syria: Ni nani anayenufaika na mafuta ya taifa hilo?


Visima vya mafuta karibu na mpaka kati ya Uturuki na Syria

Visima vya mafuta karibu na mpaka kati ya Uturuki na Syria


Rais Donald Trump anasema kwamba anatarajia Marekani itafaidika kwa kujipatia mamilioni ya madola kila mwezi kutokana na mapato ya mafuta ya Syria huku wanajeshi wa Marekani wakisalia nchini humo.

Rais wa Syria Bashar al-Assa amejibu akiishutumu Marekani kwa 'kuiba mafuta' kutoka katika taifa lake huku Urusi ambayo ni mshirika mkuu wa rais Assad akikitaja kitendo hicho kuwa ujambazi wa kimataifa.

Hivyo basi tunauliza ni nani haswa anayedhibiti mafuta ya Syria na ni nani haswa anayefaidika?


Donald Trmp

"We're keeping the oil, remember that. We want to keep the oil. Forty-five million dollars a month."Donald Trump - US President


Mataifa yenye uwezo mkubwa yanapigania udhibiti

Marekani ilitangaza kuondoka kwa vikosi vyake katika eneo la kaskazini mwa Syria mwezi Oktoba , lakini imesema kwamba itawabakisha takriban wanajeshi wake 500 ili kulinda visima vya mafuta , pamoja na vikosi vya Kikurdi ambavyo ndio vinavyofaidika na mafuta hayo.

Waziri wa ulinzi nchini humo Mark Esper amesema kuwa wanajeshi wa Marekani watasalia katika eneo hilo kulinda dhidi ya sio tu wapiganaji wa Islamic State bali pia wanajeshi wa Urusi pamoja na wale wa vikosi vya wapiganaji wanaoungwa mkono na serikali ya Syria.

Mataifa hayo mawili yalitia saini ushirikiano wa kawi wa 2018 kuipatia Moscow haki za kipekee kuimarisha sekta ya gesi na mafuta ya Syria.

Ni kutokana na hali hiyo ambapo rais Trump ametangaza maslahi yake ya kufaidika na mafuta hayo ambayo vikosi vyake vinayalinda.''It’s about money and it’s about oil....Of course we are angry, every Syrian is angry. This is looting.” Bashar al-Assad - Syrian President


Je, Syria inazalisha kiwango gani cha mafuta?

Sekta ya mafuta na gesi imekuwa ikitoa mchango mkubwa katika mapato ya serikali ya Syria , licha ya kwamba hifadhi zake za mafuta ni ndogo ikilinganishwa na mataifa mengine katika eneo la mashariki ya kati.

Mwaka 2018, Syria ilikuwa na takriban mapipa bilioni 2.5 ya mafuta , ikilinganishwa na Saudia iliokuwa na mapipa bilioni 297, Iran bilioni 155 na Iraq bilioni 147.

Visima hivyo vya mafuta viko katika mkoa wa Deir al- Zour mashariki mwa Syria karibu na mpaka wa Iraq na eneo la Hassakeh katika eneo la kaskazini mashariki. Lakini mafuta ya taifa hilo yamepungua tangu mzozo ulioanza 2011.

Mwaka 2008, Syria ilizalisha mapipa 406,000 ya mafuta kwa siku kulingana na takwimu za shirika la mafuta nchini Uingereza.

Mwaka 2011, kiwango cha mafuta kilishuka hadi mapipa 353,000 na kushuka zaidi hadi mapipa 24,000 kufikia 2018 ikiwa ni kiwango cha chini zaidi kwa zaidi ya asilimia 94.Syria oil production 2008 - 2018
canvas.png

Source: British Petroleum (BP)

Serikali ya Syria imepoteza udhibiti

Serikali ya Syria ilipoteza udhibiti wa eneo kubwa la visima vya mafuta vya taifa hilo kwa makundi ya upinzani na baadaye kwa wapiganaji wa Islamic State baada ya vita hivyo kushamiri.

Kufikia 2014 IS ilifanikiwa kuteka visima vingi vya mafuta mashariki mwa Syria ikiwemo kile cha al-Omar, huko Deir al Zour. Mauzo ya mafuta yalikuwa chanzo kikuu cha mapato yao wakijipatia takriban dola milioni 40 kwa mwezi 2015 kulingana na idara ya ulinzi nchini Marekani.

IS ilipoteza udhibiti wa visima vya mafuta vya Syria kwa vikosi vya Kikurdi vinavyoungwa mkono na Marekani baada ya wapiganaji hao wa Jihad kushindwa katika ngome yao ya mwisho mashariki.

Visima vya mafuta vya Syria vilikumbwa na uharibifu mkubwa kufuatia mashambulio ya Marekani katika lengo la kuliharibia kundi hilo chanzo chao cha kujipatia mapato.

Wapiganaji wa IS pia waliharibu miundo msingi ya mafuta hayo walipogundua kwamba visima hivyo vitatekwa na wapiganaji wa Kikurdi.

Vikosi vya Kikurdi bado vinaendelea kufaidika na mapato ya mafuta

Wapiganaji wa Kikurdi SDF walianza kuchukua udhibiti wa hifadhi kuu za mafuta kaskazini mashariki mwa Syria na katika eneo la mto Euphrates , kutoka kwa wapiganaji wa Islamic State 2017.

Kufikia sasa vimefanikiwa kurekebisha uharibifu uliofanyika na kuendeleza uzalishaji wa mafuta.
Naibu waziri wa ulinzi nchini Marekani Jonathan Hoffman hivi majuzi alinukuliwa akisema kwamba mapato ya mafuta hayo hayachukuliwi na Marekani bali SDF.

Wanajeshi wa Syria na washirika wake mashariki mwa Syria wanadhibiti takriban asilimia 70 ya mafuta ya Syria pamoja na hifadhi kadhaa za gesi , kulingana na Chales Lister, afisa mwandamizi katika taasisi ya mashariki ya kati.
Isipokuwa hifadhi hizo zinazalisha mafuta ya kiwango cha chini kabla ya vita hivyo kuzuka, hatahivyo anasema kwamba vinasalia kuwa chanzo kikubwa cha mapato ya SDF.

Ijapokuwa mashambulizi ya Uturuki kaskazini mwa Syria yamesababisha wapiganaji hao kupoteza maeneo kadhaa hifadhi nyingi za mafuta mashariki ya mto Euphrates yanasilia chini ya udhibiti wa SDF.


Mapato ya mafuta yamevisaidia sana vikosi vya Kikurdi

 

Forum statistics

Threads 1,381,428
Members 526,091
Posts 33,799,946
Top